CHADEMA wameifikisha hapa nchi

CHADEMA wameifikisha hapa nchi

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
20,142
Reaction score
24,432
Wengi watashangaa kichwa cha habari lakini ukweli watu wawili waliopo CHADEMA ndio waliofikisha nchi hapa.

Hii hali ngumu wanayoipigia kelele CHADEMA na kusema deni la taifa limepanda nchi imeingia mikataba mibovu, kila kukicha mali za nchi zinakamatwa inasikitisha kua hawa waliokua vinara wa kusababisha cancer hii,
wao ndio wamekua mstari wa mbele kulalama kama ni malaika ambao wameshushwa upya toka mbinguni na hawajafanya chochote wala hawakuwepo serikalini.

Fedrick Sumaye ndie waziri mkuu aliekaa muda mrefu madarakani kwa miaka 10 ndio kipindi ambacho taifa lilishuhudia uza uza kwa bei ya kutupa kwa kisingizio cha kubinafsisha.

Ikiwa yeye alikua ni mshauri wa rais na boss wa mawaziri wote mchango wake ulikua ni upi kipindi chake nchi ndio ilioingia mikataba mahotelini yeye hakua mzalendo wala na uchungu kipindi hicho uzalendo huo uzaliwe sasa ni mengi madudu yake lakini tusiogope kumuhoji mtu huyu bila soni haijalishi ni mwenyekiti wala nini.

Lowassa utetezi wake usio na mashiko vurugu zote za awamu ya nne yeye alishiriki kwa namna moja ama nyingine hata alipofukuzwa uwari mkuu aliendelea kulihujumu taifa akiwa nje ya baraza la mawaziri kupitia vyeo vyake vya kamati za bunge na chama.

Hawa watu wawili si watu wa kuwachekea kama ni china siku nyingi wangekua wamekufa kifo cha kishujaa cha kitanzi, Leo hii bila haya wanasimama jukwaani kuwakejeli wananchi wenye hali mbaya kiuchumi na bado pia mazuri yanayofanywa na Rais Magufili hawataki kuyaunga mkono wanayapinga ili waendelee kuneemeka na maovu yao.Tusiogope kuwahoji CHADEMA na tusikubali hoja nyepesi za mbowe na hao watu wawili.

Tanzania bila ufisadi inawezekana.

Tumuunge mkono juhudi za maendeleo zimeanza kuonekana changamoto kila mahali duniani hazikosekani!
 
Fisadi huyu

upload_2017-6-13_14-5-10-jpeg.636892
 
Wengi watashangaa kichwa cha habari lakini ukweli watu wawili waliopo chadema ndio waliofikisha nchi hapa

Hii hali ngumu wanayoipigia kelele chadema na kusema deni la taifa limepanda nchi imeingia mikataba mibovu,kila kukicha mali za nchi zinakamatwa
inasikitisha kua hawa waliokua vinara wa kusababisha cancer hii ,
wao ndio wamekua mstari wa mbele kulalama kama ni malaika ambao wameshushwa upya toka mbinguni na hawajafanya chochote wala hawakuwepo serikalini

Fedrick sumaye ndie waziri mkuu aliekaa muda mrefu madarakani kwa miaka 10
ndio kipindi ambacho taifa lilishuhudia uza uza kwa bei ya kutupa kwa kisingizio cha kubinafsisha

ikiwa yeye alikua ni mshauri wa rais na boss wa mawaziri wote mchango wake ulikua ni upi kipindi chake nchi ndio ilioingia mikataba mahotelini
yeye hakua mzalendo wala na uchungu kipindi hicho uzalendo huo uzaliwe sasa ni mengi madudu yake lakini tusiogope kumuhoji mtu huyu bila soni haijalishi ni mwenyekiti wala nini

Lowassa utetezi wake usio na mashiko vurugu zote za awamu ya nne yeye alishiriki kwa namna moja ama nyingine hata alipofukuzwa uwari mkuu aliendelea kulihujumu taifa akiwa nje ya baraza la mawaziri kupitia vyeo vyake vya kamati za bunge na chama

Hawa watu wawili si watu wa kuwachekea kama ni china siku nyingi wangekua wamekufa kifo cha kishujaa cha kitanzi,
Leo hii bila haya wanasimama jukwaani kuwakejeli wananchi wenye hali mbaya kiuchumi na bado pia mazuri yanayofanywa na magufili hawataki kuyaunga mkono wanayapinga ili waendelee kuneemeka na maovu yao

Tusiogope kuwahoji chadema na tusikubali hoja nyepesi za mbowe na hao watu wawili

Tanzania bila ufisadi inawezekana

Tumuunge mkono juhudi za maendeleo zimeanza kuonekana changamoto kila mahali duniani hazikosekani!
Huo ndio ukweli halisi ila hawa wafuasi mahaba hawalioni hilo bali uchagadema umewajaa saa zote ni bangi na matusi tu.
 
