Hawana mbinu mpya kwasababu zama si zao, na kila zama na kitabu chake
Si suala la mbinu tena ni suala linalohitaji surgical precision right away
The time is up, help Mbowe exit the door with honor. Mbowe must go ab initio
Chadema, it's time you express your gratitude to Hon Mbowe for his tireless effort and immense contributions to your party and country at large, and remind him it's time to pack and go!
Yaani recruitment ya wasanii ndilo kipaumbele chao ! it's disgusting"Freeland, post: 19861431, member: 67846"]
Nilipigwa na butwaa kubwa sana baada ya kuona yanayotokea...especially hili la wasanii
Kuna mambo mengi sana ya kitaifa yanaendelea. Utashangaa chama kinachopaswa kuiweka serikali mguu sawa kimekaa kimya as if kila kitu ni 'poa' tu. Hawana agenda tena. Mambo chungu nzima hawana habariHuu ni wakati mwafaka wa Mbowe kukaa Pembeni...Chama kimesinyaa....as if hakina watu maridadi na wenye uelewa
Afadhali kingekuwa kinaenda, nadhani kimesimama kabisa na kimevia. Hakuna kinachofanyikaChama kinaenda enda tu
Hakuna tena hoja nzito ingawa hoja nzito za kujadili zipoTulizoea CHADEMA ya hoja.....nzito nzito...Tulizoea CHADEMA ya kutoa Plan B ya matatizo ya nchi yetu
Nitashangaa kama atakayesema kinafanya nini. Real suprisedLakini CHADEMA ya sasa hata haijui inafanya nini
Hawaoni ukweli huu kwasababu hakuna anayeweza kufikiri zaidi.Huu ni wakati mzuri sana wa CHADEMA kupaa kwa sababu magufuli ni anapwaya sana katika nafasi yake
Hawazioni, wapo bize na bongofleva.Hivi blunders zote alizofanya magufuli wanashindwa ku capitalize na kuwa chachu ya growth yao
Timu zao zinakwenda solo.This is 2017...Miaka 2 tu hadi mwaka wa uchaguzi mkuu imebaki.....Ukiuliza CHADEMA wanafanya nini..hakuna kitu
No! akae pembeni right now si 2018 wakati uharibifu umekamilika.Suluhisho liliopo sasa Mbowe akae Pembeni mwaka 2018........Chama kikae chini kifanye tathimini yakinifu ya 2015....
Timu iliyopo ivunje, iundwe mpya ili kuleta mabadiliko ya kweli yanayokidhi haja na nyakati.Chama kiunde upya timu yake....Turudi kwenye chama cha hoja
Na wataendelea kumtafuta mchawi juu ya paa la nyumba wakifumbia macho joka uvunguni.Tunaenda kwenye uchaguzi mwingine katika mazingirra ya kikatiba yaleyale..Itakuwa ajabu sana kama CHADEMA watakaa kimya siku zote hadi 2020 na kuenda katika uchaguzi mwingine katika mazingira yaleyale
Mkuu Nguruvi3 kwa leo umesema Jambo la msingi sana ambalo tumeliona kwa muda mrefu sasa
Nilipigwa na butwaa kubwa sana baada ya kuona yanayotokea...especially hili la wasanii
Nianze ulipomalizia. Moja ya kazi kubwa za Mh Mbowe ni kutoa chama kutoka 'club' ya wastaafu na kuwa chama cha siasa kilichobeba matumaini ya Watanzani. Kazi hiyo ni pamoja na recruitment ya vijanaNilipokuja swala la Chadema kukosa muelekeo kwa kweli ninakuunga mkono, ni kweli Mh.
Mbowe amefanya mambo mengi, kuna mambo ambayo yalikuwa mazuri sana, na kuna mambo ambayo yalikitia chama doa kubwa, Mh. Mbowe baada ya matokeo ya uchaguzi basi ilikuwa ni lazima yeye na team yake wajihudhuru lakini kama walivyo viongozi wa kiafrika wote swala la kuwajibika ni mwiko...
