Alinda , kama utakuwa umetusoma katika yale mabandiko 4, tumemnukuu Dr Slaa akisema 'Gwajima alimpigia simu na kusema, Lowassa kakatwa, sasa nini cha kufanya? Hiyo tu inaonyesha kulikuwa na maongezi yaliyokuwepo, alichokifanya Gwajima ni kumtaarifu rasmi kuhusu matokeo ambayo wote walikuwa wanayasubiri.Alinda;13848277] Ndio Sumaye, Masha au kiongozi yeyote yule anapotaka kuhamia chama fulani huwa kuna mawasilina kabla.. Hivi unafikri Sumaye aliamka asubuhi na kusema leo naamia Chadema bila kuwa na mawasiliano na viongozi?
Hivi inakuingia akili Gwajima anyanyue simu na kwambia Dr.Slaa kuwa jamaa ameishakatwa na Dr. Slaa ajibu kuwa akaongee na Mwenyekiti? Kama ni hivi nilitegemea Dr.Slaa ajibu kuwa amekatwa kwa sababu ya ufasidi wake au ajibu kitu chochote si kusema aongee na Mwenyekiti? Hii sentensi ya Dr. Slaa inazdhhirisha alichongea Lissu ni kweli kwamba kabla ya Lowassa kukatwa kulikuwa na maongezi kati ya DR,Slaa, Gwajima na Lowassa...
Na katika simu ya Gwajima Dr. Slaa hakusema kuwa alimuombea kujiunga na Chadema bali alimpigia simu kumpa taarifa ya kukatwa! na Dr, Slaa anajibu kuwa aongee na Mwenyekiti sasa kama hawakuwa na mazungumzo kabla basi hii kauli ya niongee na mwenyekti ilikuwa ya nini?
Haya pia tumeuliza. Ukisikiliza Dr Slaa alivyoongea kwa hisia na hasira kuhusu ufisadi, hakuna mtu angetegemea hata kuwa na wazo la kumpigia simu mwenyekitiKwani wakati Gwajima anampigia Dr. Slaa simu ya kumpokea Lowassa, huyu Dr. Slaa hakufahamu kuwa Lowassa ndio yule yule ambaye alikuwa anatutangazia kuwa ni fisadi? na kama alipigiwa na Gwajima simu alishindwa kumwambia hapana sisi Lowassa ni kapi na sisi hatuchukui makapi?
Mzee Mwanakijiji , Alinda anakualika hukuHili Swali nilielekeze kwa Mzee Mwanakijiji maana anaweza kutupa maelezo ambayo yanaweza mwanga kidogo..
Ni kwanini Dr. Slaa alimkaribisha Lowassa Chadema?
Ni kweli , lakini pia mantiki na hasa kauli za Dr zinatoa uelekeo mkubwaTukubali tu kwamba kwa hali ilivyo sasa lolote linaweza kuzungumzwa kwa lengo la kutuliza/kuondoa athari/hasara itayatokana na kauli za Dk. SLAA jana....Mengi yatazungumzwa lakini ukweli wanaujua Slaa, Mbowe, Gwajima na Tundu Lissu
Intriguing questionsWana duru, naomba kuuliza hivi Mchungaji Gwajima ana mamlaka gani ndani ya Chadema mpaka wamruhusu kushiriki kuwachagulia mgombea urais.
Na tatizo la Dr.Slaa na Lowassa ni kakaribishwa Chadema kama mwanachama wa kawaida au kusimamishwa kama mgombea urais wa Chadema.
Ahsanteni.
Mkuu mbona kila kitu kinajadiliwa kwa upna wake?Hili jukwaa la great thinkers nalo mmeligeuza jukwaa la kampeni na propaganda.
Swala la Slaa kumkaribisha Lowassa Chadema sio big deal.
Tatizo ni kumsimamisha agombee urais.
Hata kule CCM walipomkata Lowassa hawakumfuta uanachama na hata angegombea ubunge wasingemkata kama ilivyo 1995 ambapo alionekana ana upungufu wa kimaadili kwa nafasi ya urais lakini akapitishwa kugombea ubunge.
Kwahiyo sioni tatizo Slaa kumkaribisha Lowassa kama mwanachama wa kawaida kuongeza nguvu kwenye timu ya kampeni.
Kama vyama vimekubali kuungana ingawa vinatofautiana itikadi, hakuna tatizo kumkaribisha mtu mmoja. Tatizo ni mtu huyo mmoja mgeni anapopewa nafasi ya kuamua hatma ya chama.
