CHADEMA UK yazidi kuvurugika, M/kiti na Katibu vijana na Katibu muenezi waamua kumfuata Lukosi CCM

Kama ilivyotabiriwa Tsunami kubwa ya wafuasi wa chadema wameanza kuhamia CCM,
Leo hii tayari
mwenyekiti wa vijana
Katibu wa vijana
Katibu mwenezi
wote hawa wamechukizwa na siasa za kihuni za chadema za kufukuzana kama kuku na kuamua kumfuata kiongozi wao CHRIS LUKOSI CCM
Inasemekana kuwa wanachama wengi wamechukizwa sana na kitendo alichofanyiwa m,uasisi wao wa tawi la UK
Kma mnavyojua hakuna mwanaume alieweza kusimama na kusema anafungua tawi UK mpaka Lukosi alipofanya hivyo
Habari nyingi zinafuata kwani kwa taarifa zilizothibitishwa ni kuwa Lukosi atafanya press release jumamosi akiwa na kundi lake kubwa la wanachama na viongozi walioamua kurudi CCM.
wanachama+wapya+wakiwa+na+Makelele.JPG

ASILIMIA 75 YA UWAONAO HAPO JUU WAMELETWA NA LUKOSI CHADEMA
Mods hata mkifuta huu uzi haisaidii kwani tayari blogs zote zimepewa na zitaurusha usiku wa leo kwa hiyo ni bora muache tuu watu wasome, kufuta thread sio suluhisho. mbona ccm huwa inaumbuliwa hapa hamfutii?

Chadema ni taasisi sasa kama nyie mliingia kumfuata mtu, ina maana elimu yenu haijawasaidia. Kama mlifuata sera na malengo ya CDM hata kama angetoka Mbowe msingemfuata. Mimi siwatofautishi na wale vijana wa Mwanza wanaodhani kutoa matamko kwenye vyombo vya habari kukashifu viongozi wa juu wa chama ndio kutawaongezea umaarufu.

Kuweni SMART ukombozi unahitaji ujasiri sio kuyumbishwa na visenti vya CCM.
 
chama cha mabishoo wanasubiri miujiza wawe matajiri hakiwezi kudumu.kila kukicha wanatafuta wapi kuna mapochopocho ya wakubwa wakadowee wataondoka wengi maana matarajio yao yanafifia

naisubiri siku ya kesho kuona movies iitwayo " lukosi missing in action" toka alipobandikwa uwenyekiti jamaa akadhani ameula. Asijue kuwa yeye ndo alikuwa ameliwa. Mi nashindwa kuelewa kitu hapa, lukosi anadai asilimia 75% uliwaiingiza yeye. Lakini hatujui ni asilinia 75% ya nini??? Wanachama au makenge???. Alafu wakati unawaiingiza uliwaaambia nini mpaka wakubali kukufuata huko???.

Kuna msemo "sour grapes". Sioni kinachoweza kumfanya mtu anganganie kulumbana na genge la watu ambao anawaita "mission town"! Kati ya ha wachadema uk na lukosi kuna kitu hatukifahamu hapo , maana lukosi katimuliwa baruti huko, lukosi naye kapandisha mashetani na id kibao,mapicha kebekebe, what is going on???. Lukosi mie nilishakushauri,kuwa huku kwetu hatutimuani kwa style hiyo sisi tunaustaarabu fulani ambao ni wa kipekee. Karibu mjomba huku hatuna kenge wala mamba, sisi wote ni ccm tatizo ni cdm. Karibu mnyalukolo !!!!".
 
Wamefuata maslahi binafsi hakuna cha itikadi,maana ingekuwa hivyo wasingerudi ccm,bali wangebaki bila chama.Kama wanarudi ccm,waulize ni nini kimebadilika huko ccm ambacho kimewafanya waamuwe kurudi huko?Ndo akili za mbayu wayu hao.