Chadema si Chadema ile iliyobeba umoja na matumaini, si Chadema ya viongozi waliokuwa na ujasiri si Chadema iliyokuwa inamsemea mnyoge bali hii ni Chadema iliyokosa mwelekeo.
Ni wakati sasa Mh. Mbowe awaachie vijana wake aliyowandaa zaidi ya miaka 10 kwani huu ni wakati wao na Chadema kinawahitaji sana. Ni wakati wa Mnyika, Mwalimu, Lissu, Lema, kuongoza chama..Mh. Mbowe uliyofanya yanatosha sasa pumzika tuone matunda ya malezi yako.
Mkuu una hoja nzito sana naomba nizipitie kwa maoni yangu binafsiMimi binafsi nimeshangazwa na ujio wa Wema CHADEMA.
kitu kimoja ambacho tunapaswa kujiuliza na labda tukipata jibu itatusaidia kuelewa kinachoendelea sasa... "Watanzania/wapiga kura wanataka nini?",
wanapokwenda kupiga kura wanaangalia nini kutoka kwa mwanasiasa?
Uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo CCM ilikuwa imegubikwa na kashfa za richmond, epa, meremeta, vijisenti n.k. lakini bado wananchi sio tu waliipa kura ccm lakini wagombea wote waliotuhumiwa na kashfa walichaguliwa bungeni (lowasa, chenge...). Hii inatufundisha nini?
Watanzania wanataka nini? Hoja nzito pekee zinatosha?
Watanzania hawa tunaowasema kweli wako tayari kwa mabadiliko?
Tuangalie uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo UKAWA walimsimamisha Lowasa matokeo yalikuwaje upande wa upinzani kulingana na uchaguzi wa mwaka 2010?
Kuna wakati nawaza na kufikiri labda sisi wanazuoni tunaojadiliana humu pia hatuelewi watanzania wanataka nini au wanatafuta nini kutoka kwa wanasiasa. Tunaweza kuwalaumu kwa haki kabisa chadema kwa kwenda kinyume na misimamo yao ya awali kwa kuwapokea kina Wema, Lowasa na wengineo, lakini LABDA narudia LABDA tunapaswa kutathmini upya watanzania wanataka nini.
Mkuu, yote uliyosema ni sahihi. Lakini bado kuna jambo moja muhimu sana kuliko hayo yote uliyoyaeleza nalo ni ELIMU NA UELEWA WA WANANCHI.Mkuu una hoja nzito sana naomba nizipitie kwa maoni yangu binafsi
1. Watanzania wanataka nini? Jibu, si wanataka nini bali wamechoshwa na nini
Wanataka mabadiliko ya kweli katika mfumo wa kuendesha nchi nje ya CCM
CCM wanatambua, kushinda kwao chaguzi si kwasababu wanapendwa au kukubalika
Wenyewe wanatambua ndiyo maana wana program ya kukibadili chama
Katika hili uwepo wao wanatambua ni nafasi ya kuwa na serikali na vyombo vyake
wanatambua bila 'misuli' hawana chao na katika kuhakikisha hilo wameenda mbali zaidi
1. Wamemiliki vyombo vya umma, wakadhibiti taasisi zikiwemo za demokrasia
2. wamefanikiwa kumiliki mhimili mmoja,RC ametukumbusha
Mwingine upo mahututi. Unaweza kujiuliza nafasi za kukaimu nafasi zinaeleza nini.
3. Katika kuhakikisha udhibiti, sasa CCM/serikali yake wameingilia vyama vya kitaaluma
Ni kuhakikisha kama kuna sehemu, basi taasisi au mhimili unakuwa na 'total collapse'
4. Wamedhibiti vyama kwa marufuku ya mikutano. Wanajua hawana uwezo wa kujibu hoja, umma wa leo si wa kudanganyika kwa 'amani na utulivu'
Wanachi hawana uwezo wa kukwepa 'kushindwa' kama tulivyoona kule visiwani
CCM ikitaka 'uwe' unavyotaka utakuwa, wana tools zote za kuwezesha hayo kufanyika
Kwa mtazamo wangu, matokeo hayawezi kuwa kipimo cha wananchi wanataka nini
Tungekuwa na chaguzi katika mazingira halisia, tungeweza kujiuliza.
