Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 16,352
- 22,963
Kwa maoni yako haya hukutaka uchaguzi ufanyike ?!. Au lengo ni nini, Magufuli asipingwe ?!.Kwanza kabisa me sio mpenzi wa vyama vya Siasa ila nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Tanzania. Nimefatilia mchakato mzima wa chama Cha Chadema na wote tumejua wagombea wa uraisi watakao chuana na Dr. John Magufuli niwe mkweli katika hai wagombea wote sijaona hata mmoja atakayepata kura kuanzia 40% kuendelea dhidi ya Magufuli, keep it in your mind.
Nimeona humu jamvini wapenzi wa Chadema wakiaminishana watashinda uchaguzi mkuu. Niwaambie kitu: Hakuna Jambo zuri kama kukubali hali halisi kuliko kujipa matumaini hewa.
Kuwa rais wa nchi sio jambo jepesi kama wanavyoaminishana wanaChadema. Kuna vitu vingi vinavyo determine mtu kuwa raisi Kama ifuatavyo:
1. Financial capability
Uwezo wa mgombea kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha au Chama kinachomsimamisha wa kufanya kampeni kwenye maeneo mengi ya Tanzania.Ukiangalia wagombea wa chadema hawana uwezo mkubwa wa kifedha. Lowassa aliweza kupata kura around 6 million; haikuja kwa urahisi ali-invest sana hela. Kwanza alinunua baadhi ya vipindi vya television ikiwemo ITV kuwafikia Watanzania wengi, ndio mgombea pekee aliyewahi kutokea wa upinzani ambaye aliyofanya kampeni maeneo mengi ya Tanzania n.k
2. Strong group support
Hapa tuna angalia makundi yenye nguvu Magufuli ana support kubwa ya viongozi wa dini zote na amecheza karata zake vizuri amejenga misikiti na amekuwa karibu Sana na viongozi wa kiislamu karibia shughuli zote pia ana support ya viongozi wa kikristo hata wale waliokuwa wanampinga sasa wapo upande wake kama mchungaji wangu Maksai wa kanisa la Korogwe huyu alikuwa ni Team Lowassa na alimpigia sana kampeni kanisani ila nowdays ni Team Magufuli na amekuwa anampaisha sana kanisani. Kuna Lusekelo, kuna Gwajima n.k Kuna magroup mengine ila naomba niishie hapo wakati Chadema haina mahusiano mazuri na viongozi wa dini.
3. 99.9% of artists support CCM
Wasanii wote wenye influence kubwa kwenye Jamii wanaisapoti CCM Kama vile Diamond and WCB in general ambao Wana wafuasi wengi sana kwa jina la "Team WCB" Kuna Alikiba, Harmonize, Mwana fa n.k
4. Kuwekeza kwenye majimbo aliyokosa kura
Hii Ni sababu itakayompa ushindi mnono Magufuli mf. Jimbo la Arumeru Arusha lilikuwa na tatizo sugu Sana la ukosefu wa Maji ila chini ya Magufuli ameleta mradi mkubwa wa Maji lakini pia walikuwa wanasumbuliwa na tatizo la Umeme tangu aingia Magufuli ameweza kupunguza tatizo la Umeme kwa kiasi kikubwa Sana. Kuimarisha usafiri wa treni Moshi, la tatu ni kuweka Dar kajenga flyover na miundombinu ya Barabara lakini uko kwetu kimara kulikuwa na tatizo maji kwa kiasi kikubwa na nikilio kikubwa kwa wakazi wa Ubongo, Kimara na Mbezi Magufuli amelitatua kwanza kwa kuaweka mabomba maeneo yote bure na wanatoa maji karibia wiki nzima. Suala mgao wa Umeme ulikuwa unaboa Sana na ilikuwa Ni tatizo kuu sana kwa dar ila now day inaweza kuchukua miezi hata 6 Umeme usikatike na hata ukikatika unarudi mapema tofauti na kipindi Cha nyuma.
NB: Kama nilivyotoa analysis yangu kwa kifupi Chadema hata kupata Asimilia 40 ya kura itakuwa ngumu kupata huo ndio ukweli wenyewe.Na bahati nzuri nyuzi zinabaki humu Kama kumbukumbu tutajionea.
