CHADEMA wamepata walichokuwa wanakitafuta ndani ya UKAWA?

CHADEMA wamepata walichokuwa wanakitafuta ndani ya UKAWA?

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,573
Ndugu wadau na wapenzi wa JF, itakumbukwa kwamba tukio la kuanza kwa vikao vya Bunge Maalum la Katiba lilitanguliwa na tukio la machafuko yaliopelekea mvutano wa kisiasa ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na hata kupelekea chama hicho kuondokewa na makamanda wao mahiri kama ZITTO ZUBERI KABWE, SAMSOM MWIGAMBA na KITILA MKUMBO.

Ni kutokana na sintofahamu hiyo ndani ya chama hicho kikuu cha Upinzani iliyopelekea, Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE kukubali kuundwa kwa umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kutangaza kulivunja Baraza kivuli la Mawaziri liliokuwa likiundwa na Wabunge wa chama chake pekee na kulisuka upya kwa kuwaingiza Wabunge wa vyama vya CUF na NCCR, Wabunge ambao awali Mh.MBOWE alisema wasingeshirikishwa kwenye baraza hilo kwa madai kuwa vyama hivyo ni washirika wa CCM kwa vigezo kwamba CUF kimeunda serikali ya umoja wa Kitaifa huko Zanzibar na NCCR kinaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni mteule wa Rais katiba bunge la Jamhuri ya Muungano.

Msimamo wa UKAWA ulionekana kuwa na nguvu jambo ambalo lilikipa chama cha CHADEMA faraja kwa vile kule kulemewa na mgogoro ndani ya chama kulianza kufunikiwa kabisa na Muungano huo wa UKAWA.

Swali: Maandamano haya yanayoendeshwa na CHADEMA nchi nzima bila kuwashirikisha washirika wengine wa UKAWA, Je CHADEMA wamejiridhisha kuwa sasa umaarufu wao umerudi na hawana haja tena ya kuendelea na washrika wa CCM?
 
Sera ya CHADEMA ni Maandamano, maandamano,maandamano. CUF na NCCR wanaamini katika maridhiano,siyo rahisi vyma hivyo kuwa kitu kimoja. kwa kifupi, UKAWA ndo umkeufa hivyo, CHADEMA wameshapata walichokuwa wanakitafuta, NCCR na CUF wamebaki kwenye mataa
 
Mbowe anakiua chama. Maskini ona jinsi wananchi walivyosusa maandamano yao. Yaani hata makamanda wenyewe wamesusa
 
Hivi hawa chadema wanaandamana kwa sababu gani?
 
Mbowe anakiua chama. Maskini ona jinsi wananchi walivyosusa maandamano yao. Yaani hata makamanda wenyewe wamesusa
Yeye mwenyewe yupo hukooo South Africa anatumbua maisha kwa kulala hotel ya dola 700 kwa aiku huku wafuasi wake wakishindia mikate
 
CHADEMA wakitaka maandamano Mbowe na washirika wake watangulize watoto na wake zao mbele na sie ndio tufuate , tumechoka sana kupata ulemavu na kujeruhiwa wakati wao wakikaa majumbani kutuangalia kwenye Matv wakiangalia tunavyopata kibano , hata kuja hospitali hawaji wakati tukiwa tumelazwabaada ya kupata kibano.
 
Mbowe anakiua chama. Maskini ona jinsi wananchi walivyosusa maandamano yao. Yaani hata makamanda wenyewe wamesusa

Mkuu, jana nimemsikia KIGWANGALA anawashauri POLISI wawaache waandamane kwa vile idadi yao haizidi hata polisi wenyewe.
 
CHADEMA ni janga la kitaifa, watu wanaacha kufanyakazi, wanakuwa vilema kwa sababu yao, hatari sana. Vijana tuwe makini sana.
 
Mkuu, jana nimemsikia KIGWANGALA anawashauri POLISI wawaache waandamane kwa vile idadi yao haizidi hata polisi wenyewe.
Tehetehetehetehetehe, tatizo ni kwamba, hata wakiachwa waandamane kwa amani, wao wanaleta vurugu na kupora vitu. Bora kinga kuliko tiba
 
CCM watafanikiwa kuwapatia watanzania KATIBA BORA itakayowaunganisha na kuwa kitu kimoja ili kuijenga nchi yao kwa miongo mingine mingi ijayo?

Nafikiri hii ndiyo hoja ya msingi kwa sasa.
 
CCM watafanikiwa kuwapatia watanzania KATIBA BORA itakayowaunganisha na kuwa kitu kimoja ili kuijenga nchi yao kwa miongo mingine mingi ijayo?

Nafikiri hii ndiyo hoja ya msingi kwa sasa.
Ni kweli Mkuu. Katiba mpya itakuwa bora zaidi kuliko hii tuliyonayo sasa
 
Hii tabu sana nchi hii kuna watu mburula sana,kuna vinaja wanajiita BAWACHA wanasumbua sana.
 
Back
Top Bottom