CHADEMA, wanaharakati kupima mabavu ya dola | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, wanaharakati kupima mabavu ya dola

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 17, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Muswada wa Katiba mpya


  Waandishi Wetu


  [​IMG]  Viongozi wa CHADEMA kwenye maandamano


  HALI ya kujaribu kupimana ubavu kati ya vyombo vya dola na baadhi ya wanasiasa, wakiwamo wabunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadhi ya wanaharakati, kupitia Jukwaa la Katiba, kwa sasa ni dhahiri, Raia Mwema, limejiridhisha.

  Kusomwa kwa mara ya pili kwa Muswada wa Mabadiliko ya Katiba kulikofanywa na Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, bungeni wiki hii, na uamuzi wa wabunge wa CHADEMA, kususia kushiriki mjadala wa muswada huo bungeni, ni matukio yanayobainisha mvutano huo wa dhahiri, wenye mwelekeo wa kupimana ubavu.

  Lakini wakati hali hiyo ikijitokeza, Raia Mwema, imepewa taarifa kuwa wapo baadhi ya Watanzania wamejiandaa kufikisha suala hili katika Mahakama, kupinga muswada wa sasa wa mabadiliko ya Katiba kuendelea na hatua nyingine zinazofuatiwa ikiwa ni pamoja na kutiwa saini ili uwe rasmi sheria.


  "Tunakwenda kupinga muswada huu katika Mahakama, ikibidi kuzuia kabisa mchakato huu hadi pale Serikali itakapokuwa tayari kuanza upya. Lengo letu ni kuweka mazingira ya usawa katika kufikia Katiba mpya," alisema mwanasiasa mmoja ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwenye msimamo mkali.


  Tangu kuanza kwa vikao vya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, siku kadhaa kabla ya kuanza kwa mkutano wa sasa wa Bunge, mjini Dodoma, dalili za mvutano huu zilianza kujitokeza na msingi wa hoja ukiwa madaraka makubwa ya Rais, katika muswada huo.


  Kati ya watu walioko kwenye orodha ya kutilia shaka madaraka hayo makubwa ya Rais katika muswada huo ni pamoja na wengine ambao si wanasiasa wala wanaharakati, bali ni wanataalamu wa sheria, wakiwamo wanasheria kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).


  Baadhi ya hao wamependekeza kuwa katika muswada huo, Rais asipewe jukumu la kupendekeza au kutunga hadidu za rejea na kwamba hadidu hizo ziwekwe moja kwa moja ndani ya muswada, ili kuondoa uwezekano wa kuzalishwa kwa Katiba yenye kukidhi utashi binafsi wa Rais ambao unaweza kupandikizwa kupitia fursa anayopewa ya kutunga hadidu za rejea.


  Hata hivyo, kwa upande wake, Serikali imekuwa ikijieleza kuzingatia maoni hayo ya wadau mbalimbali na kutahadharisha kuwa si maoni yote yaliyozingatiwa. Baadhi ya wabunge pia wamependekeza hadidu hizo rejea asiachwe Rais kuzitunga.


  Ni kutokana na mapendekezo hayo na mengine, shinikizo linajengwa kuwa ni lazima muswada huo usomwe kwa mara ya kwanza ili kuwapa nafasi zaidi Watanzania kuongezea maoni yao.


  Lakini hali inazidi kuwa tete kwa sasa kutokana na Serikali kuendelea kuchukua msimamo wa kusoma kwa mara ya pili muswada huo, kinyume cha matakwa ya baadhi ya wanaharakati na wabunge wa CHADEMA, ambao wanataka usomwe kwa mara ya kwanza kwa sababu haukushirikisha wananchi kwa kiasi cha kutosha.


  Kwa upande mwingine, taarifa zilizolifikia gazeti hili ambazo pia zimebainishwa na Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, muswada huu unapopitishwa na Bunge, kuna maombo maalumu yaliyowasilishwa kwa Rais Kikwete, ili kwanza kabla ya kufikishwa kwake kwa ajili ya kutiwa saini, utapelekwa tena kwa Watanzania, ili kuoongezea nguvu.


  Wanaharakati wanaoungana na wabunge wa CHADEMA kuwa na msimamo unaofanana ni pamoja na wanaoujumishwa katika Jukwaa la Katiba.


  Jana Jumanne, wabunge wa CHADEMA walikutana kuweka msimamo wa pamoja, na kati ya malengo yao yatakayofuata ni kuungana na wanaharakati wengine kufanya maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima, hali inayoviweka katika tahadhari vyombo vya dola nchini.


  Katika kile kinachotajwa kuwa ni hali ya mvutano na kutazamana kwa hadhari kubwa, kati ya wanasiasa na vyombo vya dola, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Saidi Mwema, ameweka bayana kuwa jeshi hilo halitavumilia hali yoyote ya uvunjifu wa amani.


  "Moja ya jukumu la polisi popote duniani ni kuhakikisha usalama na amani pamoja na kulinda maisha ya raia na mali zao. Ili Jeshi la Polisi lifanikishe jukumu lake hili, ni muhimu sana kwa raia kuenzi amani na usalama uliopo nchini.


  "Sababu ya msingi ya raia kuenzi amani, usalama na utulivu uliopo nchini ni rahisi kuona kwa sababu; amani ya nchi ikiharibika ni kama mfano wa chombo kinachozama baharini, hakuna anayepona, wote wanakwenda na maji. Ikiwepo bahati, ni wachache tu wanaonusurika.


