CHADEMA waitangazia CCM kifo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Na Danson Kaijage, Dodoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kitasimamia uasi dhidi ya sheria mbovu zinazowalinda marais wabovu wastaafu, ambao wameliingiza taifa katika matatizo makubwa ya kiuchumi.


Msimamo huo ulitangazwa jana na Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, mjini hapa katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya barafu kuwatambulisha wabunge wapya, Cecilia Pareso na Joshua Nassari.

Mbowe alisema sheria za kuwawekea kinga viongozi wa juu ambao wameshika madaraka ngazi ya juu ni mbovu na inasikitisha kuona serikali inatumia fedha nyingi za maendeleo kwa ajili ya kuwatunza watumishi wa ngazi ya juu ambao waliitia nchi hasara.


"Wapo viongozi ambao walitumia vibaya mali ya nchi lakini kutokana na kuwekewa kinga ya kutoshitakiwa bado wanaendelea kulipwa fedha nyingi pamoja na huduma mbalimbali kwa kutumia fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kuwasaidia Watanzania katika masuala ya afya na elimu," alisema Mbowe.


Pamoja na kueleza nia hiyo, CHADEMA kimesema kitafanya maandamano makubwa jijini Mwanza mara baada ya kumalizika kwa kikao hiki cha Bunge, kupinga vitendo vya polisi mkoani humo kutetea uhalifu kwa kushuhudia kipigo cha wabunge wake wawili bila kufanya lolote.


"Tutakwenda Mwanza pamoja na wabunge wote wa CHADEMA na tutaandamana hadi kieleweke, tunataka kujua polisi wamepata wapi jeuri hii ya kutetea uhalifu," alisema Mbowe.


Akizungumzia suala la hatima ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mbowe alisema chama hicho tayari kimekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa.


"Mazingira yaliyotumika kutengua ubunge wa Lema ni tatanishi. CHADEMA tunajua haki haiombwi, tumekata rufaa, tuna imani jopo la majaji litatoa uamuzi wa haki.

"Hata hivyo hatuogopi kurudi kwenye uchaguzi, tupo tayari, kwa sasa. Kamanda Lema anatembea mikoa yote kuwaeleza Watanzania kilichotokea na tumempa helikopita," alisema Mbowe.

Aliwataka wananchi wa Dodoma kuacha woga na kupigania mabadiliko ya kisiasa.

"Shughuli hii ni vita, hamuwezi mkaleta mabadiliko wakati mnaogopa polisi. Dodoma mmejaa woga…nawapongeza vijana wa UDOM, lakini Wagogo bado mmelala, nadhani mnajivunia mbunge mashuhuri mwenye misamiati ya matusi.

"Dodoma mnasubiri nini? Kuna vijana wengi, tukiitisha maandamano nani atatoka? Mniwie radhi kwa kauli hii. Tumezunguka nchi nzima maeneo mengine wamekuwa majasiri na ushindi umepatikana, nanyi mnapaswa kuamka," alisema.


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema siku za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukaa madarakani zinahesabika kutokana na wananchi kukichoka.


Alisema jambo hilo limedhihirika hivi karibuni katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki ambako chama hicho kilitumia nguvu kubwa, lakini wananchi wamekikataa.


"Arumeru ni kielelezo kuwa Watanzania wamekichoka, pamoja na kutumia fedha nyingi na vigogo wao, lakini wananchi wamewakataa," alisema na kuongeza kuwa huo ni ujumbe ambao watawala wanapaswa kuupata.


Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, alisema ingawa si mtabiri lakini anajua kuwa mwisho wa CCM kushika hatamu ni pale Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) atakapotangaza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.


Alisema ingawa Arumeru CCM walitumia watu wazito pamoja na kutoa mkwara, lakini hawajaweza kuwahadaa wananchi hao na hatimaye kuipa ushindi CHADEMA.


Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alisema chama hicho hakipo tayari ‘kuuziwa' na Rais Kikwete wajumbe wa katiba kwenye ‘gunia' na ndiyo maana wanaendelea kuchambua wasifu wa kila mjumbe historia yake, uwezo wake, uadilifu wake na iwapo wamependekezwa kweli kama kipaumbele na makundi ya jamii.


Aliwataka wananchi wa Dodoma na maeneo mengine nchini kuendelea kuwaunga mkono kwenye azima ya kutaka sheria ifanyiwe marekebisho mengine kuhusu Bunge Maalumu la Katiba na mfumo wa kura za maoni.


"CHADEMA hatutakubali kura za maoni zisimamiwe na tume ya wachakachuaji wa uchaguzi, ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi na wadau wengine," alisema.


Aidha, aliwataka wanachuo na Watanzania kwa ujumla kuzingatia kuwa serikali imepeleka bungeni muswada wa sheria ya marekebisho mbalimbali ukiwa ndani yake una marekebisho ya sheria ya Bodi ya Mikopo yenye kukandamiza zaidi haki za elimu ya juu hususan kwa vijana kutoka kwa Watanzania wa kipato cha chini.


Kwa upande wake, Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi, mbali na kuwahimiza vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu muda utakapowadia, pia amewataka wawe na tabia ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka, kwani kwa kuacha wanaendelea kuipa nguvu CCM.