Kuhusu kuwa 'f'ocal point'' , ukisoma maelezo yake ' Gwajima alimpigia simu na kwamwambia, amekatwa sasa tufanye nini""
Hapa inaonyesha kulikuwa na mawasiliano endelevu kuhusu suala hilo
Kuhusu masharti, ukimsoma anasema 'tulipokuwa tunakwenda katika kikao nilikuwa na msimamo wangu' Hivyo ni vema kusema alikuwa na msimamo tayari nje ya vikao . Si jambo baya lakini lazima liunganishwe na mlolongo mzima wa habari
Masharti aliyoweka ni Lowassa kukana CCM, kujisafisha kuhusu Richmond na kueleza anakwenda chama gani
Kukana CCM halikuwa jambo gumu, kueleza anakwenda wapi halikuwa jambo gumu. Pengine ugumu ulikuwa wa Richmond
Tuliwahi kuuliza kama analysis ilifanyika ya kutosha. Sasa hilo ni moja ya hoja zake nzito, lakini haliondoi ukweli kuwa Lowassa angesema kilichotokea basi Slaa angekuwa na mtazamo tofauti.
Inaelekea alikubaliana naye kuanzia mwanzo na wala hakuona ufisadi.
Hoja ya ufisadi ameieleza mwisho baada ya kueleza ushiriki wake. Hapo huoni kuna walakini?
Kuhusu Lowassa kuja na watu, hili nalo tumelihoji mapema sana. Tulisema inakuwaje CDM wana kura za maoni wakati huo huo wanasema wana mtaji? Tulizungumza kuhusu asset and liability.
Tunaweza kusema kwa dhati, tumezungumzia hili kabla ya Slaa. Na bado linazizima masikioni mwa wengi
Asante sana GalaxyS3 kwa mchango wako nzuri ambao kwa namna moja au nyingine umenipa mwanga kuhusu ujio wa Lowassa ndani ya Chadema, pamoja na hayo bado sina mashaka na Dr. Slaa...
Kwanini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu:
Kwa jinsi Dr. Slaa alivyomueleza Lowassa jana, hivi kulikuwa na umhimu wa yeye kuwa "mposaji" wa Lowassa kuingia Chadema? Hivi hakuona kuwa kitendo cha Lowassa kuwa mwanachama wa kawaida tiyari kilikuwa kinatia doa kubwa ndani ya Chadema?
Na kama katibu mkuu anawajibu wa kulinda chama chake, kuhakikisha kuwa kila kiongozi anafuata maadili ya chama, hivyo basi inapotokea mtu anayetaka kujiunga na chama kwa minajri ya kugombea urais (kama ulivyoeleza hapo juu) lakini maadili yake ni machafu mtu huyu hakupaswa hata kujadiliana naye maana anaelewa kuwa ni fisadi na chama chake hakipokei mafisadi..Kwa hili tusimtetee Dr. Slaa tatizo limetoka kwake.
Na huu mjadala wa Gwajima Dr. Slaa na Lowassa hakuanza baada ya Lowassa kukatwa bali ulianza muda mrefu na ndio maana Gwajima alipompigia simu " alimwambia kuwa jamaa kakatwa" na Dr, Slaa akajibu niongee na Mwenyekiti kwa hii sentesi inaonyesha kuwa walishapanga kuwa akikatwa tu basi aje Chadema.
Nafikiri tuangalie haya mambo bila upendeleo unapompeleka mtu sehemu fulani iwe kwenye chama au kazini au sehemu yeyote ile basi ili apokelewa kutatokana na jinsi ulivyomuelezea kwa wanachama/au boss/Mwenyekiti wako. Haiwezekani leo ulete mwanachama ambaye anampango wa kuwa mwakilishi wa chama/kampuni yenu mwenye madoa doa na baaadaye usema "nimemleta nyie ndio waamuzi wa mwisho" Jamani kama ninafahamu fulani ni wezi/jambazi/fisadi tena fisadi kwanini nimpe hata nafasi ya kuongea na boss wangu?
Kama Dr. Slaa hasingekuwa anamfahamu Lowassa vizuri juu ya ufisadi wake na akaja kufahamu baada ya kuwa ameishamtambulisha katika chama na hapo pia ningemuelewa lakini si sasa, alimfahamu vizuri kuwa Lowassa ni fisadi, alifahamu vizuri kuwa chama chake kinapingana na ufisadi na Lowassa na yeye ndiye alikuwa mpiga debe wa Lowassa kujiunga na chadema kuingia. Jamani jamani wanasiasa kuweni na aibu tena kwa watu wenye umri kama Dr. Slaa kwa kweli inasikitisha.
Mbowe anaweza kulaumiwa kwa mengi lakini kwa jinsi alivyouhandle mgogoro huu na katibu mkuu wake ameonyesha kiwango cha juu cha ustaarabu, uvumilivu na ukomavu wa kisiasa. Chadema na Ukawa walikuwa wanapitia kipindi kigumu sana katika kufikia muafaka wa nani atapepea bendera yao kwenye uchaguzi huku muda ukiwa hauko upande wao.