Kwa haya ya leo, ni ngumu
Hayo nayo yanajibu hoja kuwa wananchi wanapiga kura kitu gani?
Inawezakana wanapiga kura wanachokitaka, lakini si lazima wapate wanachokitaka kama tulivyoonyesha hapo juu
Hoja ya uchaguzi kugubikwa kwa rushwa na watu wakarudishwa Bungeni
Hili nalo linaelezwa vema na yote hapo juu, wakitaka liwe linakuwa, wana tools zote
Hoja kubwa inayohitimisha hayo hapo juu ni kuhusu Katiba.
CCM hawataki kabisa kuzungumzia katiba. Hii iliyopo ndiyo inawapa udhibiti wa kila aina
Mabadiliko yoyote yatakayoweka taasisi, mihimili , na demokrasia huru itawaumiza.
Hawana ushawishi mbele ya wananchi. Kama ni mgonjwa anapumuliwa mashine.
Mgonjwa huyo ukimwambia umeme uzimwe kufanya mabadiliko atakutandika kofi hapo ICU.
Hoja ya Chadema kulaumiwa: Hii haina siri, wakati Chadema inasimama kama opposition party iliweza kufanikisha mengi ikiwemo matumizi mabaya ya vyombo vya dola, mihimili kuwa huru kwa kiasi n.k.
Katika wakati tulio nao, inaonekana kana kwamba hakuna mbinu wala fikra mpya
Ikumbukwe hawa kama CCM wanadhima na wajibu kwa umma ndio maana kuna ruzuku
Tatizo linalojitokeza ni kama vile Chadema hawajui wafanye nini.
Kuna mbinu nyingi ikiwemo kujiweka katika nafasi ya chama mbadala kikiongelea mambo ya kitaifa na kimataifa. Kikiratibu na kuwa semeo la watu wasio na nafasi.
Ikitumia udhaifu unaojitokeza katika kujipambanua
Katika hali hii ya 'bongofleva' kuwa leading news, sidhani kama wapo njia sahihi.
Ndiyo maana tunasisitiza ni wakati wa kukaribisha fikra mpya, na wakati ni sasa
Tusemezane
Mkuu ukirudi nyuma katika bandiko langu, nilisema ili kuhakikisha CCM inabaki madarakani wameamua 'kuua' taasisi zinazoojenga uelewa, na kuhakikisha elimu ya Uraia haiwafikii wananchi. Ndiyo maana halisi ya ''marufuku'' ya mikutanoMkuu, yote uliyosema ni sahihi. Lakini bado kuna jambo moja muhimu sana kuliko hayo yote uliyoyaeleza nalo ni ELIMU NA UELEWA WA WANANCHI.
Kama kuna mahala ambapo utawala wa ccm umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuchota akili za watu
Ujinga wa mtanzania ni mtaji mkubwa wa ccm, wanatumia mbinu nyingi chafu na mtaji mkubwa wa wananchi wenye uelewa mdogo na uoga wa kufanya maamuzi magumu.
Ndio maana nikatoa mfano wa 2010 ambapo upinzani ulipiga kelele za ufisadi lakini hazikusaidia na wale wale waliotuhumiwa wakarejea nafasi zao za ubunge.
Unafikiri walipita kwa rushwa 100%? Sidhani!
Kuna wakati wananchi wakishaamua wanamtaka fulani haijalishi hata kama ana makandokando ya aina gani wataenda nae hivyo hivyo... Kama ikivyokuwa kwa bwana Trump huko marekani!
Kama kuna eneo la kufanyia kazi nchini kwetu ni elimu ya uraia, kuwawezesha raia kujitambua na kutambua na kusimamia haki zao, wajiamini bila woga... Tukifanikiwa hapo tutapiga hatua kubwa kwenye kujenga demokrasia imara.
Kuna kundi ambalo kisheria lina platform. Hili ni la vyama vya siasa, ndipo hoja ya Chadema inapoingia.