Labda walikuwa wanasubiri mazingaombwe ya kubadili Sekretarieti ya SISIEMU. Sioni ambacho kiliwatoa SISIEMU na kukimbilia CHADEMA na kurudi SISIEMU within 6 months. Zaidi ya JK kulamba shavu kwa Ray C, nini ambacho kimewafurahisha huko particularly ki-sera!!
 
Juzi juzi tu mlikua mnawaita makamanda na kuwamwagia sifa kibao leo wamekua hawafai. Siasa zitawashinda nyie.

majebere, walioshindwa siasa ni lukosi na hao mamluki wenzie. cdm ni sera sio mtu. lzm tutengeneze nidhamu ktk chama.
 
LUKOSI hafunguki ila kanisimulia haya machache tu na nikamuelewa
Nilikuwa natafuta injini ya kufunga kwenye gari langu.
Nikaenda dukani kununua injini.
Nikakuta injini mbili, moja ina miaka 35 na nyingine ni mpya kabisa.
Nikavutiwa sana na injini mpya nikainunua na kudharau ile ya zamani.
Nilipotaka kufunga ile injini mpya kwenye gari langu niakshtukia kuwa ile injini kwanza kabisa ni ya kibajaji na haiwezi kuendesha basi langu kupanda milima na pili hiyo injini ni ya kibajaji.
Nikarudi haraka dukani na muuzaji akakubali kunirudishia hela zangu na kuniambia kuwa lile basi langu kwa ukubwa wake linafaa lifungwe ile injini ya zamani ambayo kumbe ni vumbi tu ndio lililoifanya ionekane imezeeka lakini injini ile imetengenezwa na royce royce kampuni inayotengeneza injini madhubuti zinazofungwa kwenye ndege zote kubwa tuzionazo angani.
Nikaijaribu injini hiyo kubwa na mara moja basi langu likaanza kupanda milima kama kifaru.
My take;
USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO
Injini nyingine zinaweza kuendesha gari kwenye mteremko lakini sio mlimani
Its just a matter of time people will know why and agree with LUKOSI that every human has the right to decide their own destiny, and on their judgement there will be no one to decide what they should do.
JARIBUNI KUHESHIMU UAMUZI WA MTU, NDOA IKIVUNJIKA USIWE NDIO WAKATI WA KUTOLEANA MATUSI YA NGUONI
 
lukosi endeleza biasha ra za poda siku zako zinaesabika magari na mizigo unayosafirisha unajaza mapoda kwenye magari ya watu pole wee
 
Naona siku zinavyozidi kwenda chadema inazidi kupoteza mvuto, tuache ushabiki kuna hitajika mabadiliko ya uongozi wa juu au sera, naona kunakitwa kinakwenda ndivyo sivyo. Ina bidi cdm ijipange upya kama kweli ina nia ya kuchukua dola 2015. Huo ni mtazamo wangu tu.
 
Hapa ina maana hao jamaa walimfuata lukosi na sio sera za chama.ni bora waondoke Maana hawana jipya zaidi ya kuangalia matumbo yao.
 
Na ndio maana wakaitwa wabeba mabox ,unatoka cdm unaenda ccm kama kweli wana uchungu na inchi hii kwanini wasiende hata tlp au nccr ,mnakimbilia ccm hii inayoua tembo kwa ajili ya uchaguzi,ccm hii iliyoficha pesa uswiss kwa ajili ya uchaguzi,ccm hii ambayo imeshidwa kununua ct scan muhimbili,seketure hamna hata x ray.laana iwafuate mlipo wasaliti wakubwa nyie na njaa itawaua nyie!
 
Na ndio maana wakaitwa wabeba mabox ,unatoka cdm unaenda ccm kama kweli wana uchungu na inchi hii kwanini wasiende hata tlp au nccr ,mnakimbilia ccm hii inayoua tembo kwa ajili ya uchaguzi,ccm hii iliyoficha pesa uswiss kwa ajili ya uchaguzi,ccm hii ambayo imeshidwa kununua ct scan muhimbili,seketure hamna hata x ray.laana iwafuate mlipo wasaliti wakubwa nyie na njaa itawaua nyie!
Unawapangia maisha?
 
Back
Top Bottom