Kumekua na malalamiko ya makada ambao wametangulia hapa Igunga kwa maandalizi ya Kampeni kwa kulipwa posho ya Tsh 30,000 kwa siku! Hapa Igunga lodge ya bei ya Chini ni 15,000! Kumekua na majibu ya hovyo kutoka kwa Ndugu Komu wa CDM hq kuwa kwa sasa kama mtu hana wito na CDM basi asishiriki kampeni hizo!
My take: Posho ya Tsh 30,000 haitoshi na inawapa wakati mgumu maafisa hawa ambao wana umhimu wa kuratibu kampeni! Kuna umhimu wa Katibu mkuu wa CDM kuingilia kati suala hili na kuipandisha posho hata kufikia 50,000 kwa kuzingatia kupanda kwa gharama za maisha!
kama watu waliingia kwenye chama kutegemea kunufaika binafsi hiyo inabidi wasahau,natumaini chadema itabidi ipigane sana na tabia ya watu wanaofikiria kuingia kwenye chama ili wanufaike zaidi,je wanachama ndo wanao toa michango yao kwa ajili ya kuendesha chama tena kwa kujitolea sasa kama mtu anahisi hawezi kuishi kwa hiyo tsh30000 ameenda kufanya nini huko,tena ashukuru kupewa hiyo tsh30000 mimi nafikiri ule wakati wa chama kuanza kuomba omba hela kwa wafanyabiashara ili kuendesha chama naomba chadema wasifike huko ndiko kutaua uhuru wa kuendesha chama kwa viongozi wa chama,wanachama tutajitolea wenyewe kwa michango au kwa hali{ kufanya kazi bila malipo}na mali{ fedha etc }kuweza kufikia uhuru tunaopigania kama mtu anahisi hawezi kupigania uhuru wake mpaka alipwe akae pembeni tu
,chama kitajengwa na wanachama watakakuwa na moyo bila kutegemea kulipwa fadhila tuondokane na uccm kuhisi chama kina fedha zinatoka wapi ,hela ya ruzuku itatumika kuendeshea chama kwa baadhi ya idara ambazo zimeajiri baada ya kuonekana ni muhimu kufanya hivyo au kwenye issue za dharura zinazotokea lakini sio kulipana posho ,je wangeambiwa wake kambini badala ya guest house je ingekuaje?