^1
Hivi Tanzania ufisadi umefanyika katika swala la Richmond tu?
Halafu kitu ambacho sijapata ufafanuzi wa kutosha ni Richmond (ufisadi wa Lowassa) ilizaa Dowans na Dowans ni mkataba wa kifisadi lakini mpaka sasa serikali inaendelea kulipa Dowans pamoja na kujua kuwa Dowans imetokana na Richmond ambayo ni ufasadi wa Lowassa.. Sasa swali ambalo hata wewe nafikiri utakuwa nalo kichwani Je kwanini serikali iendelee kulipa Dowans hali wanafahamu ni mkataba wa kifisadi na ulitoka kwa fisadi Lowassa? Hiki kigugumizi cha nini?
Swali la pili hivi Tanzania tatizo la ufisadi ni Richmond tu? Kama kuna matatizo mengine ambayo ni makubwa zaidi ya Richmond tena ambayo hata Magufuli anahusishwa, ni kwanini haya hayaongelewi linaloongelewa ni Richmond tu?
Je hatufahamu kuwa katika wizara ya Ujenzi bil.265 zimetoweka bila maelezo yeyote?
Na je tunamaelezo gani kuhusu nyumba za serikali pamoja na kuuzwa kwa bei ya kutupwa lakini nyingine ziligawiwa kwa nyumba ndogo?
Tunapojadili ufisadi wa Lowassa ambaye ni mgombea rais kupita Ukawa, basi tujadili hata ufisadi wa Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM.. hama sivyo tutakuwa tunapendelea upande mmoja na upande wa pili kuufanya kuwa mtakatifu wakati sivyo..
Mwalimu,
Nilikuwa sijaona hii reply yako. Sijui kama umenielewa nilivyosema Slippery Slope. Namaanisha haya mambo ya kusema mambo yenye national interest yameongelewa ndani ya kamati kuu wamekubaliana bila kutoa specific details ni mteremko wa kuteleza sana. Hiyo ndio tabia ya CCM inayokataliwa sasa hivi. Wamefanya hivi kwenye mikataba mbali mbali, hawataki kutoa details za content ya mikataba wanaishia tu kusema tumesaini mkataba!
Nikisema majibu hayaridhishi ni kweli kuwa hayaridhishi and that is being fair to both sides kwa sababu hiyo ni FACT. List of Shame haikutangazwa kwenye kamati kuu. Iitangazwa hadharani, kujisafisha toka kwenye list of shame ni lazima kufanyike hadharani. Kama kweli kuna hard evidence Lowasa ametoa to convince kamati kuu kwa nini isiwe wazi tuachane na hizi mambo ya Lowasa na Richmond ibaki CCM na Richmond. Ugumu uko wapi kwani??
Haya mambo yanakuwa repeatative mpaka yanachosha. Point sio kuwa Lowasa anachukiwa sana na wenye maoni kama yangu, HAPANA. Tatizo CCM bado kuna mafisadi wengi sana, hii ya Lowasa bila kuhojiwa inaset a loop hole huko mbeleni watu wezi waachie tu kwa sababu wamejieleza kwenye kamati kuu bila kutoa maelezo ya maana nini hasa kimesemwa huko kamati kuu. Na huko kamati kuu kuna watu sio malaika. Jamani kwa nini hamni lioni hili suala!
Wanasema "The End, justify the Means"! But in politics there are no Ends, there are just Means. Watanzania tuwe makini, we are setting precedence kwenye serikali ijayo on how mafisadi wa EPA, Meremeta, Escrow etc will be dealt with!! Again SLIPPERY SLOPE.
Nadhani hujawaelewa hao wanaosema hivyo.Kweli LOWASA amebadilisha wengi,kwa kisingizio cha mabadiliko.. ETI watu wanauliza eti ufisadi ni RICHMOND tu,kwahiyo ndio nini,ugeugeu ni usaliti
Bavaria,
Ukipata bunge jingine ya "Wanaokubali, waseme Ndio" NDIYOOOOOOOO , ukaja kulalamika hapa. Ntakuja kukumbusha uhai ukiwepo mungu akipenda. It begins with you.
