CHADEMA wamkana Zitto

CHADEMA wamkana Zitto

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kimewasilisha taarifa zake za fedha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12.

Kwamba, hilo linathibitishwa na barua ya Msajili wa Vyama yenye kumb. Na CDA.112/123/01a/37 ya Septemba 4, 2012, iliyopelekwa kwa makatibu wakuu wa vyama vyote vya siasa.

Uthibitisho huo umetolewa kukanusha taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, iliyosema kuwa vyama vya siasa vinavyopata ruzuku kutoka serikalini havijawasilisha taarifa yake ya mapato na matumizi kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana huku akionesha nyaraka za vielelezo, Katibu wa Baraza la Wadhamini wa CHADEMA, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Anthony Komu, alisema wamesikitishwa na taarifa ya PAC.

Alisema kuwa wameamua kuchukua jukumu la kuufahamisha umma kuwa wapo tayari kutoa ushirikiano wa dhati ili sheria hiyo ifanye kazi yake kwani tangu itungwe mwaka 1992 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2009, CHADEMA kimekuwa kikifuata utaratibu kama ulivyoelekeza.

Komu alisisitiza kuwa taarifa za PAC si sahihi na hazina ukweli wowote kuhusiana na CHADEMA labda kwa vyama vingine.
Alifafanua kuwa hesabu za mwaka wa fedha zilizokaguliwa za 2009/2010, CHADEMA kiliwasilisha kwa msajili kwa barua yenye kumb. C/HQ/ADM/MSJ/04/71 ya Oktoba 2011.

Komu alionesha barua ya Msajili wa Vyama ya Septemba 4, 2012, ambayo ilionesha vyama vilivyowasilisha hesabu zilizokaguliwa kwake kuwa ni CHADEMA na NCCR-Mageuzi tu.

Kwa mujibu wa barua hiyo, CUF waliwasilisha hesabu kwa msajili bila kukaguliwa. Vyama ambavyo havikuwasilisha hesabu zao kabisa ni CCM, TLP, APPT- Maendeleo, UDP na DP.

Komu alifafanua kuwa taarifa ya fedha iliyokaguliwa kwa mwaka huu 2012/2013 bado hawajaiwasilisha kwenye ofisi ya msajili.
Alisema hatua hiyo ni baada ya ofisi ya msajili yenyewe kutoa maelekezo kwa barua yenye kumb. Na. DA.112/123/16A/97 ya Novemba 26, 2012.

"Tumefanya mawasiliano na CAG kwa ufafanuzi wa jambo hili na tutawafahamisha ipasavyo kuhusu malipo/gharama mliyotakiwa kulipa katika ukaguzi wa mahesabu hayo," ilisomeka barua hiyo ya msajili.

Hadi jana wakati CHADEMA wanatoa utetezi huo, Komu alisema ofisi ya msajili ilikuwa haijatuma hata mkaguzi au maelekezo yoyote kama walivyoelekezwa walipe kiasi gani na wapi kwa kazi ya ukaguzi wa hesabu za mwaka 2012/2013.

Komu aliilaumu PAC kujitokeza hadharani kuzungumza mambo mazito pasipokuwa na ushahidi wala kuwashirikisha wahusika ambavyo ni vyama vya siasa, badala yake ikajumuishwa na CHADEMA katika kapu hilo.

"CHADEMA tuna hadhi yetu, ni chama makini, hatuachi mambo yaende yalivyo, ndiyo maana kuliko kuanza kujibizana na mtu mmoja mmoja katika simu, tumewaita waandishi ili kutoa taarifa hii kwa umma kuwa taarifa ya PAC si sahihi," alisema.

Alisisitiza kuwa kama kweli tangu mwaka 2009 hesabu hazijakaguliwa, basi aulizwe CAG, ofisi yake inafanya nini ikiwa fedha zinatolewa mwaka wa kwanza hazikaguliwi hadi mwaka wa nne.

"Ofisi ya CAG ituambie wanafanya kazi gani, kwanini wanaendelea kutoa ruzuku kama hesabu hazikaguliwi?
"Sisi CHADEMA tuko wazi, tunapopata hata misaada kutoka nje huwa tunamuarifu msajili, maana yake ni hatari kama chama kinapokea misaada hakisemi kwa msajili," alisema.

