CHADEMA, Tusiuogope ukweli, tukubali kukosolewa

CDM kimeendelea kufanikiwa kwa kuchukua ushauri wa aina mbalimbali ikiwemo huu ulioutoa, wengi wao wanatembelea humu, wamekusikia, nasi tumekusikia, ila ni vizuri ukitaka hata mkeo akusikilize unapomkosoa anza kwanza kwa kuelezea mazuri aliyokufanyia tangu awe mke wake ndipo useme lkn kuna neno dogo linanikera........................ ukiwa hivi kila mtu atakusikia,
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake na kugundua ni wagumu mno kukubali kukosolewa pale Chama kinapo kuwa kimekwenda visivyo.
Viongozi wa CHADEMA karibuni wamebebeshwa mzigo wa kuzuka kwa vurugu kwenye mikutano mingi na kusababisha mauaji.Hizi ni shutuma nzito,lakini pro-CHADEMA wengi wamekuwa wakikabili yeyote atakaye-challenge uhusika wa CHADEMA katika haya kwa dhihaka,matusi na kejeli.
Hata mambo kadhaa yaliyo ikumba na kuitikisa CHADEMA hujibiwa kwa dhihaka,kejeli na hata matusi toka kwa pro-CHADEMA wengi na hata viongozi mara nyingine.
Mimi kama miongoni mwa mashabiki wa CHADEMA nakuwa na wasiwasi kwa mwenendo huu,CHADEMA itakapo shika dola si itageuka kipofu na kuwa mbaya kuliko CCM?
Nashauri pro-CHADEMA tugeuze mtazamo na kuitazama CHADEMA kwa mtazamo chanya na kujibu hoja kwa hoja na wala si matusi,dhihaka na kebehi.Hii haijengi bali inabomoa chama.
Viongozi wa CHADEMA nao wawe responsible kwa kutupeleka watanzania kuelekea Tanzania tuitakayo!
TANZANIA,nakupenda sana.

Gud point kaka inatakiwa ifike kipindi tukubali kuwa hakuna binadamu walio kamili, na ili kufika hasa pale tunapotaka tunahitaji watu wa kutukosoa, kwani siku zote kukosolewa kunamjenga mtu kuwa na maono chanya, hili jambo limekuwa likiniumiza kichwa na sisi vijana tusitumie macho kutazama, bali tutumie macho kuona vile tunavyovitazama.

Kukosolewa kunonesha ni jinsi gani wanaokukosowa wanamapenzi ya dhati kwako a hawataki uharibikiwe bali wanataka ufikie mafanikio unayoyaota. tukumbuke kuwa kesho ni matokeo ya kile tulichokifanya leo, kama tukiharibu leo, kesho yetu haitokuwa salama kamwe.
 
Si slaa tu , waitwao makamanda wote hawaonekani si Iringa hata Morogoro hawaonekeni. Wanaopata madhara ni watu dhalili hasa hawa wanaoandika humu ndani na CDM haiwajui. Kelele nyingiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mkuu, nilitegemea wewe kama great thinker na shabiki wa CDM ungekuja na mifano hai ya wapi CDM waliambiwa au walikosolewa kuhusu jambo fulani lakini hawakukubali.

Labda mimi sikijui vizuri kiswahili, tafadhali nisaidieni; hivi kubebeshwa mzigo ni kukosolewa au kusingiziwa kufanya kosa?

Binafsi siwalaumu pro-CDM wanaojibu hoja dhaifu kama hii kwa maneno makali. Kwa sababu, uzi unasomeka kana kwamba kuna hoja nzito imebebwa ndani yake, lakini ukisoma maelezo unajilaumu "kwa nini nimepoteza muda wangu kuufungua"!
 
Mkuu huo upostive unaouzungumzia ungeanzia kwako the way u luk at think from a netural angle.....if may ask
  1. CDM wamewahi kua?
  2. M4C lindi na Mtwara walikufa wangapi?
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake na kugundua ni wagumu mno kukubali kukosolewa pale Chama kinapo kuwa kimekwenda visivyo.
Viongozi wa CHADEMA karibuni wamebebeshwa mzigo wa kuzuka kwa vurugu kwenye mikutano mingi na kusababisha mauaji.Hizi ni shutuma nzito,lakini pro-CHADEMA wengi wamekuwa wakikabili yeyote atakaye-challenge uhusika wa CHADEMA katika haya kwa dhihaka,matusi na kejeli.
Hata mambo kadhaa yaliyo ikumba na kuitikisa CHADEMA hujibiwa kwa dhihaka,kejeli na hata matusi toka kwa pro-CHADEMA wengi na hata viongozi mara nyingine.
Mimi kama miongoni mwa mashabiki wa CHADEMA nakuwa na wasiwasi kwa mwenendo huu,CHADEMA itakapo shika dola si itageuka kipofu na kuwa mbaya kuliko CCM?
Nashauri pro-CHADEMA tugeuze mtazamo na kuitazama CHADEMA kwa mtazamo chanya na kujibu hoja kwa hoja na wala si matusi,dhihaka na kebehi.Hii haijengi bali inabomoa chama.
Viongozi wa CHADEMA nao wawe responsible kwa kutupeleka watanzania kuelekea Tanzania tuitakayo!
TANZANIA,nakupenda sana.

