CHADEMA wamfungulia kesi Nape

Napenda sana haya mambo kwasababu yanafanya maisha yawe mapya kila siku. Kwenye nchi yenye matatizo kama hii, ni sinema za namna hii tu zinazoweza angalau kupunguza machungu ya maisha.

Hakika umenena Radhia Sweety
 

Hivi ile kesi ya Uchaguzi mdogo wa Igunga ilisimamiwa na Mahakama gani vile? Wewe inaonekana hujui hata ulisemalo! Maneno ya Tundu Lissu kuhusu Mahakama zetu na Majaji wake haiwezi kuzuia Haki za msingi za chama au Mwana-CDM yeyote.Hatuwezi kuwekewa Majaji kwenye Mahakama zetu ambao hawawezi kuamua kesi yoyote au kama wakitoa uamuzi ni kwa maelekezo ya Kiongozi fulani wa CCM au Serikali yake. Tunataka utawala wa sheria na siyo sharia!

Tundu Lissu alizungumza ukweli na ushahidi uko kwenye maandishi ukiwa umeandikwa na Majaji hao hao ambao hawakubalini na uteuzi wa kijinga unaoangalia udini,ukoo,ukabila na urafiki! Uteuzi wa aina hii unaofanywa na rais wako Kiwete unaenda kwa mfumo huo na kwa maana hiyo uteuzi huo hauna tija kwa Taifa sana sana unazidi migogoro na migongano ya kiutawala.
 
huyo mnyiramba nape a.k.a napegwa anatudhalilisha siye wanyiramba kwanini lakini?wote hata huyu nchemba madelu wanatia aibu.eti majesh yameapa kukilinda chama cha mapinduzi,mh haya,
 
Yes! very nice move, now we will be able to see who is telling the truth.
 
Hata kama jaji akipendelea ni ngumu kwani cdm kuna mawakili bingwa sana, Marando, Lisu, profesa safari watakoma!
 
Endelea kuhara hapa ccm ni full aibu kotekote,mmeanzisha operesheni yenu ya kuua raia na kuisingizia chadema mkitegemea wananchi watawa support,raia wakawashtukia,waandishi nao wamewageuzia kibao,waalimu hawawataki,ma doctors ndio kabisaa sasa mmemtelekeza nape awabebee madhambi yenu,mwaka huu kazi mnayo.
 
Afadhali huyu kibaraka ajibu hizo tuhuma zake mbele ya pilato. Maana anafanya siasa za propaganda bila kuelewa dunia ya sasa ni ya utandawazi (siyo ufunga siri). Inabidi athibitishe kauli yake. Na kama anamtegemea JK amekwisha, ajaribu kukumbuka na kujikumbusha juu ya Mgosi (baba Januari) alivyokuwa mropokaji na JK alimshangaa mpaka akamkatalia kwenda kuongea na maaskofu (alimwambia, yaani wewe ukienda mropokaji hivyo.....).
 
huyu nape anapenda sana umaarufu, ila njia anazotumia zinamgarim.
Hazimgharimu yeye mkuu!zinakigharimu chama chake,nape hana anachopoteza so far,mwenyekiti wake alimkoromea atoke akapambane na operesheni za cdm,huku yeye(mwenyekiti)akipaa kwenda ughaibuni kula bata,sasa dogo anaamua kuharibu jumla,anaropoka chochote kinachojaa mdomoni.
 
Wakuu, hivi inawezekana kesi hii ikaunganishwa na ile ya Mukama kudai kuwa Chadema wameleta magaidi toka Libya kuja kufanya fujo uchaguzi wa Igunga?
 

Mkuu Matola heshima mbele,
In addition to that, kuna watu wanamshauri Nape Nnauye amfuate Andrew Chenge amtetee. Wanasahau kwamba Chenge ni Pro-Lowassa na Nape Nnauye ni Anti-Lowassa. Kwa namna yoyote vile ni vigumu Chenge kumtetea Nape Nnauye. The same applied to Nimrod Mkono. Huyu ni Pro-Mafisadi, kwa hiyo vigumu amtetee Pro-Kujivua Gamba.

Yani cha kumshauri Nape, amtafute labda Joseph Thadayo au Marehemu Masumbuko Lwamwai.

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
nape hana ushahidi kam cdm wanapewa pesa toka nje....mdomo umemponza
 

liache kuropoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…