  "Itakuwa si hekima kwa nchi yetu kuona sheria inavunjwa na watu wachache, kwa kisingizio cha siasa, hasira kali ama jazba bila kuchukuliwa hatua. Shughuli za siasa ni kitu kimoja na fujo ama vurugu za jazba ni kitu kingine.


  "Upo umuhimu wa kutenganisha mambo hayo mawili na hapana budi mamlaka za kisheria ziheshimiwe na watu wote bila kujali itikadi zao kisiasa au kijamii.


  "Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walipitisha sheria ya vyama vya siasa na sheria ya Jeshi la Polisi, sheria hizo zimeweka utaratibu na miongozo ya kufuata katika kuratibu mikusanyiko mbalimbali ikiwamo maandamano na mikutano ya hadhara.


  "Haki, wajibu na utaratibu wa kufuatwa na vyama vya siasa pamoja na Jeshi la Polisi kupewa taarifa ya mikusanyiko imefafanuliwa pia katika sheria hizo. Kwa hali hiyo ifahamike wazi kwamba Jeshi la Polisi halina nia mbaya ya kuzuia mikusanyiko ama maandamano," awesema IGP Mwema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.


  Tayari baadhi ya maeneo ya miji mikuu na yenye ushawishi wa kisiasa yamekumbwa na vurugu kubwa zilizoisukuma Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, kutoa tamko Bungeni kuelezea hali hiyo, ambayo inazidi kuashiria kuwapo kwa vuguvugu kali dhidi ya serikali.
   
 2. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwandishi alitaka kutufikishia ujumbe wa mwema. Hamna kitu hapa. Hili gazeti siku hizi!!
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  utumbo mtupu...
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KATIBA MPYA NCHINI BILA CCM INAWEZEKANA!!

  CHADEMA pamoja na Wanaharakati wote nchini, tunahitaji kukusanya sahihi milioni 1 ya wananchi wenye umri wa ya miaka 18 na zaidi na kutufanyakufanya maamuzi mazito kama vile kutupilia mbali maamuzi yoyote ya bunge kumhodhisha Rais Kikwete (mtumishi namba moja wa katiba) kujipa mamlaka ya kujimilikisha haki ya umma kujitengenezea katiba mpya bila udalali maana katiba si mali ya ikulu wala bunge bali hivyo vyombo viwili ni uzao tu wa katiba.

  Naomba nirudie, wenye katiba ni sisi wananchi tutakaotilia sahihi maamuzi kama hayo hapo juu. Najua wanasheria ndani ya CCM wanajua fika maana ya hatua hii pindi tukifika mbele ya chombo chochote huru chenye maamuzi kisheria ama kitaifa au kimataifa.

  Na kwa njia hiyo hiyo, vile vile UWEZO TUNAO wa kujikusanyia maoni juu ya utaratibu upi utumike kupatikana kwa katiba mpya na hivyo hizo hizo sahihi hizo zaidi ya watu milioni 1 ikafanya maoni hayo yakawa ni
  Authoritative Dacument inayoruhusu mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya kuendelea hata bila ya wale ambao wanapendelea kutumia udalali wa ikulu kwenye zoezi zimakwemo.

  Hadidu za rejea nazo zikakusanywa na kupitishwa na idadi kama hiyo hiyo ya sahihi milioni 1 na mchakato kuendelea kama kawaida bila zengwe. Hebu tufikiri mbele zaidi na tufikiri nje kabisa ya mifuniko ya mdau mmojawapo tu wa Baraza la Katiba Taifa aitwaye CCM.
   
 5. T

  Tyane New Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm nikama wamekosa hoja za kuzungumzia kila mp akikamata kipaza sauti ni chadema wasijue ndo wanazidi kujipalia makaa
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ZIBA SANA TUNDU LA HEWA SAFI YA 'KATIBA MPYA BILA UDALALI' TUFE NA WEWE!!

  Siku si nyingi sana siasa za KATIBA MPYA nchini kupanda daraja nyingine kabisa usiotarajiwa endapo MAWAZO MGANDO NA HOFU YA BAADHI YA WATAWALA hayatapitisha Nguvu ya Umma kusikika matakwa yake.

  Haya malalamiko mengi nchini, ufisadi serikalini, umasikini wa kutwishwa, ukatili wa vyombo vya dola na mauaji holela ya raia kila kukicha yote majibu yake ni KATIBA MPYA bila udalali nchini.

  Tanzania kwa sasa unyeti wa swala la KATIBA MPYA na wale wenye kuweka vizuizi vingi njiani, kwetu sisi wananchi ni tunawaona sawa tu na mtu yeyote yule ambaye anajaribu kutuzibia hata ka-tundu pekee la kuingizia hewa shimoni mithili.

  Watanzania kwa mahitaji yetu ya KATIBA MPYA BILA UDALALI hatuna tofauti kbisa na hali aliyokua nayo Saddam Hussein na kuhitaji kwake hewa shimoni wakati akijificha Wa-Marekani wasimtie nguvuni.

  Endelea kuziba tundu pekee la hewa safi ya KATIBA MPYA BILA UDALALI na wananchi tufe na wewe bila ajizi!!
   
 7. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,178
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu sisi tuendelee na mijadala ya namna ya kupata katiba inayo kidhi, waacheni ccm waijadili cdm kwa katiba haimo kwny ilani yao!
   
 8. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hakuna ki2 hapo! Uharo tu!
   
Loading...