CHADEMA wamchagua Meya wa CCM licha ya wingi wao

CHADEMA wamchagua Meya wa CCM licha ya wingi wao

Magufuli anaweza kuubadili upepo wa siasa za nchi hii,ila si kwa haraka kiasi hiki,kama madiwani wa chadema wamesombwa na upepo huu haraka namna hii basi niseme tu kuwa walikuwa wepesi kupitiliza,hawajui wanachosimamia,in short hawana msimamo,kwa lugha nyingine ni bendera fata upepo,inafaa wawekwe chini,wafundwe,wajue kusimamia misingi ya kisiasa ya chama kilichowapa ridhaa.

Mlikosea kununuliwa
 
Magufuli anaweza kuubadili upepo wa siasa za nchi hii,ila si kwa haraka kiasi hiki,kama madiwani wa chadema wamesombwa na upepo huu haraka namna hii basi niseme tu kuwa walikuwa wepesi kupitiliza,hawajui wanachosimamia,in short hawana msimamo,kwa lugha nyingine ni bendera fata upepo,inafaa wawekwe chini,wafundwe,wajue kusimamia misingi ya kisiasa ya chama kilichowapa ridhaa.


bado hujasema kitu hapa. Malengo sahihi ya viongozi wa nchi yawe nini hasa??! Kutetea ushindi wa chama? au kutetea maslahi ya wananchi! Ikibainika kuwa Mtu X anatetea maslahi ya wananchi zaidi kuliko Mtu Y kwa mtizamo wenye hekima, does it matter huyo mtu anatoka chama gani? Ukisema ndiyo wewe utakuwa mpumbavu tu! Kaa na kadi yako ya chama...sema moyoni mwako, mimi ni mwanachama wa chama A mwenzangu ni mwanachama wa Chama B. Tunachotafuta ni nini hasa. Tunatafuta maendeleo ya vyama???? au maendeleo ya nchi na watu wake? Vyama vimewekwa kusudi kubwa likiwa kupanua mitizamo ya kuleta maendeleo ya nchi na watu wake! Tunaunganishwa na hicho! Vyama kazi yake kushindanisha fikra za kuwezesha lengo hilo kuu. Kwa maana hii, tutasikiliza hoja za watu wakiwa na kadi tofauti-tofauti. Kadi inayowakilisha fikara chanya zaidi katika kutufikisha katika lengo letu kuu kwa ujumla wetu ndiyo hiyo tunaipa nafasi ya kutuongoza. Hoja ndiyo inatizamwa---na siyo kadi, hoja ndiyo inayoamua. Kadi kazi yake inaishia kwenye kutoa (kuleta) fursa ya kutetea hoja. Fullstop! Idadi kubwa ya Wabunge wa CCM katika bunge lililopita walijipatia sifa ya wapumbavu kwa sababu hii unayoitetea hapa--kuunga mkono upumbavu pale bungeni kwa sababu tu ya kutetea upuuzi uliopelekwa na chama chao. Jifikirishe vizuri! Mungu akupe nuru kuona vizuri.
 
Kama hii habari ni kweli basi haina haja ya upinzani kupewa nchi, humo kwenye halmashauri ndio tulitegemea wachukue uzoefu lakini ndio kwanza wanatukatisha tamaa.

Mkuu wa wilaya ccm, Mkurugenzi ccm,Meya ccm, Naibu Meya Ccm..... Mnatukatisha tamaa wananchi!
 
Kama hii habari ni kweli basi haina haja ya upinzani kupewa nchi, humo kwenye halmashauri ndio tulitegemea wachukue uzoefu lakini ndio kwanza wanatukatisha tamaa. Mkuu wa wilaya ccm, Mkurugenzi ccm,Meya ccm, Naibu Meya Ccm..... Mnatukatisha tamaa wananchi!


Uzoefu si ndo huo sasa ushaanza?! Kutakuwepo mikutano ya full council, kutakuwepo kamati mbalimbali, kutakuwepo ziara za mafunzo; taratibu watakuwa wanajifunza jinsi ya kuendesha halmashauri. Hawa madiwani wengine wamefanya kazi kama wajasiriamali muda mwingi wa maisha yao, wengine hii ndo mara ya kwanza wanaingia kwenye full council. Ukimpa diwani kama huyu uwenyekiti si unatafuta shida? Waache kwanza waone vikao vinaendeshwajue, maamuzi yanafikiwaje na utekelezaji wake unaendaje af sasa mwaka 2020 madiwani hawa wapya ambao ni mara ya kwanza kuingia katika full council, kama wakichaguliwa tena af wakiomba uenyekiti hapo sasa tunakuwa na hoja ya kuwapatia kiti. Leoleo mtu katoka kuuza vitunguu sokoni, wenzake pale sokoni wamemchagua awe diwani wewe unataka awe mwenyekiti wa Council??? Kajifunze haya mambo lini, saa ngapi!? Ndo wameanza hivo kuchukua mafunzo.... vuta subira!
 
HALMASHAURI YA WILAYA YA BABATI

Ina Madiwani kama ifatavyo:

CHADEMA - 19
CCM - 16

Jana walifanya uchaguzi wa:
1- Mwenyekiti wa Halmashauli (almaarufu wa Kanseli)...
2- Makamu Mwenyekiti wa Halmashauli

Matokeo:
"WOTE WAMETOKA CCM."

KUNA FUNZO KUBWA SANA HAPO
Uongo wa aina hii unajenga sifa ya wewe kuitwa mpumbavu
 
Back
Top Bottom