Kwavile vyama vya siasa vina platform kazi ya elimu ya Uraia kwao ni wajibu na haki
Mkuu na hapa ndipo hoja yangu ilipo kuanzia mwanzo, kwamba, badala ya kushughulika na mambo madogo kama tunayosikia sasa, walipaswa kusimama kidete ili marufuku na madhila mengine yaondoke na kuwawezesha kuendelea na kazi. Kukaa kimya kwasababu kuna marufuku si jawabu la tatizo."Mwalimu, post: 19901963, member: 11689"]Watatekeleza vipi wajibu huo wa kutoa elimu ya kiraia wakati mikutano ya hadhara imepigwa marufuku?
Au katika mazingira ambayo tamko la mwanasiasa linaweza kusababisha kushitakiwa kwa uchochezi?
Ni jukumu letu sote lakini pia ukumbuke hoja yangu ya awali kuwa kuna jitihada za kuua au kudumaza taasisi zinazoshughulika na demokrasia.Vipi kuhusu nafasi ya wadau wengine kwenye kutoa elimu ya uraia?Au jukumu hili ni la vyama vya kisiasa pekee? ....na kwa muktadha wa mjadala huu tuseme ni jukumu la vyama vya upinzani? ...manake suala la elimu ya uraia sio kwa maslahi ya chama tawala...
Ni kweli raia wana mchango wao katika hili, lakini pia umehoji uelewana pengine tujiulize hawa Raia wasio na uelewa wanawezaje kuwa na uelewa kwa hili la elimu?Lakini najaribu kuangalia upande wa pili juu ya mazingira ya kisiasa kwa ujumla na nafasi yetu sisi kama raia kwenye ushiriki wa kikamilifu. Sisi wote ni mashahidi jinsi mchakato wa katiba mpya ulivyovurugwa kiasi kwamba hakuna matumaini kama utakuja kufufuka tena.
Si ndio maana tuna mjadala hapa kama sehemu ya mchango wetu? Ni kweli Raia wana nafasi lakini usisahau swali lako, uelewa ni kiwango gani? Maana unaweza kuwa na milioni 30 wenye uelewa wakawa 3,000! Pamoja na hayo 3,000 wanaweZa kusaidia milioni 30, lakiji je wana platform?Ndio maana bado naendelea kujiuliza swali hili tena na tena; nini nafasi yetu kama raia kwenye ujenzi wa demokrasia imara? Au tunasubiri ujio wa "messiah" kutoka chama cha upinzani aje kutuokoa?
Kuna kuishiwa pumzi na kuzembea kuvuta pumzi.Hivi vyama vya siasa vitafanya juhudi kwa kadiri ya uwezo wao na inawezekana vikafika mahala vikaishiwa pumzi... Sisi wananchi/raia tunasimama kwenye nafasi yetu?
Wakuu Nguruvi3 na JingalaFalsafa nawasoma vyema.
Mimi naamini mabadiliko yatakuja kwa njia mbili,
Njia ya kwanza ni njia ya kistaarabu kupitia sanduku la kura
AU
Njia ya pili ni pale wananchi wakichoka wakaamua kuanzisha mabadiliko Tunisia style bila kusubiri wanasiasa na vyama vyao vya upinzani.
Kwa upande wetu njia ipi tutatumia ni juu yetu sisi kwa namna tunavyoendenda sasa... vyama vya siasa vikishindwa basi wananchi wenyewe wakichoka wataamua basi imetosha!
Wakuu Nguruvi3 na JingalaFalsafa nawasoma vyema.
Mimi naamini mabadiliko yatakuja kwa njia mbili,
Njia ya kwanza ni njia ya kistaarabu kupitia sanduku la kura
AU
Njia ya pili ni pale wananchi wakichoka wakaamua kuanzisha mabadiliko Tunisia style bila kusubiri wanasiasa na vyama vyao vya upinzani.
Kwa upande wetu njia ipi tutatumia ni juu yetu sisi kwa namna tunavyoendenda sasa... vyama vya siasa vikishindwa basi wananchi wenyewe wakichoka wataamua basi imetosha!