Alinda,
I think you are missing the point here. Hakuna mjadala wa kusema eti Lowasa ndio fisadi peke kwenye nchi hii, wala hakuna mjadala wa kuwa Dowans, Meremeta, Escrow, EPA, kuuza nyumba za serikali sio ufisadi. Au kuwa upi ulikuwa ufisadi mkubwa zaidi. Sidhani kuwa kuna anaesema hivyo, atleast i know i am not saying that. Ukiwa katika kundi la kunguru halafu ukajitangaza kuwa wewe ni njiwa lazima utegemee watu watakao uhoji huo u'njiwa wako. Sasa ukiianza kujitetea kwa kuwauliza mbona hamuwaulizi wale kunguru wengine kama vile unaonewa unakuwa unatia mashaka kwenye huo u'njiwa wako unaouhubiri.
Leo hii Magufuli akijidai kuibuka na kusema eti zile nyumba alipata amri toka juu, nae pia atakuwa kikaangoni kama alivyo Lowasa. Nasikitika kuwa kwenye mjadala huu unataka kujadili ufisadi wa Magufuli, labda kama sijaelewa huu mjadala unahusu nini au somehow ume evolve into something else completely. Huu mjadala unasema CHADEMA/UKAWA na uwekezaji usiotabirika. Naelewa ni kwa sababu gani issue ya Dr. Slaa imekuwa valid kuongelewa humu kwa sababu yeye ni matokeo ya mwanzo kabisa ya huo uwekezaji unazungumziwa.
Dada angu labda uniambie unataka tu uwasikie wadau wakimkaanga Magufuli na madudu yake, lakini sidhani kama ndio mada hasa inayozungumziwa hapa. Nimeona sehemu umemshauri Nguruvi aanzishe mada ya kuwalinganisha Lowasa na Magufuli kwenye uchaguzi huu, sasa kwenye huo mjadala wadau wakiendelea tu kuongelea Richmond bila kusema hivyo vingne na mimi ntaungana na wewe kukemea huo ubaguzi wa kihoja.
Mkuu Bavaria nadhanimuhimu ni kubadili mind set za watu.
Nakubaliana na GalaxyS3 kuwa lazima watu watambue umuhimu wa viongozi wao pale walipo
Kama unadhani haliwezekani labda ungejiuliza lini katika historia ya nchi hii mawaziri wakuu wawili wameondoka chama tawala? Kwanini unadhani ni impossible na lini unadhani utakuwa mwanzo wa kubadilika kama si leo hii?
Wanaukumbi.
Hii imekaaje Lowassa akiomba kura Kanisani.
https://www.youtube.com/watch?v=rJl2zsTKrA4&feature=youtube_gdata_player
Cc: JokaKuu, Pasco, Barubaru, Mkandara, FaizaFoxy, Mag3, Nguruvi3, Mshume Kiyate, Jasusi Zakumi, Mzee Mwanakijiji, NasDaz, Rev. Kishoka, GalaxyS3 TUJITEGEMEE, ZeMarcopolo, njiwa, The Boss, Kapwela, Mipangomingi, Waberoya, Nyenyere,
Wapi na lini nilimshamehe Lukuvi? najua sasa hivi hamuwezi kuona makosa ya Lowassa kwa mahaba nadhani baada ya uchaguzi tutakumbushana hizi kauli za kuomba kura Kanisani...msamehe tu.
..kama uliweza kumsamehe Lukuvi, why not Lowassa?
..Magufuli naye ana rekodi ya kuongea kilugha kwenye shughuli za kiserekali. Je, hakuna mushkeli hapo?
..ushauri wangu ni kwamba tujikite kwenye sera na ilani za wagombea.
Don't read too much into it.Wanaukumbi.
Hii imekaaje Lowassa akiomba kura Kanisani.
https://www.youtube.com/watch?v=rJl2zsTKrA4&feature=youtube_gdata_player
Cc: JokaKuu, Pasco, Barubaru, Mkandara, FaizaFoxy, Mag3, Nguruvi3, Mshume Kiyate, Jasusi Zakumi, Mzee Mwanakijiji, NasDaz, Rev. Kishoka, GalaxyS3 TUJITEGEMEE, ZeMarcopolo, njiwa, The Boss, Kapwela, Mipangomingi, Waberoya, Nyenyere,
Don't read too much into it.
