Hamad Rashid mara nyingi tu ameshazungumzia masuala yanayohusu tanzania Bara.
Umeshawahi kusikia Mbowe anazungumzia swala la Pemba?
Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kupiga kura yake kuipeleka CHADEMA ikulu kwa sababu zifuatazao
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ifai-hata-kidogo-kuwa-chama-cha-upinzani.html
Kweli wewe na Uelewa wako PEMBA ina Wawakilishi; Wabunge Wengi ki Mraba zaidi ya Tanganyika sasa unataka na huyo MBOWE bado aizungumzie PEMBA? sasa huo sio UKIRITIMBA ni nini?
Kweli haujui kuwa Tanganyika ina matatizo mengi zaidi ya PEMBA? na ina Utajiri lakini unachotwa na VIONGOZI wakuu wabovu wasiojua jinsi gani ni bora kutunza na kulinda Maliasili; Madini; Malighafi za nchi...
Kweli umenishitua...
Attitude za watu kama ZeMarcopolo ndio zinaimaliza nchi yetu. Anapoandika thread zake unapata "tone" ya mtu ambaye ni arrogant,mbinafsi,mnafiki,mzandiki,mwenye uzoefu wa mipasho isiyo na tija kwa taifa bali kwa kundi la watu fulani, mtu aliyejengwa na propaganda zaidi kuliko umahiri wa kuandika mambo yenye kuleta tafari ya maslahi mapana ya Tanzania. Kuwa yeye ni yeye tu na yeye ndiye mwenye funguo za mlango wa chumba cha fikra sahihi za ni wapi Tanzania inakopaswa kwenda. Na kwamba kila mtu anayetaka kufikiri lazima aombe funguo toka kwake. Ukiangalia mabali zaidi kwa kutumia jicho la tatu unagundua kuwa aandikacho ZeMarcopolo na ile hali inayokuja na kile aandikacho ndio kitambulisho hasa cha watawala wetu tulionao madarakani ndani ya CCM na hata serikalini. Kwa hiyo ZeMarcopolo ndani ya JF ni kielelezo halisi na ushahidi wa fikra za watawala(sio viongozi)wetu na wale wanaofaidika kupitia watawala hao.
Kwahiyo kwa hiyo ni wajibu wa mbunge wa Pemba kuzungumzia maswala ya Tanzania bara lakini mbungewa Tanzania Bara hapaswi kuzungumzia maswala ya Pemba.
Najua hiyo ni sehemu ya sera ya chadema ya majimbo lakini haiko sahihi kwenye hilo.
Kweli nimeamini hata ufahamu wako umekaa kizali zali tu ndio maana hupati shida kutema pumba humu.
na CUF je?
Anzisha mada yako kuhusu CUF. Hapa tunaijadili CHADEMA. Inaonekana shule ulikuwa unafeli sana wewe kwa ajili ya kushindwa ku concentrate kwenye kitu kimoja :smile-big:
chadema imeshindwa kuitumia vizuri nafasi yake kama chama kikuu cha upinzani kwa manufaa ya taifa.
Hali ilianza kuonekana tangu awali baada ya uchaguzi mkuu ambapo chadema ilikataa kushikisha vyama vingine kwenye uongozi wa upinzani bungeni. Uamuzi huu wa chadema uliwasikitisha wapenda mabadiliko wengi.
Hii ni tofauti na chama cha wananchi cuf ambacho kiliishirikisha chadema kwenye uongozi wa upinzani bungeni katika bunge liliopita. Manufaa yake kwa taifa tumeyaona, bunge la tisa liliweza kusimamia hoja nzito za kitaifa na kuitetemesha serikali mpaka waziri mkuu akajiuzuru. Bunge hili la 10 lina wabunge wengi zaidi wa upinzani lakini hakuna mafanikio yoyote katika kujenga hoja!
Zaidi ya hilo, mara kadhaa chadema wamekuwa wakikimbia mijadala kwa mtindo wa kususa ambao haujawahi kuleta manufaa yoyote. Jambo kama la kususia hotuba ya mkuu wa nchi halikuwahi kutokea bungeni wakati cuf ilipokuwa chama kikuu cha upinzani kwenye bunge la 9.