Naye Mkurugenzi wa masuala ya Bunge wa chama hicho, John Mrema, alimtaka Profesa Shaban Mlacha wa Chuo Kikuu cha Dodoma kuacha kuwanyanyasa wanafunzi wa chuo hicho ambao ni wanachama wa chama hicho.


Alisema kamwe chama hicho hakitakaa kimya wakati wanafunzi wa chuo hicho wananyanyasika kwa sababu za kisiasa.



 
Chadema wawe na msimamo wasiwe kama Kenya na kuachiana baada ya kuchukua Madaraka

Wamemuachia Moi kila kitu alichochukua yeye na watoto wake; juzi juzi mtoto wake katoa talaka kalipa $ 62 million; wapi?

Lini mtu ana hizo pesa kama sio kuiba? Wasihurumie hao wastaafu; lazima warudishe na waishi kwa pensheni wao na wanao
 
Hii nchi tangu Mwl. Nyerere afariki imekuwa ya viongozi tu ndio wanaofaidi, wanadanganya wananchi eti wamejenga lami, wamejenga sijui madarasa nk, lakini ukweli wenyewe ni kwamba rasilimali tulizonazo na zilizotumika hazilingani kabisa na hali tuliyonayo hata kwa 10%. Viongozi wetu wa serikali na chama tawala wamefilisika kimtazamo na sera, wao wemeweka maslahi yao na chama tu, huko wananchi tuliowengi hatufaiki na lolote kutoka na rasilimali zetu zaidi . Rais hana aibu kwenda kuwa ombaomba za nje kila kukicha kweli aibu sana kwa nchi yetu na usaliti wa hali ya juu kwa wananchi.
Katiba hii tuhakikishe tunatoa kinga ya kushitakiwa kwa viongozi walioliletea taifa hasara walioko madarakani, waliomaliza muda wao na kutaifisha mali zao, hii iwe fundisho kwa kila atakaye uongozi. Na kila mmoja wetu aweke maslahi ya watu awatumikiao kwanza.
Nawakilisha
 
Kweli chama kimeamua liwalo na liwe kwani watasema haki daima!

Na tukumbuke hapa Duniani haki hata siku moja haijawahi kushindwa!
Inapindishwa tu lakini tukirudi kwenye kutaka haki ni dhahiri haki itakuwa haki tu!

Viva Chama cha Demokrasia na Maendeleo!
Vijana tunaunga hoja mkono kwa 100%
 
Haki huwa haitolewi kwa hiari...Inagombewa!
Piganieni haki...mwisho beberu atakimbia miguu ikimgonga kisogo.
 
Kweli chama kimeamua liwalo na liwe kwani watasema haki daima!

Na tukumbuke hapa Duniani haki hata siku moja haijawahi kushindwa!
Inapindishwa tu lakini tukirudi kwenye kutaka haki ni dhahiri haki itakuwa haki tu!

Viva Chama cha Demokrasia na Maendeleo!
Vijana tunaunga hoja mkono kwa 100%
Unaunga mwenyewe hoja mkono, siyo tunaunga hoja mkono.
 
Haki huwa haitolewi kwa hiari...Inagombewa!
Piganieni haki...mwisho beberu atakimbia miguu ikimgonga kisogo.
Toka mmeanza kuandamani mmepata faida gani? Zaidi ya watu kuumizwa na wengine kupoteza maisha yao huku viongozi wenu wakijineemesha tu!
 
Toka mmeanza kuandamani mmepata faida gani? Zaidi ya watu kuumizwa na wengine kupoteza maisha yao huku viongozi wenu wakijineemesha tu!
Wewe ni kinda maana hujui kuwa demokrasia ina gharama zake, hata ikibidi damu!
Hakuna ccm itakayokaabidhi nchi kwa chama kinginew na kubali mezani kuwa wameshindwa...haya ni mapambano..ni vita...ni uasi...ni kuingia msituni!
 
Wewe ni kinda maana hujui kuwa demokrasia ina gharama zake, hata ikibidi damu!
Hakuna ccm itakayokaabidhi nchi kwa chama kinginew na kubali mezani kuwa wameshindwa...haya ni mapambano..ni vita...ni uasi...ni kuingia msituni!
Kama viongozi wenu ndio wanawafundisha hivi basi mjue mmepotea.
 
Kama viongozi wenu ndio wanawafundisha hivi basi mjue mmepotea.
Wa mjini hApotei, labda vijijini kuna misitu mtu anaweza kupotea.
Soma thread huko...Maeneo ya Kagera watu wamechafukwa na roho, wanatamani 2015 ije haraka wamuue mnyama fedhuli!
Hakuna PA kupumulia this time!..mmebanwa left-right!...aibu!
 
Wa mjini hApotei, labda vijijini kuna misitu mtu anaweza kupotea.
Soma thread huko...Maeneo ya Kagera watu wamechafukwa na roho, wanatamani 2015 ije haraka wamuue mnyama fedhuli!
Hakuna PA kupumulia this time!..mmebanwa left-right!...aibu!
Mtasubiri sana mkuu....sidhani kama chama chenu hata kitafika 2015!!!
 
Maoni ya Rejao ni sahihi mbona kwa mtazamo wake nyie mko mjini sisiem mpaka porini wanyama wa porini wanaipigia kura za ndiyo.... nyie mtaambulia kura za mama ntilie tu na kiasi kidogo cha vijana (machinga) na ni mara chache wao kukakaa kusubiri kupiga kura.
 
Back
Top Bottom