Wapi na lini nilimshamehe Lukuvi? najua sasa hivi hamuwezi kuona makosa ya Lowassa kwa mahaba nadhani baada ya uchaguzi tutakumbushana hizi kauli za kuomba kura Kanisani.
Jasusi;
Kwanini tusi-read. Je inawezekana CDM wamemtosa Dr. Slaa kwa sababu mkatoliki?
Mkuu mnashangaa nyie lakini mimi hainishangazi kabisa. Na najua watu watasema mimi mdini lakini ndio hali halisi (Reality) na ndivyo Edo alivyo. Hakuomba aombewe tu ila kasema ni zamu ya Warutheli na ndio kauli yake!..Wengi wanamsikia tu hawajui ya Nigeria na Ujarumani..Wanaukumbi.
Hii imekaaje Lowassa akiomba kura Kanisani.
https://www.youtube.com/watch?v=rJl2zsTKrA4&feature=youtube_gdata_player
Cc: JokaKuu, Pasco, Barubaru, Mkandara, FaizaFoxy, Mag3, Nguruvi3, Mshume Kiyate, Jasusi Zakumi, Mzee Mwanakijiji, NasDaz, Rev. Kishoka, GalaxyS3 TUJITEGEMEE, ZeMarcopolo, njiwa, The Boss, Kapwela, Mipangomingi, Waberoya, Nyenyere,
Wanaukumbi.
Hii imekaaje Lowassa akiomba kura Kanisani.
https://www.youtube.com/watch?v=rJl2zsTKrA4&feature=youtube_gdata_player
Cc: JokaKuu, Pasco, Barubaru, Mkandara, FaizaFoxy, Mag3, Nguruvi3, Mshume Kiyate, Jasusi Zakumi, Mzee Mwanakijiji, NasDaz, Rev. Kishoka, GalaxyS3 TUJITEGEMEE, ZeMarcopolo, njiwa, The Boss, Kapwela, Mipangomingi, Waberoya, Nyenyere,
..mbona Magufuli naye amesema aombewe?
..tangu anachukua fomu Magufuli amekuwa akisema aombewe.
..kwanini hukulalamika wakati huo, unalalamika sasa hivi?
Kwani CDM hakuna wakatoliki wengine? Kwanini Dr. Slaa tu?
Kwa faida ya Wanaukumbi unaweza kutuwekea audio au video clip ya Magufuli akiomba kuombewa Kanisani ili ashinde urais kama Mkatoliki?..mbona Magufuli naye amesema aombewe?
..tangu anachukua fomu Magufuli amekuwa akisema aombewe.
..kwanini hukulalamika wakati huo, unalalamika sasa hivi?
Hamna tatizo mtu yeyote kuombewa haya maneno mbona ujayasema.Nimesikiliza clip yote sijaona alipoomba kura, nimesikia anaomba aombewe, labda kama nime miss habari kamili
Mkuu mnashangaa nyie lakini mimi hainishangazi kabisa. Na najua watu watasema mimi mdini lakini ndio hali halisi (Reality) na ndivyo Edo alivyo. Hakuomba aombewe tu ila kasema ni zamu ya Warutheli na ndio kauli yake!..Wengi wanamsikia tu hawajui ya Nigeria na Ujarumani..
Kama aliweza kurudisha shule na Hospital zilizojengwa na Mkoloni Mjarumani mikononi mwa kanisa lake atashindwa nini? Yeye Mrutheli, Mbowe sijui, Mtei sijui, Wakaskazini wengi sijui...kwa nini anapewa support kubwa hivyo sijui!. Panapofuka moshi kuna moto! Mimi ningependa tu kujua huyu Gwajima Askofu mzima ameingiaje katika uongozi wa Chadema au UKAWA hadi awe mshauri na msemaji wao?
- Unategema nini kitaandaliwa hapo? Nimeandika haya najua yatakuja mashambulizi ya hali ya juu kwa sababu watu hawatazami reality, wanataka kudanganyana na bikra ya ndimu! Udini upo mkuu wangu na hautakwisha kirahisi...