CHADEMA wameifikisha hapa nchi

CHADEMA wameifikisha hapa nchi

Mkuu, ongeza na wa tatu anaitwa [HASHTAG]#lissumsaliti[/HASHTAG] ameanzisha wimbi jipya la kuhubiri ukabila bila aibu kwa lengo la kuiingiza nchi yetu kwenye chuki za kikabila. Kabla sijachukia mtu wa kabila lolote, nitaanza kwanza kumchukia yeye. Damn ......!
Mkuu tumsamehe bure yule mashinji alishasema hata lissu akipona atakua sio lissu yule ndio maruwe ruwe yameshaanza hivyo!
 
Wengi watashangaa kichwa cha habari lakini ukweli watu wawili waliopo CHADEMA ndio waliofikisha nchi hapa.

Hii hali ngumu wanayoipigia kelele CHADEMA na kusema deni la taifa limepanda nchi imeingia mikataba mibovu, kila kukicha mali za nchi zinakamatwa inasikitisha kua hawa waliokua vinara wa kusababisha cancer hii,
wao ndio wamekua mstari wa mbele kulalama kama ni malaika ambao wameshushwa upya toka mbinguni na hawajafanya chochote wala hawakuwepo serikalini.

Fedrick Sumaye ndie waziri mkuu aliekaa muda mrefu madarakani kwa miaka 10 ndio kipindi ambacho taifa lilishuhudia uza uza kwa bei ya kutupa kwa kisingizio cha kubinafsisha.

Ikiwa yeye alikua ni mshauri wa rais na boss wa mawaziri wote mchango wake ulikua ni upi kipindi chake nchi ndio ilioingia mikataba mahotelini yeye hakua mzalendo wala na uchungu kipindi hicho uzalendo huo uzaliwe sasa ni mengi madudu yake lakini tusiogope kumuhoji mtu huyu bila soni haijalishi ni mwenyekiti wala nini.

Lowassa utetezi wake usio na mashiko vurugu zote za awamu ya nne yeye alishiriki kwa namna moja ama nyingine hata alipofukuzwa uwari mkuu aliendelea kulihujumu taifa akiwa nje ya baraza la mawaziri kupitia vyeo vyake vya kamati za bunge na chama.

Hawa watu wawili si watu wa kuwachekea kama ni china siku nyingi wangekua wamekufa kifo cha kishujaa cha kitanzi, Leo hii bila haya wanasimama jukwaani kuwakejeli wananchi wenye hali mbaya kiuchumi na bado pia mazuri yanayofanywa na Rais Magufili hawataki kuyaunga mkono wanayapinga ili waendelee kuneemeka na maovu yao.Tusiogope kuwahoji CHADEMA na tusikubali hoja nyepesi za mbowe na hao watu wawili.

Tanzania bila ufisadi inawezekana.

Tumuunge mkono juhudi za maendeleo zimeanza kuonekana changamoto kila mahali duniani hazikosekani!

Haya nayo ni maajabu ya dunia. Wanalaumiwa Lowassa na Sumaye ila Ben na JK wao malaika hakuna wanapotakiwa wala kuwajibishwa? Kwani Lowassa na Sumaye ndiyo walikuwa marais vipindi hivyo?
 
Kumbe waliolitia hasara hili taifa wanajulikana???
Sasa inasubiliwa nini kuwapeleka mahakamani ili watumikie adhabu???
 
Haya nayo ni maajabu ya dunia. Wanalaumiwa Lowassa na Sumaye ila Ben na JK wao malaika hakuna wanapotakiwa wala kuwajibishwa? Kwani Lowassa na Sumaye ndiyo walikuwa marais vipindi hivyo?
ben na jk wamemlaumu nani au umewaona wapo jukwaa gani wakiponda kama si wajinga na malofa!
 
Huo ndio ukweli halisi ila hawa wafuasi mahaba hawalioni hilo bali uchagadema umewajaa saa zote ni bangi na matusi tu.
Tuseme hayo madai ni ya ukweli, je walifanya hayo wakiwa chama gani? Pia tusisahau kuwa kwa katiba yetu tuna rais mtendaji ambaye siyo ceremonial, ikiwa na maana kuwa waziri mkuu ni mshauri tu, maamuzi makubwa yapo kwa raisi. Sasa nyie mnasema chadema wanakumbatia hao mawaziri wakuu, sasa niulize nyie mmechukua maamuzi gani kupambana na wale waliokuwa wafanya maamuzi wakubwa ambao bado wapo ndani ya chama???
 
Back
Top Bottom