Chadema wakwepa kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wakwepa kodi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BRIA, May 22, 2011.

 1. B

  BRIA Senior Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Chadema wamedaiwa kukwepa kodi na mamlaka ya kodi TRA.hili wadau mnalionaje?
   
 2. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wanataka wananchi wafanye nini? Kwani Tanzania hakuna sheria? Kama wamevunja sheria wapelekwe Mahakamani ukweli ufahamike. Wakianza kubishana na CDM waende kwa msajili wa vyama. THEY SHOULD BE PROFESSIONALS AND SHOULD NOT START SEEKING PUBLIC SYMPATHY.
   
 3. h

  hans79 JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  wapelekwe kwenye mamlaka husika,sheria za kod zajulikana n fain na kulipa ulichokwepa sio kuleta porojo luoga alikuwa wapi?aache unafik achunguze kila chama,pia pana hoja kwa nn achunguze had alipoguswa kwa uzembe wake huyo luoga?
   
 4. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM hadi Leo hawatoa mahesabu Yao ya uchaguzi na hakuna anayezungumza hawa walioweka wazi mahesabu Yao mbele ya umma na serikali ndio wanaozungumzwa na kufuatiliwa au ni kutafuta kudhoofisha nguvu ya chadema?
   
 5. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hawa TRA hovyo sana,

  Wao hawana uwezo mpaka media ziseme hivi wakati CCM walipoingiza magari zaidi ya 100 (land cruiser hardtop) na ushuru ukalipwa kidogo kuliko ilivyo stahili mbona hawakusema lolote? Inaonyesha hata wao wanafanya kazi zao kisiasa na hili ni hatari kwa taasisi kubwa kama hiyo.

  Luoga hujafunguka tu, mambo yameshabadilika fanyeni kazi acheni ushabiki na kulindana siku si nyingi mtajuta kwa mliyoyafanya.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  watoe report inayoonyesha hawalipi kodi sio wanakuja na maneno ya kwenye taarabu hapa
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hii habari iko nusu nusu! Nani wa TRA na lini alisema kuwa CDM wamekwepa kodi? Je, CDM wamekwepa kodi ya sh ngapi, lini na ni kodi kuhusu nini? Be specific please!
   
 8. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tatzo TRA wanashindwa kutofautisha profesionalims and politics....kama mtu au chama fulani hakilipi kodi sheria si zipo bas waenda kwa vyombo husika...
   
 9. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  kwanza sio wamekwepa bali ni bado hawajawasilisha vielelezo vinavyotakiwa na TRA kwa hiyo wakishawasilisha na kukawa na defect ndo wanaweza kuwadecleared wakwepa kodi na kuna sheria za kuchukuliwa dhidi wa wakwepa kodi na sio kwenda kulalamika ktk gazeti la mzalendo wakati bado hata TRA bado hajamaliza kukagua vielelezo sababu bado havijawasilishwa.

  Hizo ni siasa za majitaka kweli ccm mmeshikwa pabaya na CDM yaani mnakukuruka kuwataftia kashfa mtazichimba hadi shimoni. Na kuonyesha udhaifu wa wenzenu sio kigezo cha nyie kuwa wema, au wasafi otherwise tunawaona wote wasanii. Maisha bora kwa mtz hayaji kwa kuishambulia chadema bali fanyeni wajibu wenu nyie ni chama tawala lazima wapinzani wawashambulie ktk any weakness angle na nyie instead of working out and kutimiza ilani yenu mnaanza kushambulia wanaowakosoa na kama semina elekezi Dodoma was all about mmepotea na anguko lenu litakuwa kuu na la kishindo.

  Hata ka mkiwachafua CDM vipi watz washawachoka na hawasikii chochote hata ka mkisema chadema wanakula nyama za watu.

  Kumbukeni ktk mkutano wa NEC mwaka 1995 mwalimu Nyerere alisema ''viongozi bora wa taifa hili watatoka CCM.... Ila CCM ikikosa uongozi bora. Watanzania watatafuta uongozi bora kwingine'' na ndio linalotokea sasa watz wanatafuta viongozi bora kwingine hawasikilizi kashfa zenu na siasa taka zenu, mnatumia kila resource ktk uwezo wenu kuwachafua wenzenu lakini kumbukeni ''always truth prevaills'' ukweli utasimama na mtabakije na aibu!!

