CHADEMA wafungua upya kesi dhidi ya Polisi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,843
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefungua upya kesi dhidi ya amri ya polisi ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa baada ya kuifanyia marekebisho hati ya awali ya mashtaka kwa kuwaondoa baadhi ya washtakiwa.

Mawakili wa Chadema Gasper Mwanaliela, John Mallya na Paul Kipeja waliwasilisha mahakamani hati mpya ya madai kwa kuondoa wadaiwa wawili ili kukidhi mahitaji ya kisheria.

Wadaiwa katika hati mpya ya mashtaka iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Awali, washtakiwa wengine walikuwa ni wakuu wa polisi Wilaya za Kahama, Maswa na Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Mssanzya

Chanzo:Mwananchi online
 
Hiyo kesi ni muhimu sana kipindi hiki ambacho serikali ya awamu ya 5 inaonyesha dhahiri ina lengo la kuurejesha mfumo wa Chama kimoja.

Ushahidi wa wazi ni tukio la jana huko jijini Mwanza ambako wafuasi wa CCM waliruhusiwa kuandamana na baadaye kuhutubiwa na viongozi wao wa Chama wa mkoa.

Hiyo ni double standard ya waziwazi inayofanywa na Policcm ambao siku chache zilizopita walidiriki hadi kuwakamata viongozi wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, aliyekuwa akipita kwenye matawi mbalimbali ya Chadema akiwasalimia viongozi hao wa matawi, kwa madai ya kukiuka amri waliyoiita ya halali ya zuio la kufanya mikutano yoyote ya kisiasa.

Hata hivyo alipoulizwa RPC wa Mwanza, Ahmed Msangi, sababu za kuruhusu maandamano na mikutano wa CCM akadai kuwa hakuwa na taarifa kama kulikuwa na kitu kama hicho!!

Kumbe intelejensia ya Jeshi letu la Polisi, huwa inaishia katika kubaini matukio yatakayofanywa na vyama vya siasa vya upinzani pekee!!!!!
 
Katika kusoma kwangu kote , sijawahi kuona mahali popote palipowahi kuandika DHULUMA IMEWAHI KUISHINDA HAKI , kama kuna kiongozi anayedhani ubabe wake utafanikiwa basi atakuwa amejidanganya vibaya sana !!!
 
HAWA POLISI WETU WANAJIDHALILISHA SANA KWA KUPOKEA KILA MAAGIZO YA CCM MWISHO WA SIKU WAO NDIYO WANAISHIA KUHANGAIKA NA KESI,KAMA WALIWARUHUSU CCM WAKAANDAMANA NA NA BAADAYE KUFANYA MKUTANO NA POLISI KULINDA HUO MKUTANO JE TUELEWE HAWA CCM NA POLISI LAO MOJA AU? HUU NI UKANDAMIZAJI WA WAZI KABISA
 
Katika kusoma kwangu kote , sijawahi kuona mahali popote palipowahi kuandika DHULUMA IMEWAHI KUISHINDA HAKI , kama kuna kiongozi anayedhani ubabe wake utafanikiwa basi atakuwa amejidanganya vibaya sana !!!
Hii kesi CHADEMA wanashinda mchana kweupe.
 
Aaa kumbe pale mara ya kwanza walikurupuka..sasa mbona wao huwa wanajiona wako makini kumbe ni mbwembwe tu.
 
Kwa kesi za aina hii, namkumbuka Mtikila kwa nguvu zote (R.I.P)
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimefungua upya kesi dhidi ya amri ya polisi ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa baada ya kuifanyia marekebisho hati ya awali ya mashtaka kwa kuwaondoa baadhi ya washtakiwa.

Mawakili wa Chadema Gasper Mwanaliela, John Mallya na Paul Kipeja waliwasilisha mahakamani hati mpya ya madai kwa kuondoa wadaiwa wawili ili kukidhi mahitaji ya kisheria.

Wadaiwa katika hati mpya ya mashtaka iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Awali, washtakiwa wengine walikuwa ni wakuu wa polisi Wilaya za Kahama, Maswa na Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Mssanzya

Chanzo:Mwananchi online

Hizi RUZUKU hizi na watashindwa nakupigwa fsini. Tusubiri
 
Naona mwanga na haki vikipatikana kupitia mahakama
 
Daima haki huwa inachelewa
 
Back
Top Bottom