Komu aliongeza kuwa chama kinaweza kupokea hata misaada ya Al- Shabaab au mambo mengine kama ya EPA, ndiyo maana wanawataka PAC waende mbele zaidi ili utaratibu wa uwazi uende kwenye vyama vyote kama wanavyofanya CHADEMA.

"Tulipata fedha kutoka Denmark ukiwa msaada kwa ajili ya kujenga uwezo, tulimwandikia msajili, naye akatujibu kwa barua Na. DA/112/123/16a/10 ya tarehe 19, Agosti 2013.

"Tunashukuru kwa taarifa hii ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa," ilisomeka barua hiyo.

Juzi, vyama vya CCM, CUF na NCCR-Mageuzi navyo vilimjia juu Zitto vikidai anatafuta umaarufu, kwani hesabu zao zimekaguliwa.

Zitto aitisha CHADEMA

Zitto alisema anayo mamlaka kama mwenyekiti wa kamati hiyo kuwafunga jela wote wanaoendeleza malumbano hayo ilhali agizo lilishatolewa, na kusema kuwa hilo ni onyo kwa CHADEMA na CCM, aliodai ni vinara wa malumbano.

"Mimi sifanyi siasa hapa, natekeleza jukumu langu kama mwenyekiti wa kamati, kwa hiyo hili ni onyo kwao, nipo tayari kunyongwa nikitetea masilahi ya umma," alisema.

Alieleza kuwa ni vema vyama hivyo vikapeleka ripoti kwa msajili na kuachana na malumbano yasiyo na tija, huku akiwashukia waliokuwa wakidai kuwa anatafuta umaarufu kwa maelezo kuwa tayari ni maarufu.


Source: Tanzania Daima Ijumaa
 
Kama hii taarifa ya Bw. Anthony Komu ni sahihi basi Zitto Kabwe atakuwa ana matatizo makubwa sana kwenye ubongo wake. Kwamba haelewei haya ndani ya chama chake hadi kukiingiza kwenye kapu la kutaka kikatiwe ruzuku? Vipi kwa NCCR Mageuzi ambao nao taarifa za ukaguzi wake zinaonekana kufika kwa CAG na msajili wa vyama? Right, inawezekana analenga kile anachokiita maslahi ya taifa lakini hata kutaka kujiridhisha kwa taarifa anashindwa?
 
Hivi zile za USWISS zimeshakaguliwa? Hvi ameshawaita wahusika wakajieleza mbele ya kamati yake? Mbona aliahidi kutupatia majina yahao walioficha hzo hela huko lkn mpaka sasa kimya? Je nikwamba Zitto kashapewa10% akatulia? Je zitto anayoyaongelea ataweza kuyasimamia na kuyatekeleza?
 
Zitto naye ni kutafuta attention tu,

Kwa wahasibu mnajua, kuwasilisha ni utaratibu tu, pesa ilishaliwa hakuna kitu PAC inaweza kufanya. Kwani waliwahi kufanya nini kwa pesa iliyokwisha liwa? Basi tu na yeye apate makaratasi ya kupitia na kupiga kelele.

Pesa ya serikali bora umefuata taratibu wahusika wamesaini basi, mambo ya ilifanya nini na kwa nini huwa hakuna.
Mtu kazi anafanya masaa 3 anaandika kafanya kwa siku 10 na mabosi wanasaini. Kiutaratibu hakuna kosa, PAC watapewa makaratasi bac!!
 
Zitto ni mnafki. Period.

Yeye ni sehemu ya uongozi Chadema licha ya kwamba anaongea kwa niaba ya kamati ya PAC lakini ana uwezo wa kuwasiliana na viongozi wenzake internal. Huyu jamaa bichwa lilishamvimbaga kwa kutafuta sifa za kijinga ila kwa hili amejikaanga mwenyewe na kila mwenye akili timamu sasa anafahamu fika Zitto ameamuwa kupigana vita ya makundi ndani ya Chadema kwa kuitumia kamati ya PAC.

Vita hii haiwezi kwani atakuwa defeated tu, anajaribu kudivert akili za wajinga kutoka kwenye hoja kuu ya katiba mpya.

