CHADEMA vunjeni UKAWA

CHADEMA vunjeni UKAWA

Kisendi

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
699
Reaction score
180
Kama kweli tunataka mabadiliko UKAWA ivunjwe tu kwa sababu zifuatazo:-

1. Kuna baadhi ya majimbo CHADEMA walikuwa na nafasi 2010 lakini leo wamewapa CUF na NCCR Mageuzi.

i) Segerea - Mpendazoe alikosa kiduchu tu
ii) Tarime - CHADEMA ina nguvu
iii) Serengeti - CHADEMA ina nguvu... na maeneo mengine mengi.

2. Urais NCCR Mageuzi na CUF wanataka.Swali la kujiuliza mwaka 2010 dr. Slaa alifanya vizuri sana.

Mimi binafisi sioni umuhimu wa kugombania nafasi ya Urais kama NCCR Mageuzi na CUF wanataka Urais. Ni heri UKAWA ukavunjwa ili CHADEMA waendelee na hakuna kulala.

Na watapata wabunge wengi tu watakosa Kusini na baadhi ya mikoa kama Tanga na Zanzibar.
 
Kinachosikitisha ni baadhi ya vyama kung'ang'ania majimbo ambayo hawajawekeza kabisa. Wakati CHADEMA wanafanya mikutano na kuhamasisha wananchi kujiandikisha, wao wapo majumbani kwao tu.

Hatuwezi kuota kwenda ikulu huku wenzetu wamekaa tu na hiyo nia dalili ya kugawa majimbo bure kabisa kwa CCM.
 
Segerea Mpendazoe alikosa kwasababu Wapinzani waligawana kura. i.e Jumla ya kura za Wapinzani zilikuwa zaidi ya CCM. Tarime CDM walikosa lakini kura za CDM + CUF zilikuwa zaidi ya CCM. The same scenerio kwa majimbo mengine. Je, nini kinachokufanya uamini kwamba 2015 hali kama hiyo haitatokea tena?

Lakini pia, lengo kuu la UKAWA ni kumuondoa mkoloni mweusi CCM madarakani, sio CDM kupata viti vingi vya ubunge. CDM ime sacrifice hayo kwa masilahi mapana ya Watanzania.
 
Kinachosikitisha ni baadhi ya vyama kung'ang'ania majimbo ambayo hawajawekeza kabisa.wakati cdm wanafanya mikutano na kuhamasisha wananchi kujiandikisha wao wapo majumbani kwao tu wamekalisha mbunye.Hatuwezi kuota kwenda ikulu huku wenzetu wamekaa tu na hiyo nia dalili ya kugawa majimbo bure kabisa kwa ccm

Unaweza kuyataja hayo majimbo mkuu, ili na sisi tupate mwanga.
 
Je wewe umekalia nini? Hivi huwezi changia hoja mpaka uporomoshe matusi.
Kinachosikitisha ni baadhi ya vyama kung'ang'ania majimbo ambayo hawajawekeza kabisa.wakati cdm wanafanya mikutano na kuhamasisha wananchi kujiandikisha wao wapo majumbani kwao tu wamekalisha mbunye.Hatuwezi kuota kwenda ikulu huku wenzetu wamekaa tu na hiyo nia dalili ya kugawa majimbo bure kabisa kwa ccm
 
Kwenye kuungana lazima ukubali kupoteza baadhi ya hazina zako ili kuongeza zaidi na kufikia malengo. Sasa hivi sioni vyama vingine vikihamasisha wapiga kura kuhusu kujiandikisha. Nadhani lazima mapambano yafanyike kwa hali zote kwa pande zote. Naunga mkono UKAWA
 
Jamani tuacheni ubaguzi, angalieni kenya wameunganisha nguvu wakafanikiwa sana! sasa tukiaanza kubaguana sasa hatutafika mahala. wananchi wapeni ukawa nchi ndio kauli mbiu wadau!
 
CUF na NCCR Mageuzi walivaba sana kujiunga na CHADEMA, time will tell karibuni. Mimi sina imani kabisa na hawa jamaa wa Ufipa maana wamekaa kiuchu uchu na usakatonge.
 
MAJIMBO TATA KWA UKAWA ! majimbo hayo ni-1. Segerea 2 Temeke 3 Ukonga 4 Ilala 5Ilala 6.Kinondoni 7.Kigamboni 8. Serengeti 9.Mafia 10.Morogoro mjini 11.Kilosa 12.Mtwara mjini 13.Vunjo ambalo kaachiwa kaachiwa Mbatia akapambane na Mrema.
 
Kisendi

wewe sheeenz zanzibar sio mkoa kua na adabu na baba zako
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli,mleta uzi ana pointi ya msingi sana lakini ngoja tu tuseme kuwa un apoungana unasacrifce baadhi ya tunu zako.Kwa mafano jimbo la Serengeti,katibu mkuu wa nccr mh.Mosena Nyambabe analing'ang'ania lakini ukiangalia,nccr haina hazina yoyote ktk hilo jimbo,haina hata ofisi moja ya tawi jimbo zima.

