Mishahara haitoshi? Hivi ushajiuliza wa Tanzania wangapi wanalipa kodi ipasavyo? Sasa chukuwa kodi inayolipwa kwa sasa halafu igawe kwenye hiyo mishahara uitakayo halafu uone zinabaki kiasi gani za kuliendesha taifa.
Nna uhakika njia mbadala zinazobuniwa na Serikali, kama vituo vya veta, kilimo kwanza, kuhamasisha ujasiriamali ndiko suluhisho la mishahara midogo.
Hivi hata ukiingia mitaani ndio mshahara utapanda? Unaweza ukapandishiwa mshahara wa kiini macho, yaani mshahara upande na thamani ya fedha ishuke sana na iwe afadhali ya huo mshahara mdogo kuliko kuwa na mipesa mingi isiyo na faida.
Hivi leo tunaona jitihada za Serikali kwa kuanzisha benki za wakulima, mortgage, pembejeo, mabara-bara, mashule, veta na kadhalika. Mambo hayo yote yanalenga kustimulate uchumi, na ndio njia ya kukuza kipato.
Usijidanganye kuwa kuingia mitaani ndio suluhisho, hasara zake ni kubwa kuliko unavyofikiria.