Kadri siku zinavyoenda wananchi wanazidi kushuhudia jinsi chadema inavyoshindwa kuwakilisha maslahi ya taifa bungeni. Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba siku hizi wabunge wa chadema wakiongea taarifa pekee inayoweza kutolewa ni kwamba wamemchana kiongozi fulani.
Anayeongoza katika tabia hii ya kuchana ni sugu ambaye jana ameelezewa kuwa alimchana mbunge wa iramba mashariki. Huo ndio ulikuwa mchango wake kwenye bajeti ya waziri mkuu!!!
Kwa kweli inasikitisha pale input ya speech ya mbunge katika kuchangia bajeti ya waziri mkuu inapokuwa ni kumchana kiongozi! Mambo haya hayakuwepo bungeni wakati cuf ilipokuwa chama kikuu cha upinzani bungeni. Hamad rashid wa cuf alikuwa maridadi zaidi katika kusimamia shughuli na hoja za upinzani bungeni kuliko anavyofanya kiongozi wa upinzani wa bunge hili la 10.
Picha inayowekwa na chadema ni kwamba upinzani ni vurugu. Wananchi wastaarabu wanaanza kuchukizwa na tabia za uvunjifu wa kanuni na kumkosea heshima spika zinazofanywa na wabunge wa chadema. Hamad rashid wa cuf hakuruhusu hili, lakini kiongozi wa sasa wa upinzani bungeni anaona vurugu na kubishana na spika kama burudani.
Nikumbushe tu kuwa taarifa zilizopo zinaonyesha hakuna mbunge hata mmoja wa chadema aliyeweza kutekeleza ahadi zake alizotoa kwa wananchi jimboni. Kwahiyo wananchi wanaweza kuwa na imani na wabunge wa chadema iwapo wataona angalau bungeni wana michango yenye tija.
Kwavile jimboni wabunge wa chadema hawatekelezi ahadi na bungeni wanaenda kuchanana wananchi watakuwa hawana sababu ya kuchagua chadema. Hasahasa ikizingatiwa kuwa chadema kimekuwa ni chama kinachoainisha matatizo bila kutoa jinsi yoyote ya utatuzi.
Vilevile cuf watakuwa na sababu ya kuwaambia wananchi kuwa chadema wameharibu image ya upinzani bungeni - jambo ambalo ni kweli. Jambo hilo litaiwezesha cuf kuchukua kura nyingi za wapenda upinzani ambazo zingeweza kuwa za chadema katika majimbo ya tanznia bara. Kwa vigezo hivyohivyo chadema itaendelea kukosa kura za zanzibar.
Bottomline: Chadema imeligeuza bunge kuwa jukwaa la kampeni. Cuf walipokuwa wanaongoza upinzani bungeni walisimamia hoja kwa maslahi ya taifa. Tabia ya vurugu na kumkosea heshima spika inayofanywa na chadema ni mtaji wa kisiasa kwa cuf.
Ushauri: Chadema ijiepushe na tabia za mipasho mbele ya tbc mkiwa bungeni. Sugu apewe mafunzo maaluma ya kuchagua maneno ya kuongea bungeni itafaa zaidi iwapo hotuba zake zitapitiwa na mnyika kabla hajazisoma.
Mawazo yako yanavumiliwa kadri yanavyostahili.
Hata hiyo hoja ni jinsi vurugu za chadema bungeni zinavyoipa mwanya CUF kisiasa...
Na yule wa Nkasi anasema tulime bangi liwe zao la biashara...Bado yule wa Korogwe hajasema serikali itambue uchawi nkCHADEMA imechoka kiasi kwamba Mh. Sugu anachangia pumba bungeni na Mh. Nassari yeye hajui umuhimu wa Nyuki, kwa kweli 2015 CUF njia nyeupe kwao ya kuwa chama kikuu cha upinzani.
hatuwezi kushirikiana na vibaraka wa ccm. bora tuwe wachache wanao elewana bila kuzungukana. wewe utashirikiana na mbatia, lyatonga au ccm b?. mia