Na huyu mh.amekuwa akigombea ktk hili jimbo miaka nenda rudi lkn hajawahi kuwa tishio kwa ccm hata siku moja.Leo hii CDM imeimarika Serengeti,viongozi wa cdm vitongoji,vijiji na kata kila kona ya jimbo,vijana wa boda boda pale stendi ya Mugumu mjini kila wakilala wakiamka ni CDM leo unaenda kuwambia eti nccr ambayo hata hawajawahi kuujua huo msamiati hapo kabla.
 
Kisendi

ccm oyeee, safari hii mnanyolewa kipara bila kutia maji nywele tena kwa bati lenye kutu.
 
Last edited by a moderator:
Segerea Mpendazoe alikosa kwasababu Wapinzani waligawana kura. i.e Jumla ya kura za Wapinzani zilikuwa zaidi ya CCM. Tarime CDM walikosa lakini kura za CDM + CUF zilikuwa zaidi ya CCM. The same scenerio kwa majimbo mengine. Je, nini kinachokufanya uamini kwamba 2015 hali kama hiyo haitatokea tena?

Lakini pia, lengo kuu la UKAWA ni kumuondoa mkoloni mweusi CCM madarakani, sio CDM kupata viti vingi vya ubunge. CDM ime sacrifice hayo kwa masilahi mapana ya Watanzania.

Wewe kwa muono wako tu MTATIRO ATAFURUKUTA SEGEREA...JE ANAKUBALIKA....TATIZO NI KUKUBALIKA MAANA WASIWASI WANGU NI CCM KUSHINDA KWA KISHINDO SEGEREA
 
Kinachosikitisha ni baadhi ya vyama kung'ang'ania majimbo ambayo hawajawekeza kabisa. Wakati CHADEMA wanafanya mikutano na kuhamasisha wananchi kujiandikisha, wao wapo majumbani kwao tu.

Hatuwezi kuota kwenda ikulu huku wenzetu wamekaa tu na hiyo nia dalili ya kugawa majimbo bure kabisa kwa CCM.

Hata mimi hii kitu inanipa shida sana, anyway kwa sisi wakristo tunaamini Yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu. Nadhani katika hili inabid cdm nao wafe msalabani kwa ajili ya taifa letu. Hizo nafasi wacha wapate na hivyo vyama vingine ili lengo la kuitoa ccm lifanikiwe. Huko mbele ya safari tutaweka mambo sawa.
 
Mnajiita wapinzani huku mkicheza ngoma ya ccm, ukweli ni kwamba UKAWA ni Tumaini la sie wanyonge kuitoa ccm madarakani.

Hebu piga picha jukwaa moja Mbatia, Lipumba, Mbowe na Makaidi wakimnadi mgombea mmoja Urais nini kitatokea.

Kuuvunja UKAWA ni kurudi miaka Ishirini nyuma, na ukitokea huo Upuuzi tusahau kuing'oa ccm madarakani. Tutaanza kunangana wenyewe kwa wenyewe na kumsahau adui yetu mkuu ccm.

Tusijifanye vipofu angalia mfano mdogo ACT na Chadema, ilifika wakati wakawa wanajibizana wao kwa wao na kusahu kuwa wote lao ni moja kuing'oa ccm.

Tuache ubinafsi, sio uongo kuwa kupitia UKAWA hata wasipochukua nchi wapinzani wanaweza kuwa na viti vingi zaidi bungeni kuliko wakisimama kila Chama kivyake.!
 
Kwa kweli,mleta uzi ana pointi ya msingi sana lakini ngoja tu tuseme kuwa un apoungana unasacrifce baadhi ya tunu zako.Kwa mafano jimbo la Serengeti,katibu mkuu wa nccr mh.Mosena Nyambabe analing'ang'ania lakini ukiangalia,nccr haina hazina yoyote ktk hilo jimbo,haina hata ofisi moja ya tawi jimbo zima.

Na huyu mh.amekuwa akigombea ktk hili jimbo miaka nenda rudi lkn hajawahi kuwa tishio kwa ccm hata siku moja.Leo hii CDM imeimarika Serengeti,viongozi wa cdm vitongoji,vijiji na kata kila kona ya jimbo,vijana wa boda boda pale stendi ya Mugumu mjini kila wakilala wakiamka ni CDM leo unaenda kuwambia eti nccr ambayo hata hawajawahi kuujua huo msamiati hapo kabla.

Shida ndo hiyo. Kuna hatari ya kukosa majimbo mengi kwa ukawa. WATOE KWA MJIMBO KWA STATISTICAL ZA KARIBUNI NA 2010 ili tusogee. Kuishinda CCM sio kazi rahisi sana. We need to think and think
 
hata mimi hii kitu inanipa shida sana, anyway kwa sisi wakristo tunaamini yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu. Nadhani katika hili inabid cdm nao wafe msalabani kwa ajili ya taifa letu. Hizo nafasi wacha wapate na hivyo vyama vingine ili lengo la kuitoa ccm lifanikiwe. Huko mbele ya safari tutaweka mambo sawa.

ngoja tuuone. Tuombe uzima
 
Back
Top Bottom