Inapotokea mnatofautiana kimtazamo kwenye maamuzi fulani ni uungwana "kukubaliana kutokukubaliana/agree to disagree", na hiki naamini ndicho Mbowe alichomaanisha aliposema katibu mkuu amepumzika na atawakuta mbele ya safari. Pengine alikuwa na matumaini kwamba pamoja na kutofautiana kwao wanaweza kufikia muafaka kwenye masuala mawili matatu kwa mustakali mwema wa upinzani nchini.
Bahati mbaya Mheshimiwa Slaa ame-react vingine kabisa!
.... Ndio maana tunasema reaction yake haikuwa na ulazimaGalaxyS3,
..ppl r just reacting to what Dr.Slaa did.
..viongozi wa cdm kusema Dr amepumzika ilikuwa ni juhudi tu kuepusha haya ambayo Dr alifanya jana.
..bahati mbaya Dr didnt see it that way, badala yake aliona huo ni UWONGO na UZUSHI dhidi yake.
..Dr angetumia approach aliyofanya Prof.Lipumba sidhani kama tungekuwa tunamjadili yeye binafsi badala ya hoja zake.
..kwangu mimi Dr did not show CLASS/UNYENYEKEVU/UKOMAVU. Sijui kazi ya PR firm iliyoandaa mkutano ule ilikuwa ni nini haswa.
Alinda,
Ukilisema hivyo unapingana kabisa na misingi ya kidemokrasia. Katika justice, ndio maana hata convicted killers bado wanakuwa na haki ya ku appeal. D katika CDM inasimamia Demokrasia. Sasa kusema Slaa kwa sababu tu alidecide Lowasa ni mchafu hakuwa na haja ya kusemezana na mwenyekiti wake that is a slippery slope! Pili, hili suala aliletewa na rafiki yake and probably mtu ambaye (at the time) alikuwa anamuheshimu,.
kwa hiyo alilipeleka lakini tayari akijua kwa misingi ya chama chake itakuwa ni ngumu kwa huyu mtu kupita. Boy, was he surprised!! Nukta yangu ya msingi hapa ni kuwa, kila mtu ana haki ya kusikilizwa bila kujali tuhuma zake hata kama kuna lundo la ushahidi juu ya hizo tuhuma. Hiyo ndio MISINGI. Hakuna kucut corners, inatakiwa kufuatwa kikamilifu hasa hasa ukiwa una deal na watu usiowakubali ili usiwe muonevu. .
Mimi sijui ile nadharia kuwa Slaa alimpigia debe Lowasa unaitoa wapi ndugu yangu. Kama nilivyokujibu hapo juu, vyama vya siasa sio vya watu fulani. Vina viongozi wanaoviongoza kutokana na katiba za vyama hivyo. Mtu yoyote anahaki ya kujiunga na chama chochote hilo liko wazi. Maamuzi kwenye vyama hufanywa kwa hoja na sio visasi, kuchukiana wala kubagua. Ukiona hukubaliani na maamuzi ya wengi ndani ya chama chako na huwezi kukaa kimya, unajitoa kwenye hicho chama. Na hicho ndicho alichofanya Slaa jana. Sidhani kama kulikuwa na kupiga debe hapa.
Alinda , kumbe ni kuanzia May wapo katika maongezi. Naunganisha na ile kauli ya 'amekatwa Dodoma, tunafanyaje'Kama alifahamu msingi ya chama chake kuwa hakiwezi kumpitisha mtu kama Lowassa je alishindwa nini kumwambia Gwajima ukweli? Hiyo heshima gani inayokushinda kusema unachoamini na kusimamia misingi ya chama chako. Maongezi ya Gwajima alianza tangu May hivyo alikuwa na muda mzuri wa kutafakari na kuona je Lowassa anafaa kujiunga na Chadema ua hafai? na kama aliona kuwa hafai angemwambia Gwajima ukweli, kama alisimama mbele ya mamilion wa watanzania na kusema Lowassa hafai alishindwa nini kusema haya akiwa na Gwajima?
Je alitaka Lowassa awe mgombea urais?
Je alitaka Lowassa awe katika kampeni zake?
au alitaka Lowassa kuwa mwanachama wa Chadema kama walivyo wanachama wengine na kama ni hivi nini faida za kuwa na Lowassa.. Na je nani alimtafuta nani je ni Lowassa alimtafuta Dr. Slaa kupitia Gwajima au ni Dr. Slaa alimtafuta Lowassa?
Naombeni wanajamvi tuunganishe dot.