ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
CHADEMA imeshindwa kuitumia vizuri nafasi yake kama chama kikuu cha upinzani kwa manufaa ya taifa.
Hali ilianza kuonekana tangu awali baada ya uchaguzi mkuu ambapo CHADEMA ilikataa kushikisha vyama vingine kwenye uongozi wa upinzani Bungeni. Uamuzi huu wa cHADEMA uliwasikitisha wapenda mabadiliko wengi.
Hii ni tofauti na chama cha wananchi CUF ambacho kiliishirikisha chadema kwenye uongozi wa upinzani Bungeni katika Bunge liliopita. Manufaa yake kwa taifa tumeyaona, Bunge la tisa liliweza kusimamia hoja nzito za kitaifa na kuitetemesha serikali mpaka Waziri Mkuu akajiuzuru. Bunge hili la 10 lina wabunge wengi zaidi wa upinzani lakini hakuna mafanikio yoyote katika kujenga hoja!
Zaidi ya hilo, mara kadhaa CHADEMA wamekuwa wakikimbia mijadala kwa mtindo wa kususa ambao haujawahi kuleta manufaa yoyote. Jambo kama la kususia hotuba ya Mkuu wa Nchi halikuwahi kutokea Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani kwenye bunge la 9.
Kadri siku zinavyoenda wananchi wanazidi kushuhudia jinsi CHADEMA inavyoshindwa kuwakilisha maslahi ya taifa Bungeni. Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba siku hizi wabunge wa CHADEMA wakiongea taarifa pekee inayoweza kutolewa ni kwamba "wamemchana kiongozi fulani".
Anayeongoza katika tabia hii ya "kuchana" ni Sugu ambaye jana ameelezewa kuwa alimchana mbunge wa Iramba Mashariki. Huo ndio ulikuwa mchango wake kwenye bajeti ya Waziri Mkuu!!!
Kwa kweli inasikitisha pale input ya speech ya mbunge katika kuchangia bajeti ya Waziri Mkuu inapokuwa ni kumchana kiongozi! Mambo haya hayakuwepo Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni. Hamad Rashid wa CUF alikuwa maridadi zaidi katika kusimamia shughuli na hoja za upinzani Bungeni kuliko anavyofanya kiongozi wa upinzani wa Bunge hili la 10.
Picha inayowekwa na CHADEMA ni kwamba upinzani ni vurugu. Wananchi wastaarabu wanaanza kuchukizwa na tabia za uvunjifu wa kanuni na kumkosea heshima Spika zinazofanywa na wabunge wa chadema. Hamad Rashid wa CUF hakuruhusu hili, lakini kiongozi wa sasa wa upinzani Bungeni anaona vurugu na kubishana na Spika kama burudani.
Nikumbushe tu kuwa taarifa zilizopo zinaonyesha hakuna mbunge hata mmoja wa CHADEMA aliyeweza kutekeleza ahadi zake alizotoa kwa wananchi jimboni. Kwahiyo wananchi wanaweza kuwa na imani na wabunge wa CHADEMA iwapo wataona angalau Bungeni wana michango yenye tija.
Kwavile jimboni wabunge wa chadema hawatekelezi ahadi na Bungeni wanaenda "kuchanana" wananchi watakuwa hawana sababu ya kuchagua CHADEMA. Hasahasa ikizingatiwa kuwa chadema kimekuwa ni chama kinachoainisha matatizo bila kutoa jinsi yoyote ya utatuzi.
Vilevile CUF watakuwa na sababu ya kuwaambia wananchi kuwa CHADEMA wameharibu image ya upinzani Bungeni - jambo ambalo ni kweli. Jambo hilo litaiwezesha CUF kuchukua kura nyingi za wapenda upinzani ambazo zingeweza kuwa za CHADEMA katika majimbo ya Tanznia Bara. Kwa vigezo hivyohivyo CHADEMA itaendelea kukosa kura za Zanzibar.
Bottomline: CHADEMA imeligeuza Bunge kuwa jukwaa la kampeni. CUF walipokuwa wanaongoza upinzani Bungeni walisimamia hoja kwa maslahi ya taifa. Tabia ya vurugu na kumkosea heshima Spika inayofanywa na CHADEMA ni mtaji wa kisiasa kwa CUF.
Ushauri: CHADEMA ijiepushe na tabia za mipasho mbele ya TBC mkiwa Bungeni. Sugu apewe mafunzo maaluma ya kuchagua maneno ya kuongea Bungeni – itafaa zaidi iwapo hotuba zake zitapitiwa na Mnyika kabla hajazisoma.
Addendum:
Rais Kikwete aliposema kuna watu wamemuombea AFE kuna watu hawakuamini.
Sasa haya mnayoandika hapa yanadhihirisha kuwa kweli watu wa namna hiyo mpo.
Hizi ni hulka mpya kabisa mnazozileta vijana wa bavicha kwenye siasa!!!
Inasikitisha sana kwa sababu lengo la kunzishwa kwa bavicha na jinsi ilipo sasa na inakoelekea ni tofauti kabisa.
Bavicha siku hizi inatumiwa kama organ ya kuwasababishia watu vifo - INASIKITISHA...

.....Wewe unapaswa kufa kabisa.
Watanzania wengi wanakuombea ufe....
wengi tunakuombea usiku na mchana ufe tujue tumedondosha msaliti mmoja