CHADEMA: uongozi uko wapi hapa?

CHADEMA: uongozi uko wapi hapa?

The Boss unataka viongozi wa safishe nini?
Kama shonza alishavuliwa uanchama na bavicha unataka uongozi uingilie nini?

Unataka viongozi waanze kujibishana na wakina shonza?

Hatua stahiki zimesha chukuliwa na chama na watu wamepewa adhabu na kila mtu ana pokea adhabu kwa namna yake!

Shonza hawezi kuzuiwa kuongea au kuandika ana chotaka maana ameshavuliwa uanachama na sasa hivi ana tapatapa na wenzie na hilo halizuiliki!

Kwa akili za kawaida lazima tukubali kuongoza nchi ni kazi ngumu pengine kuliko zoote
kwa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu....sasa kama watu au mtu ambao wanajaribu
kuishawishi jamii kuwa wako tayari kwa kazi ya kuongoza Taifa unategemea kwamba
watu hao watakuwa 'makini' kwa jambo lolote lile dogo au kubwa linaloweza
'tia shaka' mbele ya macho ya watu wengine 'uwezo na utayari' wao wa kuendesha Taifa...

Kinachotokea BAVICHA sasa na huku Uongozi wa Taifa wa CHADEMA ukihushwa moja kwa moja au kukaa kimya
huku hali ya hewa ikizidi kuchafuka.....unajiuliza swali moja tu hapa..
'where is the leadership now'?

Hivi seriously hawaoni kuwa hii vurugu ya BAVICHA inaleta picha gani?

hasa kwa watu waliokuwa wanahitaji kushawishiwa kuwa kuna 'watu wenye uwezo wa kuongoza from CHADEMA'?

Kama chama tu kinayumba yumba na hakuna 'clear leadership in time of crisis ndogo kama hii ya BAVICHA'
Mtaweza kweli kundesha Taifa lenye watu millioni 45 wenye vichwa na vurugu tofauti?

Naona kama kundesha Taifa la watu milioni 45 ni ngumu zaidi kuliko kuendesha chama cha watu less than
two millions....sasa kama chama ni hivi...mnashawishi vipi uwezo wa kundesha Taifa?
 
Last edited by a moderator:
tafuta kitabu kichachosema ''the 48 laws of power'' kisha soma sheria namba 4.......kingine ni kwamba tamko lilishatolewa na kufanyiwa kazi na hatua kuchukuliwa na watu wakatimuliwa....haya unayoyaona leo hasa tamko la huyo shonza ni njia ya kutangatanga tu ....lakini kama hofu yako ni ukimya wa viongozi wa juu tafuta kitabu hich au google utapata jibu ..mambo mengine hayana mda wa kukupotezea mda.....jambo la shonza na wenzake lilishapatiwa tiba na ndio maana wngine wameanza kukwapua simu ...maisha huko mttaani magumu sana....
 
Chadema watakuwa wehu kumpa platform chokoraa wa kisiasa ,hakuna sababu ya kujustify na kucondone plot ya CCM ya kuonyesha kuna mgogoro Bavicha ambao haupo wasaliti wametupwa nje kwenye shimo la takataka wanafurukuta waache waendeleee kufurukuta wakichoka wataacha

Chadema kunastrategist wa hali ya juu hizo singo zilizozungumzwa kwa miaka kumi iliyopita zinakuwa recycled in another form haziwezi kuwababisha viongozi wanajua haya yanakotokea na yanakoelekea ,soon watawafanya wao wajisikie si ridhiki
Bahati nzuri manager wao Prezzo kwenye hsitoeia ya usaliti hajawahi kushinda hata moja ikiwemo matusi,actions,makala vyote vimebuma
nawashauri viongozi wa Bavicha waendelee na workplan zao waache masalia waendelee kujikaanga shame
 
Naijua CHADEMA tangu izaliwe hadi hapa ilipo leo. Nadiriki kusema kuwa kwa facts nilizo nazo, huu utakuwa upepo tu unapita! Lakini ni upepo unaohitaji umakini sana usitoke na paa la mjengo pale Kinondoni. Lipo tatizo la Washindani wa Chadema kuunganisha dots katika kuondoka kwa Wanachama Waanzilishi wa Chadema wenyeji wa Mkoa wa Mbeya kama vile yule Meneja mstaafu wa TCC, yule Founder Member kutoka Mwakaleli na kina Mary Kabigi, kama ushahidi pana tatizo la ukanda fulani kupendelewa katika nafasi za uongozi. Na shida kubwa ya siasa ni kwamba wakati mwingi maamuzi ya wananchi hayajipi nafasi kufanya analysis tosha kuona kama pengine hawa watu kutoka Mbeya walifanya makosa fulani ya kisiasa ndiyo maana hawakupewa nafasi muhimu za kiuongozi katika chama.