Nimewauliza wanaccm wengi swali hili; kwanini mnaichagua ccm? majibu yake ni yale yale kama yakwako; Hakuna sababu ya msingi...ni hatari.Mzee hapa nimechambua kutokana na siasa ilivyo sio kwasababu ya hisia zangu hatuwezi kumezeshana uongo wahati ukweli unaonekana.Kuhusu kupenda au kutopenda kwa CCM kuendelea madarakani nazani hiyo ipo kwa wafia chama hata hao chadema unao wahabudu sioni wanatofautiana Nini na CCM
Magufuli alipata nguvu kwa sababu ya ndio alikuwa mgombea mkuu wa CCM pili baada ya makosa mengi aliyofanya Lowassa baada ya kuwa akipiga kampeni dakika 5 karibia maeneo mengi pia kuchafuliwa kwa kashifa ya ufisadi.Kwa maoni yako haya hukutaka uchaguzi ufanyike ?!. Au lengo ni nini, Magufuli asipingwe ?!.
Nikukumbushe kitu kimoja . Wakati Magufuli anachukuwa fomu za kuomba kazi aliyonayo Leo, hakuwa na nguvu kama kina Lowassa, Membe na hata Sitta. Lakini leo ni Rais na si hao waliokuwa ma giants.
Kitu muhimu ungesema tume tulionayo si tume huru ya uchaguzi . Lakini ukisema swala la kukubalika, huwezi kujiamini mambo ya kura za siri.
Sitakuja kupenda chama chochote Cha siasa Cha Tanzania by any means atanikikuuliza wewe kwanini unakipenda chama Cha Chadema wewe ujanijibu Nini?Nimewauliza wanaccm wengi swali hili; kwanini mnaichagua ccm? majibu yake ni yale yale kama yakwako; Hakuna sababu ya msingi...ni hatari.
Nataka madiliko baada ya miaka 60 ya ccm. Nchi zilizoendelea zote ambazo tunawapigia magoti kuomba hela wanabadilisha chama kila baada ya miaka 4 au 8. Na sisi tunashangaa kwanini tunawakimbilia kuomba hela; tunapenda hela yao lakini hatupendi wanachofanya kupata hela hiyo.Sitakuja kupenda chama chochote Cha siasa Cha Tanzania by any means atanikikuuliza wewe kwanini unakipenda chama Cha Chadema wewe ujanijibu Nini?
Nimekuuliza sasa lengo lako ni nini ?! Hutaki apingwe kwenye uchaguzi ?!. Au ulitaka chama gani kimuwekee mgombea wa kumpinga !!Magufuli alipata nguvu kwa sababu ya ndio alikuwa mgombea mkuu wa CCM pili baada ya makosa mengi aliyofanya Lowassa baada ya kuwa akipiga kampeni dakika 5 karibia maeneo mengi pia kuchafuliwa kwa kashifa ya ufisadi.
Mimi nimemuuliza mara mbili swali hilo bado hajajibu anakuja na theories zake za kilumumba lumumba.Nimekuuliza sasa lengo lako ni nini ?! Hutaki apingwe kwenye uchaguzi ?!. Au ulitaka chama gani kimuwekee mgombea wa kumpinga !!
Nashangaa unaniuliza swali la kipuuzi Kama Hili au kichwa nikigumu kuelewa kusoma kote thread yangu na umeshindwa kujua Nini nimelenga any way nilichoandika hapo Ni mtazamo au maono yangu ya uchaguzi wa mwaka Huu.Nimekuuliza sasa lengo lako ni nini ?! Hutaki apingwe kwenye uchaguzi ?!. Au ulitaka chama gani kimuwekee mgombea wa kumpinga !!
Je unavyoona wewe Chadema ndio itaisaidia hii iwe Tajiri?Nataka madiliko baada ya miaka 60 ya ccm. Nchi zilizoendelea zote ambazo tunawapigia magoti kuomba hela wanabadilisha chama kila baada ya miaka 4 au 8. Na sisi tunashangaa kwanini tunawakimbilia kuomba hela; tunapenda hela yao lakini hatupendi wanachofanya kupata hela hiyo.
Ndio maana yake.Je unavyoona wewe Chadema ndio itaisaidia hii iwe Tajiri?
Niambie Ni kwanini?Ndio maana yake.