  Msije sema hamkuambiwa
   
 10. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sikujua kama CCM kuna siku watakuwa hovyo kiasi hiki, maji yako shingoni wanatapatapa, kila wanachofanya kuidhoofisha chadema wanashindwa, sijui wanaandaa mkakati gani saa hizi maana hili la kukwepa kodi linaloandikwa na gazeti lao mzalendo pekee naona nalo halina mshiko na litazimika muda sio mrefu.
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  TRA hovyooo kabisa, wanafanya kazi kisiasa duh nchi imeoza kabisa hii
   
 12. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,465
  Likes Received: 1,413
  Trophy Points: 280
  Wahindi ndio wakwepaji kodi wakubwa, TRA wanajua ila hawana time nao. Taasisi kama hii nayo ni kuifuta tu kwanza haina ubunifu wa kuongeza njia za kukusanya mapato zaidi ya kutengeneza mianya wa rushwa kwa watendaji wake
   
 13. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama ni kweli wawapeleke CHADEMA mahakamani,hao TRA wametumwa na CCM
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naona TRA nao wamejiunga na siasa za maji taka, ila nao wajiandae funza wote wataanikwa.
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nani anayekusanya Kodi? Jibu TRA
  CHADEMA wamekwepaje Kodi? jibu wanalo TRA
  Nani amewasaidia CHADEMA kukwepa kodi? Jibu ni TRA
  Nani anayetakiwa kuwajibika? Jibu ni TRA kwa kushindwa kusimamia ukusanyaji wa Kodi maana Kama CHADEMA chama cha upinzani kimeweza kufanikiwa kukwepa kodi je ni Mangapi yanapita TRA

  Ni Muda sasa wa kuifunua TRA
   
 16. h

  hans79 JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  je tra hawana ujuzi wa kufahamu thamani ya mzigo?inaelekea wanafanyakaz kwa hisia hawana uwezo na fan hiyo,nalo tatizo la kuajiliwa kwa vimemo bila taaluma kwa tz ndo uozo uliopo.mfano takukuru hufanyakaz wanapoletewa ubembea,kaz ipo kila sekta tz uozo mtupu
   
 17. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,719
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Kwani we unalionaje mkuu??!!!

  Kukwepa kodi ni kawaida katika nchi kama Tanzania, wewe unakwepa kodi na kama sivyo basi unatamani kukwepa kadhalika mimi na wengineo..humu jamvini kuna watu wengi tu ingawa hawawezi kukiri hapa wamewahi au wanatamani wapate loopholes wakwepe kodi mfano kuna watu wanaagiza magari kutoka Japan, kisha wanachakachua CIF price ili waweze kukwepa kodi....kuna wengine wana vikampuni vyao wanajilipa mishahara lakini hawajikati PAYE wakisubiri TRA audit ilhali wanafahamu kuwa PAYE ni self assessed alimradi orodha ni ndefu.

  Nadhani mkuu ulitaka tuseme kuwa TRA wana agenda mbaya dhidi ya CDM, inawezekana lakini CDM wakitaka wanaweza kuigeuza hii scenario kuwa ni mtaji wa kisiasa...wawaite TRA wafanye Audit kisha kama kuna kodi itakuwa haikulipwa basi walipe na adhabu yaani faini na kama walilipa zaidi basi wapewe tax credit au refund...wakifanya hivyo watakuwa wamejisafisha mbele ya umma kama chama cha watu makini, watu wanaozingatia sheria za nchi kwa kulipa kodi stahiki.

  Baada ya hapo CDM watakuwa wameweka precedent ambayo vyama vingine ili viweze kujidai kuwa ni makini basi na vyenyewe viikaribishe TRA kwa audit...kwa hiyo CDM itakuwa imeongoza wengine wamefuatia...hii itawapa chati kwa kiwango kikubwa.

  Shida yetu hapa JF ni lack of objectivity katika kuangalia mambo; jazba na ushabiki wetu kwa vyama una-cloud our reasoning and judgement na matokeo yake vitu vingi tunaviangalia kwa malyenge wakati vitu vingine kwa watu walio positively minded wanaweza kuvigeuza kuwa ni opportunity..inasikitisha kwa kweli!!!!
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hiyo haiwezi kuwa justification au utetezi dhidi ya tuhuma hizo za kukwepa kodi. Maana yangu ni kwamba it doesn't matter wakwepaji mko wangapi, kama ni kweli kwamba wewe ni mkwepaji. Kutoa mahesabu ni ku-complya na matakwa ya Msajili na CAG. Hili la kodi ni la TRA and they should come clean on this.
   
 19. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kazi kweli kwa CDM, kukwepa kulipa kodi ni UFISADI!
   