Mimi ninavyoona utakuwa upumbavu wa hali ya juu sana kuruhusu hatua yoyote linayoleta picha kuna ukanda unapendelewa katika kupewa nyadhfa ndani ya chama. Again...huu ni upepo, lakini ni upepo mbaya!

Naomba niungane na wale wanaohofu pana leadership problem katika hili tatizo tulilo nalo. Something must done, and quickly! Challenge ni kuibuka washindi katika Crisis hii, hata kama ni kutumia principle za compromise. Pride, au niseme ego, must always be managed--whether it is an individual person's ego, a company ego, or some organization's ego. Nina mashaka maamuzi yanayotakiwa kufanywa hapa yatagusa sana ego ya chama. Save the party--hata kama ni kucompromise kitu fulani! Mshindani asipewe nafasi kutumia tatizo hili kwa faida yake...

Mwanangu The Boss wala usihofu. Kama CCM inaweza kuendesha nchi tena kwa autopilot hata CDM wanaweza ingawa it is a calamity. Nionacho hapa Tanzania ni kwamba tunapata viongozi wanaofanana na watanzania. Sipendi kutoa hitimisho la jumla ila nchi yetu inahitaji kubadilika vinginevyo kila kibaka atakuja na kutuibia kuanzia babu wa Loliondo, wachungaji na mashehe uchwara hadi wanasiasa uchwara. Waingereza husema; show me your friends I will tell you who you are. CDM ikubali ina crisis tena ya kujitakia. Kwanini kuruhusu nguo chafu kufuliwa hadharani badala ya kuzifua mapema? Mwanangu hapa una hoja.
 
Kwa akili za kawaida lazima tukubali kuongoza nchi ni kazi ngumu pengine kuliko zoote
kwa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu....sasa kama watu au mtu ambao wanajaribu
kuishawishi jamii kuwa wako tayari kwa kazi ya kuongoza Taifa unategemea kwamba
watu hao watakuwa 'makini' kwa jambo lolote lile dogo au kubwa linaloweza
'tia shaka' mbele ya macho ya watu wengine 'uwezo na utayari' wao wa kuendesha Taifa...

Kinachotokea BAVICHA sasa na huku Uongozi wa Taifa wa CHADEMA ukihushwa moja kwa moja au kukaa kimya
huku hali ya hewa ikizidi kuchafuka.....unajiuliza swali moja tu hapa..
'where is the leadership now'?

Hivi seriously hawaoni kuwa hii vurugu ya BAVICHA inaleta picha gani?

hasa kwa watu waliokuwa wanahitaji kushawishiwa kuwa kuna 'watu wenye uwezo wa kuongoza from CHADEMA'?

Kama chama tu kinayumba yumba na hakuna 'clear leadership in time of crisis ndogo kama hii ya BAVICHA'
Mtaweza kweli kundesha Taifa lenye watu millioni 45 wenye vichwa na vurugu tofauti?

Naona kama kundesha Taifa la watu milioni 45 ni ngumu zaidi kuliko kuendesha chama cha watu less than
two millions....sasa kama chama ni hivi...mnashawishi vipi uwezo wa kundesha Taifa?


Jamani si kila kitu kinahitaji majibu, vurugu ya bavicha imekwisha baada ya baadhi ya watu kutimuliwa but kila kukicha masalia wanakuja na matamko yao hivi tukisema uongozi wa juu uanze kujibu kila hoja si tutafanya kazi hiyo kila siku? maana mwingine anasema Wabunge saba wa CDM kukihama chama hicho, mwingine amefukuzwa lakini bado anadai yeye ni bado mwanachama halali wa CDM, Mwingine anasema oooh! barua ya kumfukuza Shoza imekosewa, mwingine anahoji kwanini Dr. Silaa haudhurii misiba ya wasanii? alot of rubish.

Kimsingi yote hayo yanakihusu chama but mi nathani is better viongozi wa kitaifa wakadeal na mambo muhimu ya kitaifa kuliko kuhangaika na hawa vijana wachache wenye uchu wa madaraka kwasababu msingi wa fujo za BAVICHA ni vijana walioshindwa uchaguzi kujiunga pamoja na kuanza kukichafua chama, sidhani kama itakuwa busara kuwa bussy nao while kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya.
 
Tatizo ni watu wa kawaida wanapata tafsiri gani juu ya uongozi wa CHADEMA.
Inawezekana hapa JF watu wakaelewa juu ya tuhuma na kufukuzana. Lakini ni mamilioni angapi ya Watanzania wasiopita
JF watakavyopokea haya?

