CHADEMA: Uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa lini?

CHADEMA: Uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa lini?

Benson Mramba

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
766
Reaction score
1,884
Vikao vikuu vya Kikatiba vya CHADEMA 2016 viliazimia kuwa Uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa ufanyike mwaka huu 2018 ili kutoa fursa kwa Chama kujiandaa na chaguzi za Serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 ila mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya jambo hili kufanyika.

Azimio kama hili lilifanyika mwaka 2006 kuwa uchaguzi ufanyike 2008 ukafanyika 2009 na likarudiwa tena mwaka 2011 kuwa uchaguzi ufanyike 2013 lakini ukafanyika 2014.

Jambo ambalo ni wazi ni kuwa Mwenyekiti Freeman Mbowe amekuwa akitumia mbinu hii ya kutangaza tarehe ya mapema ili ya uchaguzi ili kutambua wapinzani wake, na mara akishawatambua huahirisha uchaguzi kwa mwaka mmoja kwa madai kuwa maandalizi hayakamilika na kuwa muda wake kikatiba haujaisha.

Katika muda huu wa nyongeza ndio huutumia kushughulika na timu pinzani hadi anaimaliza yote. Haya ndio yalimkuta Chacha Wangwe na Zitto Kabwe wakati huo kwa nyakati tofauti.

Ni vema sasa Taifa na Wana CHADEMA wakajulishwa ratiba kamili ya Uchaguzi wa CHADEMA na pia ni wakati muafaka kwa Mwenyekiti Mbowe kulitangazia Taifa kama anagombea tena ama la ili kufungua mjadala wa kitaifa ikiwa ni pamoja kuandaa mrithi wake.
 
Wewe jamaa sijui Chadema walikufanyaje...ni mishahara wanayolipwa kina Mrema na wenzake bado inakuuma au kuna mengine?
 
Vikao vikuu vya Kikatiba vya Chadema 2016 viliazimia kuwa Uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa ufanyike mwaka huu 2018 ili kutoa fursa kwa Chama kujiandaa na chaguzi za serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 ila mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya jambo hili kufanyika.

Azimio kama hili lilifanyika mwaka 2006 kuwa uchaguzi ufanyike 2008 ukafanyika 2009 na likarudiwa tena mwaka 2011 kuwa uchaguzi ufanyike 2013 lakini ukafanyika 2014.

Jambo ambalo ni wazi ni kuwa Mwenyekiti Freeman Mbowe amekuwa akitumia mbinu hii ya kutangaza tarehe ya mapema ili ya uchaguzi ili kutambua wapinzani wake, na mara akishawatambua huahirisha uchaguzi kwa mwaka mmoja kwa madai kuwa maandalizi hayakamilika na kuwa muda wake kikatiba haujaisha.

Katika muda huu wa nyongeza ndio huutumia kushughulika na timu pinzani hadi anaimaliza yote. Haya ndio yalimkuta Chacha Wangwe na Zitto Kabwe wakati huo kwa nyakati tofauti.

Ni vema sasa Taifa na Wanachadema wakajulishwa ratiba kamili ya Uchaguzi wa CHADEMA na pia ni wakati muafaka kwa Mwenyekiti Mbowe kulitangazia Taifa kama anagombea tena ama LA ili kufungua mjadala wa kitaifa ikiwa ni pamoja kuandaa mrithi wake!
we jamaa huwa mnafiki sana toka enzi upo shule ya msingi ila hubadiliki
 
Wewe jamaa sijui Chadema walikufanyaje...ni mishahara wanayolipwa kina Mrema na wenzake bado inakuuma au kuna mengine?
huyu kilichompata chadema hawezi kukisahau , alistukiwa kirahisi sana ! mpaka leo anaona aibu hata kukanyaga kwenye tawi lolote la chadema.

Na tunasubiri aje akione cha moto , hakuna kucheka na wasaliti kudadeki !
 
Wakati tunamsubilia mbowe ajibu pia hawa mrema ,cheyo nao uchaguzi wataufanya lini?
 
huyu kilichompata chadema hawezi kukisahau , alistukiwa kirahisi sana ! mpaka leo anaona aibu hata kukanyaga kwenye tawi lolote la chadema.

Na tunasubiri aje akione cha moto , hakuna kucheka na wasaliti kudadeki !
Anatia huruma sana.
 
Lazima nigombee uwenyekiti taifa safari hii kupima jinsi demokrasia ambavyo imeota mizizi kwa mchina kukubalika si mmatumbi , mchina cdm na sitakubali ile demokrasis ya kuombwa na wazee kuondo jina langu ni mpishe mchagga.
 
Uchaguzi wa mwenyekiti utafanyikaje wakati wapinzani wakikusanyika wanafunguliwa kesi kwa kusema kuwa wanapanga njama za kumpindua mfalme.
 
mkuu unakosea sana anza kwanza kuuliza ...halmashauri kuu ya ccm imeshateuliwa...na 90% wajumbe kutoka kanda ip...time will tell
 
huyu kilichompata chadema hawezi kukisahau , alistukiwa kirahisi sana ! mpaka leo anaona aibu hata kukanyaga kwenye tawi lolote la chadema.

Na tunasubiri aje akione cha moto , hakuna kucheka na wasaliti kudadeki !

Halafu ni KLM mwenzenu, hapo sasa!
 
Back
Top Bottom