Nb: Eti kamati yenyewe ya PAC makamu mwenyekiti ni Aden Rage Al shabaab mwizi aliyewahi kufungwa jela kwa wizi wa pesa za FAT.

Nimeshangaa sana huyu kwanza akakamilishe ukaguzi wa hesabu za Simba pale Msimbazi na akabidhi pesa za Okwi.
 
Tunaomba na ile misaada Zitto anayopewa na wananchi kila siku kwenye mikutano yake atupe mrejesho na kama zimeshakaguliwa na CAG.
 
huyo siyo Zitto wa chadema,huyo ni Zitto wa POAC, akitoka huko poac atajiunga na wenzake kuilaani vikali kauli hiyo ya poac na Mwenyekiti wao,kama alikuwa akisoma mahali wakati anaongea maneno hayo basi ntajua huo ni ujumbe kutoka kwa Wassira na siyo wake(Zitto)
 
Maneno mengi ya nini. Kama ripoti ipo si kupeleka tu ukiambatanisha na barua iliyokubali kupokea na kufanyiwa kazi kwa riooti husika!!!!!!???????

Halafu kwa nini anachukuliwa personally wakati ni mwenyekiti wa kamati????!!!!!
 
Zitto aligongelea msumali wa mot0 kwa wapiga dili ndani ya vyama ndio maana waona povu jingi lawatoka hapa.
 
Naona hapa kuna mtu anatafutwa.Sina uhakika kwa sababu mimi ni mtaalam wa kukagua Local Government,ivi ni nani mwny jukumu la kukagua,ni CAG au chama!Zito angetueleza kama CAG alienda CDM akanyimwa nyaraka,limitation of scope


CAG anatakiwa azifuate au vyama vinatakiwa vipeleke?????!!!!!

Watu wanatafutwa kila siku na ndio kazi ya taratibu na kanuni achilia mbali sheria zooote ni kumulika wazembe!!!!!!

Attendance register pia inatafuta mtu anayeitwa mchelewaji,au kazi yake nini?????!!!!!!
 
Zitto naye ni kutafuta attention tu,

Kwa wahasibu mnajua, kuwasilisha ni utaratibu tu, pesa ilishaliwa hakuna kitu PAC inaweza kufanya. Kwani waliwahi kufanya nini kwa pesa iliyokwisha liwa? Basi tu na yeye apate makaratasi ya kupitia na kupiga kelele.

Pesa ya serikali bora umefuata taratibu wahusika wamesaini basi, mambo ya ilifanya nini na kwa nini huwa hakuna.
Mtu kazi anafanya masaa 3 anaandika kafanya kwa siku 10 na mabosi wanasaini. Kiutaratibu hakuna kosa, PAC watapewa makaratasi bac!!

Kakuambia tayari yeye ni maarufu hiyo attention itamsaidia nini? Sema kijana anatishia ulaji wa wanasaccoss wenu wa chadema.
 
Zitto ni mnafki. Period.

Yeye ni sehemu ya uongozi Chadema licha ya kwamba anaongea kwa niaba ya kamati ya PAC lakini ana uwezo wa kuwasiliana na viongozi wenzake internal. Huyu jamaa bichwa lilishamvimbaga kwa kutafuta sifa za kijinga ila kwa hili amejikaanga mwenyewe na kila mwenye akili timamu sasa anafahamu fika Zitto ameamuwa kupigana vita ya makundi ndani ya Chadema kwa kuitumia kamati ya PAC.

Vita hii haiwezi kwani atakuwa defeated tu, anajaribu kudivert akili za wajinga kutoka kwenye hoja kuu ya katiba mpya.

Nb: Eti kamati yenyewe ya PAC makamu mwenyekiti ni Aden Rage Al shabaab mwizi aliyewahi kufungwa jela kwa wizi wa pesa za FAT.

Nimeshangaa sana huyu kwanza akakamilishe ukaguzi wa hesabu za Simba pale Msimbazi na akabidhi pesa za Okwi.

Kiongozi hilo nalo neno. Zitto kiongozi wa ngazi ya juu sana ndani ya CDM lakini inanishangaza kuona kama hajui hata hesabu za chama chake kama zimeshakaguliwa. Huo ni unafiki wa hali ya juu sana.
 
Back
Top Bottom