CHADEMA wadai kada wao amefichwa polisi Dar

CHADEMA wadai kada wao amefichwa polisi Dar

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,750
Reaction score
2,636
IMG-20250713-WA0065.jpg

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikidai kuwa kada wake Leonard Magere amefichwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro ametaka suala hilo waulizwe Idara ya Uhamiaji.

Magere ambaye ni mtaalamu wa Fedha na Uwekezaji wa CHADEMA, anadaiwa kukamatwa jana Julai 12 katika Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Julius Nyerere akijiandaa kusafiri kwenda nje ya nchi.

"Hadi saa 5 usiku jana, polisi walisema watamoeleka Kituo kikuu cha polisi (central) Dar es Salaam. Lkini leo asubuhi viongozi wa chama walipofika central wakaambiwa Magere hajafikishwa kituoni hapo," imesema taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo Julai 13.
Imeongeza kuwa, viongozi hao walishaur8wa kwenda kituo cha polisi cha uwanja wa ndege ambako nako hawakumkuta.

Alipoulizwa suala hilo, Kamanda Muliro ameshauri maswali hayo waulizwe Idara ya Uhamiaji.

Juhudi za kumpata msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Paul Msele hazikufanikiwa kwa kuwa simu yake haikupokelewa.
 

Attachments

  • IMG-20250713-WA0063.jpg
    IMG-20250713-WA0063.jpg
    306.2 KB · Views: 18
Mafwele muuaji aliyepewa jambia la kuua na MAJALIWA KASSIM MAJALIWA
Sasa analitumia jambia KUUA WATU waso na hatia
 
Back
Top Bottom