Kwa mfano tuhuma lukuki juu ya M/Mwenyekiti BAVICHA zimetolewa JF......huk nje hakuna anayejua zaidi ya Taarifa kwamba wasaliti wamefukuzwa.

CDM ni muafaka sasa kujipanga upya kama wanataka kuonekana kama chama kiongozi.
 
Sasa unataka Viongozi wa juu wa chadema wahangaike kujibizana na masalia wa Chauma na ambao pengine walishavukuzwa ila bado tu kudhibitishawa kuvukuzwa kwao na vikao vya juu vya Chama? Waache waendelee kuonyesha sura zao kamili baada ya kujificha kwa muda mrefu hadi walipofichuliwa na Kamanda Saanane.
 
Tatizo ni watu wa kawaida wanapata tafsiri gani juu ya uongozi wa CHADEMA.
Inawezekana hapa JF watu wakaelewa juu ya tuhuma na kufukuzana. Lakini ni mamilioni angapi ya Watanzania wasiopita
JF watakavyopokea haya?

Kwa mfano tuhuma lukuki juu ya M/Mwenyekiti BAVICHA zimetolewa JF......huk nje hakuna anayejua zaidi ya Taarifa kwamba wasaliti wamefukuzwa.

CDM ni muafaka sasa kujipanga upya kama wanataka kuonekana kama chama kiongozi.

exactly my point
thank you...
 
Jamani si kila kitu kinahitaji majibu, vurugu ya bavicha imekwisha baada ya baadhi ya watu kutimuliwa but kila kukicha masalia wanakuja na matamko yao hivi tukisema uongozi wa juu uanze kujibu kila hoja si tutafanya kazi hiyo kila siku? maana mwingine anasema Wabunge saba wa CDM kukihama chama hicho, mwingine amefukuzwa lakini bado anadai yeye ni bado mwanachama halali wa CDM, Mwingine anasema oooh! barua ya kumfukuza Shoza imekosewa, mwingine anahoji kwanini Dr. Silaa haudurii misiba ya wasanii? alot of rubish.

Kimsingi yote hayo yanakihusu chama but mi nathani is better viongozi wa kitaifa wakadeal na mambo muhimu ya kitaifa kuliko kuhangaika na hawa vijana wachache wenye uchu wa madaraka kwasababu msingi wa fujo za BAVICHA ni vijana walioshindwa uchaguzi kujiunga pamoja na kuanza kukichafua chama, sidhani kama itakuwa busara kuwa bussy nao while kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya.

Kufukuza watu sio dawa ya kila tatizo
hasa kama watu hao walishashika madaraka kwenye chama...
Wanakuwa na 'credibility' wanapoongea hata kama ni uongo
watu wenye busara wanajua hili...
 
The Boss unataka viongozi wa safishe nini?
Kama shonza alishavuliwa uanchama na bavicha unataka uongozi uingilie nini?

Unataka viongozi waanze kujibishana na wakina shonza?

Hatua stahiki zimesha chukuliwa na chama na watu wamepewa adhabu na kila mtu ana pokea adhabu kwa namna yake!

Shonza hawezi kuzuiwa kuongea au kuandika ana chotaka maana ameshavuliwa uanachama na sasa hivi ana tapatapa na wenzie na hilo halizuiliki!


Je unaamini vikao vya kumfukuza vilikuwa vya halali?
sheria na kanuni zoote zilifuatwa?
Image ya chama kwa nje haijaathirika?
na why all the time kuwe na 'wasaliti'?
mara madiwani,mara masalia.mara hivi...huoni ina reflect chama kinavyoongozwa?
 
tafuta kitabu kichachosema ''the 48 laws of power'' kisha soma sheria namba 4.......kingine ni kwamba tamko lilishatolewa na kufanyiwa kazi na hatua kuchukuliwa na watu wakatimuliwa....haya unayoyaona leo hasa tamko la huyo shonza ni njia ya kutangatanga tu ....lakini kama hofu yako ni ukimya wa viongozi wa juu tafuta kitabu hich au google utapata jibu ..mambo mengine hayana mda wa kukupotezea mda.....jambo la shonza na wenzake lilishapatiwa tiba na ndio maana wngine wameanza kukwapua simu ...maisha huko mttaani magumu sana....


Na wewe soma no 5
uone kama mgogoro huu na mingine haina madhara kwa chama..
 
The Boss kwa kweli kuna haja ya uongozi wa juu wa Chadema kuzungumzia hali ilivyo katika baraza la vijana la chama hicho.

Sisi washabiki wa Chadema tunajikuta tukijiuliza maswali mengi bila majibu

Hawajui waseme nini kinachotokea sasa hawakukitegemea, ubaguzi kitukibaya sana,na haya ndio malipo yake.