Mfumo wa ccm ni wa zamani tangu mwaka 1954. Watu wengi waliokulia kwenye mfumo huu walikuwa na lengo la kupigania uhuru wa nchi miaka ya 1960. Wengi chini ya Nyerere walikuja kuwa wajamaa. Huu ni mfumo maskini sana na mataifa waliyochukua mfumo huu walijikuta wakiwa maskini wakubwa e.g. Msumbiji, na nchi kadhaa za America ya Kusini.Niambie Ni kwanini?
Naona umemezeeshwa propaganda Sana unaweza ukawa ukipendi Chams Cha CCM ila chadema ni kibovu kuliko hata CCM yenyewe tangu lini chadema wanajua uchumi? Lakini pia akina demokrasia Kama Ccm hiv umewahi kuona hata ilani ya CHADEMA? Ebu kuwa serious.Mfumo wa ccm ni wa zamani tangu mwaka 1954. Watu wengi waliokulia kwenye mfumo huu walikuwa na lengo la kupigania uhuru wa nchi miaka ya 1960. Wengi chini ya Nyerere walikuja kuwa wajamaa. Huu ni mfumo maskini sana na mataifa waliyochukua mfumo huu walijikuta wakiwa maskini wakubwa e.g. Msumbiji, na nchi kadhaa za America ya Kusini.
Watu hawa kwenye mfumo wa ccm wamejenga himaya au genge lenye lengo la kujilinda wao wenyewe. Ukiwaunga mkono wanakupa nafasi kwenye genge lao. Wamezoea kutawala na kupata fedha kirahisi kwa njia ya madili ya serikalini. Hawajui biashara wala hawana ujuzi wa mikakati mbalimbali. Hawajui namna ya kujituma na kufanya kazi kwa maarifa, wamezoea kufanya mambo ili mradi wao wanafaidika haijalishi.
Ona jinsi viwanda vyote walivyoacha wakoloni vilivyokufa chini ya Mwalimu. Ona mashirika mbalimbali yaliyokuwepo, ni mengi sana siyataji hapa yalivyokufa, shirika la ndege, shirika la meli, mashamba ya mkonge, kahawa, hata korosho ona zinavyokosa soko, tumbaku, n.k. Watu kama akina Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli, hawajawahi kufanya biashara na hawajui biashara, unafikiri mtu kama huyu atasimamia mgawanyo mzuri wa dili au mkataba wa madini? Kenya marais waliopita walikuwa watu wenye mashamba makubwa, mahoteli n.k, wanajua uchumi ni nini.
Chadema ina watu wanaojua uchumi na wao wenyewe wamewahi kufanya kazi nje ya siasa sio kama wana ccm ambao ni watu wa mtandao wa ccm tangu kuzaliwa wanapiga siasa tu. Usitegemee mtu huyo aweze kuleta mabadiliko na kunyanyua kilimo na biashara nchini, atakuwa mtu wa kukwapua tu vilivyo tayari mezani. Ndivyo walivyo ccm na hivyo tunahitaji akili mpya.
Wewe ni m CCM kindakindaki. mnafahamika kwa kujivunia na kuusifu u dictator wa Jiwe, badala ya kuuonea haya.Kwanza kabisa me sio mpenzi wa vyama vya Siasa ila nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Tanzania.
Mzee una ushabiki maandaziWewe ni m CCM kindakindaki. mnafahamika kwa kujivunia na kuusifu u dictator wa Jiwe, badala ya kuuonea haya.
Miaka minne bila ya chembe ya aibu, wengine mmewazuiwa kufanya siasa, lakini bado mnawaogopa.
Mnajijua pamoja na makelele na vitisho vyote, hamjaweza kugusa nyoyo za waTZ, 90% ya mnayofanya sio mahitaji yao ni yenu na mikogo yenu.
Kiburi chenu chatokana na tegemeo la kubebwa na walofaidika na teuzi na matumizi ovu ya vyombo vya dola.
Kama mwana ambae amekuwa akiandamwa na kuonewa na wazazi wake,mwaka huu HATUOGOPI tena.
40% ni mbali sana... 17%watajikamua sana.Umeandika mambo mengi wakati huwa mnapata msaada toka kwa Tume feki ya uchaguzi, na jeshi la polisi; hayo yote uliyoandika hayana maana.