Hiyo kesi ni muhimu sana kipindi hiki ambacho serikali ya awamu ya 5 inaonyesha dhahiri ina lengo la kuurejesha mfumo wa Chama kimoja.
Ushahidi wa wazi ni tukio la jana huko jijini Mwanza ambako wafuasi wa CCM waliruhusiwa kuandamana na baadaye kuhutubiwa na viongozi wao wa Chama wa mkoa.
Hiyo ni double standard ya waziwazi inayofanywa na Policcm ambao siku chache zilizopita walidiriki hadi kuwakamata viongozi wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, aliyekuwa akipita kwenye matawi mbalimbali ya Chadema akiwasalimia viongozi hao wa matawi, kwa madai ya kukiuka amri waliyoiita ya halali ya zuio la kufanya mikutano yoyote ya kisiasa.
Hata hivyo alipoulizwa RPC wa Mwanza, Ahmed Msangi, sababu za kuruhusu maandamano na mikutano wa CCM akadai kuwa hakuwa na taarifa kama kulikuwa na kitu kama hicho!!
Kumbe intelejensia ya Jeshi letu la Polisi, huwa inaishia katika kubaini matukio yatakayofanywa na vyama vya siasa vya upinzani pekee!!!!!