Kama mwongozo wa EAC unasema hivyo ni dhahiri Mahakma ya Jumuia itatengua maamuzi ya Bunge letu. Hivi kwa nini tunapenda kupata aibu hivi kila wakati? CCM hakuna aliyebaki mwenye ufahamu timamu akasimama na kuelekeza wenzake?
Kweli kumbe kifo kikifika hakuna wa kukizuia. CCM iliyokuwa moja ya vyama mahiri Africa iko ICU inapumulia gas na na mtungi wa gas umebaki robo na hakuna ziada.
kina January Makamba wansojifanya MaLiberals hara hili dogo kiasi hiki wameshindwa kukishauri chama chao na hayo nahafidhina yanayoendelea kuishi ktk karne ya 3.
Asiyeona husubiri kuonyeshwa. sidhani kama hii ilihitaji msomi wa PhD kuishauri ccm. Tabia ya namna hii ya defensive and protective politics ndiyo iloua vyama vingi vya kihafidhina barani Afrika.
tambueni kwamba kama nchi hatuwezi kuendelea kamwe kama hatutaruhusu mawazo tofauti kutupa changamoto za dhati. kumbukeni ni vigumu kukaa kwenye confortable zone alafu ukategemea kuendelea. Sasa subitini muone aibu itakayowakuta
Najua mnajidanya kwa kufanya reference kwenye hukumu ya tarehe 31 Machi 2007 iliyotengua ubunge ea wabunge 9 wa Kenya kwenye bunge la EaC lililopita na Kenya kulazimika kuchagua tena. katk hukumu Tz ilisifiwa kwa kuwa na utaratibu wa kuchagua wabunge wa bunge la EAC, lakini tambueni mazingira yamebadilika sana. lkn muhm kuwa na kanuni ni jambo moja na kanun hizo kuwa za haki kadri ya maelekezo ya mkataba wa EAC ni jambo jkngine.
haoa mabishano yapo jambo moja muhimu. Ni kwa kiasi kanuni zilizopo zinatoa nafasi na haki kwa wanostahili kiipata kwa upande mmoja, na kwa kiasi gani kanuni hizi zinatumoka vibaya kutoa haki kwa wasiyostahili na kuminya haki ya eanostahili kwa upande mwingine.nadhani hapa ndipo busara ya sheria itakapojikita.
Aingii akilini kuona chama chenye wabunge 48 na maana hii kinachoongoza official opposition bungeni kikose mwakilishi kwenye bunge la EAC huku chama ambacho hakina Mbunge hata moja ndani mbunge la Ranzania wala zbar ndicho kitoe mwakilishi.
kwa utaratibu uliyopo kana hauvadilishwi hicho nilichokisema hapo juu kinawezekana kutokea bila shaka. kwa nazingira ya kisiasa yaliyopo kati ya ccm na CDM hii ni lazima itokee ( siyo kamali) ni 100% sure.
Naamini watu wengi wamesihi ccm kutumia busara kuamua hili badala ya husia na husuda za kisiasa zisizo na tija kwa taifa, lakini kama walivyoozea hawakusikia. Aibu siku zote umkuta mjinga.
Haya yaliewezekana miaka iliyopita lakini kwa kizazi hiki hayatawezekana. Tujisahihishe