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Last edited by a moderator:
Kufukuza watu sio dawa ya kila tatizo
hasa kama watu hao walishashika madaraka kwenye chama...
Wanakuwa na 'credibility' wanapoongea hata kama ni uongo
watu wenye busara wanajua hili...


Lakini kuwabembeleza sio dawa pia, imagine kama wewe ni baba mwanao anaenda kukuzungumzia nyumba ya jirani kuwa "Baba ni mjinga sana, hatusaidii chochote" unayasikia maneno hayo halafu jioni mtoto huyohuyo anarudi nyumbani kwako na unawatoto wengine wanaokuheshimu wanasikia kaka au mdogo wao anavyokusanifu unategemea kujenga familia ya namna gani.
 
Naijua CHADEMA tangu izaliwe hadi hapa ilipo leo. Nadiriki kusema kuwa kwa facts nilizo nazo, huu utakuwa upepo tu unapita! Lakini ni upepo unaohitaji umakini sana usitoke na paa la mjengo pale Kinondoni. Lipo tatizo la Washindani wa Chadema kuunganisha dots katika kuondoka kwa Wanachama Waanzilishi wa Chadema wenyeji wa Mkoa wa Mbeya kama vile yule Meneja mstaafu wa TCC, yule Founder Member kutoka Mwakaleli na kina Mary Kabigi, kama ushahidi pana tatizo la ukanda fulani kupendelewa katika nafasi za uongozi. Na shida kubwa ya siasa ni kwamba wakati mwingi maamuzi ya wananchi hayajipi nafasi kufanya analysis tosha kuona kama pengine hawa watu kutoka Mbeya walifanya makosa fulani ya kisiasa ndiyo maana hawakupewa nafasi muhimu za kiuongozi katika chama.

Mimi ninavyoona utakuwa upumbavu wa hali ya juu sana kuruhusu hatua yoyote linayoleta picha kuna ukanda unapendelewa katika kupewa nyadhfa ndani ya chama. Again...huu ni upepo, lakini ni upepo mbaya!

Naomba niungane na wale wanaohofu pana leadership problem katika hili tatizo tulilo nalo. Something must done, and quickly! Challenge ni kuibuka washindi katika Crisis hii, hata kama ni kutumia principle za compromise. Pride, au niseme ego, must always be managed--whether it is an individual person's ego, a company ego, or some organization's ego. Nina mashaka maamuzi yanayotakiwa kufanywa hapa yatagusa sana ego ya chama. Save the party--hata kama ni kucompromise kitu fulani! Mshindani asipewe nafasi kutumia tatizo hili kwa faida yake...

Compromise ,compromise..
naona hili neno halipo kabisa CHADEMA.....
 
Je unaamini vikao vya kumfukuza vilikuwa vya halali?
sheria na kanuni zoote zilifuatwa?
Image ya chama kwa nje haijaathirika?
na why all the time kuwe na 'wasaliti'?
mara madiwani,mara masalia.mara hivi...huoni ina reflect chama kinavyoongozwa?

labda niulize tu, ivi kuna mwanachama yeyote mwenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro aliyewai kufukuzwa?
 
Lakini kuwabembeleza sio dawa pia, imagine kama wewe ni baba mwanao anaenda kukuzungumzia nyumba ya jirani kuwa "Baba ni mjinga sana, hatusaidii chochote" unayasikia maneno hayo halafu jioni mtoto huyohuyo anarudi nyumbani kwako na unawatoto wengine wanaokuheshimu wanasikia kaka au mdogo wao anavyokusanifu unategemea kujenga familia ya namna gani.

Unaweza usimbembeleze lakini uki overreact heshima yako itashuka mno
unaweza mkanya na kumdharau kwa muda...sio ku panic na ku overreact...
usisahau in politics 'uhuru wa kuongea na kukosoana' ni very essential kwa ukuaji wa demokrasia..
hakuna ku 'worship watu'...watu wote ni 'fair game' kwa kukosolewa
 
sijaona kama kuna mgogoro mkubwa mpaka ifikie hatua ya ku-judge kuwa CHADEMA watashindwa kuongoza nchi! kwanza wale wote waliokuwa wanaleta sintofahamu BAVICHA tayari walishaondolewa, hawa akina Juliana wanaokuja hapa na hoja za kimipasho sio viongozi wa BAVICHA tena,,,kifupi CHADEMA hapa imeonyeshs ukomavu wa hali ya juu!

Bado mmoja babu slaa na vp alis atoa maelezo ya kujikoposha 140m? Wapiga kura tunataka kujuwa hili.

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
labda niulize tu, ivi kuna mwanachama yeyote mwenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro aliyewai kufukuzwa?

Dah kwa swali hili, subiri matusi tu.

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Back
Top Bottom