Wawahoji wao ndo wana vyombo vya mahojiano?fine wamewahoji wakakubali wao ni mafisadi then wanawapeleka wapi sasa?ebu waambie hao wenye mamlaka ya kukusanya kodi zetu waende kuwahoji hao watu wanaokunyima usingizi
subiri warukeruke wataingia timing mtawaona nyuma ya nondo serikali imedhamiria kusafisha uvundo wote!
 
viongozi wakuu wa utapeli na ufisadi mmewakumbatia mnaogopa hata kuwahoji!

Acha siasa nyepesi dogo. Unataka kumuhoji nani zaidi ya kuleta siasa za majitaka? Mahakama ya kawaida ipo na mkiona hiyo inachelewa kuna ya mafisadi. Magufuli amebaki kuleta siasa nyepesi majukwaani zisizo na mvuto eti majizi yako na yanakimbilia cdm. Yeye ndio rais na anaongoza kibabe, ni mpinzani gani mwenye kesi ya ufisadi hadi sasa?

Uza ubongo huo ww unakaa nao kwa hasara. Hao mnaowaongopea mnapambana na ufisadi wameshawajua hamna jipya ila vitisho ndio vinawanyamazisha.
 
Never Ever, Roho iliniuma mlimpommiminia risasi Lissu, hata wewe ungeteuliwa tatizo huweki namba zako za simu kwenye mabandiko yako.
Mkuu wengine hatuna uroho wa madaraka kama wale waliohama kisa wamekatwa!
 
Mleta thread nakuapia ni kati ya haya;
  1. UU mvuta bange wa miaka mingi kiac kwamba imeshaharibu baadhi ya nerves kichwani
  2. Unavuta petrol
  3. Ni mnywaji 'katili' wa viroba kwa muda mrefu
  4. Ulikumbwa na utapiamlo mkali sana utotoni ulioharibu uwezo wako wa kufikiri na kupambanua mambo.
Jitafakari katika hayo.
 
Acha siasa nyepesi dogo. Unataka kumuhoji nani zaidi ya kuleta siasa za majitaka? Mahakama ya kawaida ipo na mkiona hiyo inachelewa kuna ya mafisadi. Magufuli amebaki kuleta siasa nyepesi majukwaani zisizo na mvuto eti majizi yako na yanakimbilia cdm. Yeye ndio rais na anaongoza kibabe, ni mpinzani gani mwenye kesi ya ufisadi hadi sasa?

Uza ubongo huo ww unakaa nao kwa hasara. Hao mnaowaongopea mnapambana na ufisadi wameshawajua hamna jipya ila vitisho ndio vinawanyamazisha.
Msingi wa chadema ulipotelea hapa na kuleta mpasuko kwenye majibu mepesi subiri kabla ya 2020 mtawasalimia kwenye nondo!
 
Chadema hawakuwahi kuwa na serikali iweje uwatuhumu?
Wakati Sumaye na Lowassa wakiwa viongozi hali ya uchumi ilikuaje? Je deni liliongezeka ama lilishuka au kasi yake ya ukuaji iikuaje?

Je wakati wa Mizengo pinda?

Mfalme akipigana vita na kushinda hupewa sifa zote hivyo kama kama Rais ndio kila kitu iweje leo muwasingizie wasaidizi badala kumlaumu mfalme?

Pia tuache kuweka tuhuma za jumla jumla. Weka facts alifanya hiki matokeo ni haya.

Mfano waziri wa uvuvi alikamata isivyo halali meli za wavuvi ambapo leo tunadaiwa mabilioni kama fidia.

Waziri wa ujenzi alibomoa nyumba mwanza leo serikali inadaiwa.

Waziri wa ujenzi alivunja mikataba bila kufuata sheria leo bombadier imeshikiliwa.

Hii itasaidia kumpa mtu credit au kumchafua kama unavyotaka kutuaminisha.

Acha maneno weka facts
 
Back
Top Bottom