Jana katika mkutano mkubwa sana wa hadhara uliondaliwa na UKAWA ktk viwanja vya mbugani wilaya ya Nyamagana jiji la Mwanza, kwa kweli yaliongelewa mambo mengi na mazuri sana kwa mustakabali wa taifa letu, na umati ule uliokuwepo pale uwanjani uliamini kuwa Ukawa ndo tumaini jipya la Watnzania......Lakin kwa siasa za nchi yetu mimi sio mfuasi wa chama chochote cha siasa naomba nieleweke kwa hilo.
Katika hotuba ya Mnyika aligusia pia suala la mgomo, akinukuu kauli ya m/kiti mh, Mbowe alisema kwamba:- maandamano ni lazina yawepo, iwe polic wametoa kibali au hapana....Mnyika akachambua kwa kusema:- unaweza kuandamana hata kwa simu tu.....akatoa namba za Mh, Samwel Sitta na za Andrew Chenge ili wananchi iwe kwa kutuma sms au kuwapigia waheshimiwa hawa na kuwaeleza kupinga kwao kuendelea na Bmk....
Sasa wasiwasi wangu ndo unaijia hapo kuwa itawasbabishia wengi matatizo kwa maana badala ya mtu kuelezea kwa kina hoja zake najua wengi wataishia kuwaporomoshea matusi hawa viongozi, sasa ndo nimeuliza kwa hilo mh, Mnyika alikuwa yuko sawa kutangaza namba za mtu hadharani?