Chadema wafanye nini sasa baada ya kuibiwa haki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wafanye nini sasa baada ya kuibiwa haki?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masauni, Nov 3, 2010.

 1. M

  Masauni JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imenisikitisha sana kuona CCM,ilivyopora haki ya watanzania. Sasa CHADEMA wafanye nini?
  Nina pendekeza mambo yafuatayo

  • Wadai tume huru ya uchaguzi na katika jambo hili wasiishie kulalamika bungeni tu bali wapeleke malalamiko kwa wafadhili(EU,UN,).Hao ndo wenye nguvu za kuwalazimisha serikali ya CCM.
  • Waendelee kuwaeleza wananchi kuhusu haki zao.Ufahamu wa watanzania bado ni mdogo sana, mpaka watu wa mjini uelewa wao ni mdogo.
  • wakifanya mambo hayo kwa nguvu kubwa, tunaweza kupata haki
   
 2. M

  Malembeka Shija Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanakalia msumari wa moto,na wewe unawashwa au?kama vipi kalia mirunda ya kujengea
   
 3. Vica

  Vica Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: May 27, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  jamani vipi matokea ya Segerea bado?
   
 4. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  Kuna masuala mengi ya kufanya baada ya haya matokeo.
  1. Viongozi wakae chini wafanye tathmini ya mchaakato mzima wa uchaguzi na hasa namna kura zilivyopigwa, kuhesabiwa na hatimaye kutangazwa. Katika hili waangalie katika majimbo yale wanayoona kuna ushahidi mkubwa wa fraud kufanyika kulikopelekea kuyakosa majimbo hayo kama vile jimbo la segerea, kibaha, na shinyanga mjini. Wakiwa na ushahidi mzuri basi wafungue kesi kupinga matokeo. Nasisitiza hili lifanyike kwa yale majimbo yenye ushahidi tu ili kuzuia kupoteza muda mwingi na gharama katika kusimamia kiesi ambazo mwisho wa siku mtashindwa tu.

  2. Jambo la pili la kufanya baada ya uchaguzi, ni kujaribu kuyatekeleza yale yote ambayo wabunge wa chadema waliyaahidi majimboni kwao kuwafanyia wananchi. Katika kutekeleza hili wabunge wa Chadema watarajie upinzani mkubwa saana toka serikalini. Serikali itafanya hivyo kuonyesha kuwa wapinzani hamna uwezo wa kutekeleza lolote bila serikali kuamua. Kama kutakuwa na kikwazo chochote toka serikalini katika kuyafkia yale mloyaahidi kwa wananchi basi rudi haraka saana kwa wananchi muwaeleze, hii itawasaidia saana hapo 2015. Kufanikiwa kwenu kuteleza mloyaahidi kwetu ndio uhakika wa ninyi kurudi tena 2015, au ndio kutengeneza njia ya kupotea kabisa na pia kuuwa kabisa upinzani bungeni.

  3. Chadema inabidi ijaribu kufanya kazi kwa karibu saana na vyama vingine vya upinzani vilivyo makini, mjaribu saana kupunguza kuhisiana vibaya, yaani chama kwa chama. Kumbukeni nyote mnataka kuwatumikia wananchi. Matokeo mengi yanayotoka ya ubunge, yanaonyesha wazi kuwa kama block ya upinzani ingeingia kwenye uchaguzi kama kambi moja kwa kusimamisha wagombea pale tu wanapkubalika napata ushawishi kusema upinzani ungepata majimbo mengi saana bungeni zaidi ya 170. Najua katika hili kuna matatizo yake, lakini pia kuna njia zake za kupambana. Hamuwezi kuungana kama chama kimoja, lakini mnaweza kukubaliana kuwa na mgombea mmoja tu atakaye chaguliwa na vyama vyote. Kulitimiza hili ni muhimu kuacha dharau kati ya chama kimoja dhidi ya kingine. Mimi naamini kuwa kama chama kina uwezo wa kuingiza mpinzani bungeni japo mmoja tu basi ni muhimu saana kuwa naye hasa katika kipindi cha uchaguzi kwa lengo la kuwa na viti vingi bungeni.

  3. Jambo la tatu la kufanya ni Chadema kutumia picha ya matokeo ya uchaguzi huu kutengeneza "STRATEGIC POLITICAL MAP" ya kuitumia kujiandaa na 2015 election. Maana matokeo ya mwaka huu yanaonyesha wapi Chadema inajulikana na kukubalika zaidi na wapi haijulikani . Map hiyo itasaidia kujua aina gani ya nguvu iwekwe wapi na kwa wakati gani. Tumeona namna ambavyo chadema haikufanya vizuri kama kanda ya mikoa ya Lindi na Mtwara, tabora, Singida, Dodoma, tanga, Rukwa na Kigoma.

  4. Jambo la nne ni kuwa Chadema inatakiwa ijipange na kuanza maandalizi rasmi ya uchaguzi ujao 2015 hivi sasa. Kwa chama chenye mipango mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi ujao. Katika hili kuna haja ya kufikiria saana jinsi ya kupata wagombea wa ubunge, kijumla au kimakundi kama vijana, walemavu, wazee,wasomi na watoto. Tumeona wote chadema ilivyokuwa na wakati mgumu kuwapata wagombea ubunge wa vitu maalumu wa wanawake. Hili linakichafua saana chama maana watu wasiokipenda wanapata nafsi ya kukikosoa vibaya.
   
Loading...