Elections 2010 CHADEMA: Wakati wa kuandaa Mawakala wa vituo vya Kura ni sasa

Nicky82

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
941
64
Napenda kuona CHADEMA wakati huu wa kampeni ikiwakumbusha wananchi umuhimu wa kupiga kura na kuhakikisha kura zao zinaehesabiwa kwa yule mgombea wao waliyemchagua.

Hii itahitaji CHADEMA kuwa na Mawakala makini na wenye kujitolea ambao kwa moyo thabiti watakuwa tayari kusimamia na kulinda kura kwa niaba ya wale wote watakaokuwa wamepiga kura kuichagua.

Ni ukweli usiopingika kuwa hili ni moja kati ya mianya ambayo CCM huwa wanaitumia kwa kuiba kura, kuandika kura hewa au kwa kubadili matokeo. Tukiwa na takribani miezi mitatu hadi siku ya kupiga kura Oktoba 31, ni lazima CHADEMA waanze utaratibu sasa wa kutoa elimu kwa uma ya jinsi ya kusimamia zoezi la uhesabuji wa kura ili kuhakikisha kuwa hadi ifikapo siku ya Uchaguzi katika Kila kituo CHADEMA iwe na wakala wake atakeyekuwa pale kwa lengo la kulinda na kusimamia kura zake.

Binafsi panapo majaliwa nitahakikisha nakuwa WAKALA wa moja kati ya vituo vya kupigia kura lengo likiwa ni moja tu, kulinda,kutetea na kuhakikisha kura yangu na za wananchi wengine tuliochagua UKOMBOZI zinahesabiwa kwa Dk. Slaa, Wabunge na Madiwani wake
.

Nitakuwa tayari kushinda njaa ikibidi, Nitajitolea, sitahitaji posho, wala sitanunuliwa kwa bei yoyote na CCM, kwani hakuna thamani kwangu inayozidi Fahari ya kuona TAIFA hili likikombolewa kutoka kwenye mikono ya wezi na wanyang'anyi.
 
Back
Top Bottom