Maziwafreshi
New Member
- Feb 10, 2015
- 1
- 3
Nimekuwa msomaji na mfuatiliaji wa kawaida wa jukwaa hili lakini leo nimeamua kuzama mzimzima baada ya kuguswa na hoja kadhaa ambazo si nzuri kwa mstakabari wa mabadiliko tunayoyapigania.
Juzi kulikuwa na makala moja hapa yenye kichwa CHADEMA ISIPOTOA TAMKO HILI LITATUGHARIMU UCHAGUZI UJAO ambayo kimsingi iligusa mtaa wangu kwani mimi pia naishi mtaa huo wa Nyasaka B, na nyingine iliyosema CHADEMA TOENI SEMINA ELEKEZI KWA WENYEVITI WA MITAA ambazo zote zilichangiwa kishabiki bila kujali hoja husika.
Kwanza nikiri kuwa makala ile iliwakilisha kilio cha wengi na pia siyo kweli kuwa ukikosoa jambo unaloona aliendi sawa na matarajio yako kwa chama basi wewe ni CCM, au una chuki na kiongozi hapana. Busara ni kufanya utafiti na kutoa majibu kulingana hoja husika lakini wengi badala ya kujadili hoja wanakuja na personal attack.
Wananchi wanataka kuona utofauti wa CHADEMA na CCM ili kujenga imani zaidi wala siyo kufanya yaleyale au zaidi ya CCM kisa eti mbona nao walifanya hivyo. Hapo tutapotea njia!!
Mfano mtu anapotaka Wenyeviti wa mitaa wapewe semina elekezi anakuwa na nia nzuri kwani siyo wote wanafahamu malengo ya chama, wengi waliingia CHADEMA baada kuangalia upepo unavumaje, ilikuwa ukigombea kupitia CHADEMA unapeta sasa hivi lengo ni moja tu kudelete kabisa CCM hivyo hatuchagui mtu bali chama.
Nilisikitika sana niliposikia kauli hizi... Nani kakuambia kuwa hao wenyeviti wa Sisiem waliopigwa chini, walikuwa hawachukui 10% kamisheni? Tena nikusahisishe kidogo, hao wenyeviti wa magamba, walikuwa wanajimegea more than 10% commission AU Tupe idadi ya idadi ya askari polisi wanaofanya kazi katika jiji la mwanza Ili tujadili Kama askari wanatosha kutoa ulinzi kwa kila mkaazi wa jiji la mwanza?, msipolima wenyewe barabara mnategemea nani awalimie..
Yaani badala ya kutafuta namna ya kuboresha barabara zetu kupitia kamati za maendeleo ya kata (WDC) tumeona njia pekee ni kuwafanya walipa kodi matrekta? Badala ya ku- harmonize na vituo vya polisi vilivyo katika maeneo yetu, kuaangalia askari wanapangaje doria zao ufumbuzi ni kukesha tukilinda mitaa yetu? Badala ya kusaidia wananchi wamiliki ardhi na kujenga nyumba zao,tunataka kulipwa 10%?
Hoja hapa ni je matendo hayo ni sahihi na ndo msimamo wa chama? Na je yanaweza kuchochea kuaminiwa zaidi na wananchi hata kutupa dhamana kubwa?
Tunataka viongozi wabunifu wanaoendana na falsafa ya mabadiliko. Polisi hawatoshi sawa, lakini je ni kweli kuwa maeneo yote ya nchi wananchi wanakesha kujilinda wenyewe? Rekodi za ulinzi wa aina hii zikoje uko nyuma? Wizi unaotokea mchana mbona hakuna zamu ofisi moja baada ya nyingine kulinda mitaa inayowazunguka? Michango hii inayotambulishwa na uongozi mpya inatofauti gani na kodi ya maendeleo tuliyokuwa tukilipa huko nyuma? Je, ni kweli kuwa baada ya kodi hizo kupigwa stop hakuna maendeleo?
Imani yangu ni kuwa humu wamo viongozi wa CHADEMA wanapitia kila post kama nilivyokuwa nikifanya mimi kabla ya leo, hivyo hapa ni sehemu sahihi kabisa wala hakuna haja ya kupanga foreni ofisi za kata, wilaya, mkoa hata taifa na kuacha kutafuta mkate wa kila siku.
Naomba tuache kuchangia ili kuonekana tumechangia ni bora kukaa kimya na hata wakadhani u mjinga kuliko kuongea katika namna itakayothibitisha kuwa u mjinga