 20. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Yashindwa kuwasilisha taarifa kama ilivyoagizwa na TRA
  Na Mwandishi Wetu
  CHAMA cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimeingia matatizoni kuhusiana na masuala ya ukwepaji kodi baada ya kushindwa kuwasilisha taarifa ya ulipaji kodi kama walivyoagizwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefahamika. Awali, TRA ilikiagiza CHADEMA kuwasilisha taarifa yao ifikapo Ijumaa iliyopita baada ya kudaiwa kuwepo kwa ukwepaji wa kodi unaofanywa na viongozi wa chama hicho kupitia mishahara ya watumishi na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya chama. Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Placidus Luoga, alikiri jana kushindwa kwa CHADEMA kuwasilisha taarifa hizo kama walivyowaagiza katika barua waliyowaandikia mwanzoni mwa wiki iliyopita. Barua hiyo ya TRA ilitokana na kutolewa kwa habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho ambazo zilichapishwa na MZALENDO zikidai kuwa uongozi wa juu wa CHADEMA umehusika katika ukwepaji wa kodi katika mishahara na ununuzi wa vifaa vya uenezi vya chama hicho. “Bado hatujapata taarifa yao... TRA hatuwezi kusema jambo lolote kama kweli wanalipa kodi ya mishahara kwa watumishi wao au la... ila taarifa zitakapoletwa ndiyo tutajua nini cha kufanya,” alisema Luoga. Sheria ipo wazi kwa mtu au taasisi isiyolipa kodi, hivyo uamuzi wa adhabu si vizuri kuweka wazi kwa sasa hususan kipindi ambacho TRA haina taarifa zao za ulipaji kodi," alisema Luoga. Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo ndiyo watajua nini cha kufanya kama TRA kwa mtu ambaye halipi kodi kupitia sheria na taratibu za mamlaka hiyo pamoja na kupata ukweli wa chama hicho kuwa kinakwepa kulipa kodi.
  “Mwajiri atawajibika kumlipia kodi mtumishi wake ikiwa TRA itaona mfanyakazi anastahili kulipa kodi, hivyo nao CHADEMA wakibainika kwenye hilo basi itabidi walipe kodi,’’alisema. Uongozi wa CHADEMA unadaiwa kukwepa kodi katika uingizaji wa vifaa mbalimbali ikiwemo vya uenezi ambavyo viliingizwa kutoka China kwa njia ya panya kupitia eneo la Holili mkoani Kilimanjaro. Vifaa hivyo vilinunuliwa na chama hicho kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2010 baada ya kupata msaada wa sh. milioni 100 kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara nchini. Hata hivyo, ununuzi wa vifaa hivyo unadaiwa kughubikwa na utata kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kudai kuwa aliongeza sh.milioni 188 ili kununua vifaa hivyo na kufanya kiasi cha fedha kilichotumika kuwa sh.milioni 288.
  Utata kuhusiana na ununuzi huo unathibitishwa na habari za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA pale Mbowe aliposema anakidai chama hicho sh. milioni 188 ambazo aliongeza ili kununua vifaa, lakini ameshindwa kuonyesha risiti aliyotumia kulipa wakati wa kuviingiza nchini ili kuthibitisha madai yake. MZALENDO ilifichua kuwa mshahara wa Dk. Slaa ni zaidi ya sh. milioni saba ambazo ni nyingi kuliko za wabunge alizowahi kuzipigia kelele akidai ni nyingi, ambapo pia mshahara wa katibu mkuu huyo haukatwi kodi na TRA.
  Baada ya kufichuliwa kwa taarifa hizo, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamefichua kwamba ufafanuzi uliotolewa na viongozi hao ni wa uongo.
  Habari zilisema Komu kudai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi ni uongo wenye lengo la kutaka kuficha jinsi baadhi ya viongozi waandamizi walivyounda mtandao wa kutumbua fedha za CHADEMA.
  MZALENDO ilifanikiwa kupata waraka ambao unaonyesha kuwa mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokaa Januari 29 hadi 30 mwaka huu, Dar es Salaam ni tofauti na maelezo waliyotoa Komu na Marando.
  Kwa mujibu wa waraka huo ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita ambazo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi.
  Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.
  Kwa upande wa posho, Slaa analipwa mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi huku fedha za majukumu zikiwa ni sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000.
  Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa ni maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.
  Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Licha ya kupewa fedha hizo, Dk.Slaa ameendelea kupewa posho nyingine ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi huku akiwa tayari amelipwa na chama sh. milioni 40 kumalizia nyumba yake ambayo sasa anaishi.


  Chanzo: Gazeti la Mzalendo, Mei 22, 2011

  Kodi ni wajibu haina hiari!
   
Loading...