Kwanini Unaogopa kuwakosoa WAISLAMU; Wanaandamana WENGI TU HAKUNA POLISI, HAKUNA FFU na MABOMU hakuna

Sasa WAO NDIO Wanaweza kuingoza NCHI VIZURI SANA sababu MKUU WA POLISI NI MWISLAMU; JAJI MKUU MWISLAMU;

MKUU WA MAJESHI MWISLAMU na JAJI KIONGOZI MWISLAMU... Sasa wewe UKILINGANISHA na CHADEMA, CHADEMA

hakina Chochote unakiita kidhaifu... Kimbilia kwa WAISLAMU Wao naona wataweza kuongoza DOLA vizuri...
 
Mimi siamini kama wana CHADEMA hawapendi kukosolewa, la hasha. Watu wanachotaka ni kukosoana kwenye ukweli ndani yake. Mtu anapoamka na kusema CHADEMA ni chama cha kikanda unataka ajibiwe nini?? Remember people are entitled to their opinions but not facts. Facts have to be true. Unakosoa ikiwa una facts then watu watasikiliza, lakini maneno ya uzushi na fitna lazima watu watakushambulia. Mbona kuna thread nyingi tu za kushauri CHADEMA humu na zinaheshimika??
 
Hivi kwanini katika picha zote za vurugu za Nyololo Mufindi Dr. Slaa haonekani? Yeye alijificha wapi wakati aliwaambia mashabiki wake waje wasiogope kitu mpaka kieleweke?

Sasa mtu kama huyu ajibiwe nini? Kwani anaropoka tu. Siku hiyo cdm walitangaza kuwa wasio na kadi waondoke kwani hakuna mkutano wa hadhara.
 
Unajua mtu anayetaka kuzama huwa anajitahidi kutapa tapa huku na kule alimradi afike ng'ambo.....kitu au mtu yeyote atakayetaka kumgusa ni ugomvi au vurugu ajabu....kwa mtu asiejua anaweza kusema hivi huyu mtu akifika nchi kavu si ataua wengi kwa makofi na mateke!
Watu wengi hasa vijana wasio na matumaini wameona kama chadema ndio mkombozi wao....wanachotaka ni kusonga mbele hivyo kupinga harakati zao ni kama kumshika shati a drowning man....na sio maisha katika hii period yatakuwa kama your prediction....na haimanishi kuwa chadema wakishika dola hatuwezi kuwabadilisha wakizingua...
treni ya m4c imeshashika run way cha muhimu ni kujoin na wala sio kui-halt!
 
Sasa mtu kama huyu ajibiwe nini? Kwani anaropoka tu. Siku hiyo cdm walitangaza kuwa wasio na kadi waondoke kwani hakuna mkutano wa hadhara.

Mtu kama huyu ajibiwe whereabouts za Dr. Slaa wakati vurugu zinatokea. Kwanini akuplay role ya uongozi ya kutoa maelekezo kwa wanachama wake? Alikuwa wapi?

Soma historia ya Tanganyika. Kuna chief anaitwa Kunambi. Huyu chief alitoa ushauri mzuri sana kwa Govenor ambao ulifanya circular no. 6 ya kukataza watumishi kushiriki siasa kufutwa. Ukielewa busara iliyotumiwa na Goveror kumuelewa chief Kunambi, utaelewa kuwa Dr. Slaa hakupaswa kuwatelekeza mashabiki na wanachama wa Chadema wakati wa vurugu zilizosababishwa primarily na yeye kuwahakikishia mashabiki hao kuwa hakuna kukubali amri ya polisi "mpaka kieleweke"
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake na kugundua ni wagumu mno kukubali kukosolewa pale Chama kinapo kuwa kimekwenda visivyo.
Viongozi wa CHADEMA karibuni wamebebeshwa mzigo wa kuzuka kwa vurugu kwenye mikutano mingi na kusababisha mauaji.Hizi ni shutuma nzito,lakini pro-CHADEMA wengi wamekuwa wakikabili yeyote atakaye-challenge uhusika wa CHADEMA katika haya kwa dhihaka,matusi na kejeli.
Hata mambo kadhaa yaliyo ikumba na kuitikisa CHADEMA hujibiwa kwa dhihaka,kejeli na hata matusi toka kwa pro-CHADEMA wengi na hata viongozi mara nyingine.
Mimi kama miongoni mwa mashabiki wa CHADEMA nakuwa na wasiwasi kwa mwenendo huu,CHADEMA itakapo shika dola si itageuka kipofu na kuwa mbaya kuliko CCM?
Nashauri pro-CHADEMA tugeuze mtazamo na kuitazama CHADEMA kwa mtazamo chanya na kujibu hoja kwa hoja na wala si matusi,dhihaka na kebehi.Hii haijengi bali inabomoa chama.
Viongozi wa CHADEMA nao wawe responsible kwa kutupeleka watanzania kuelekea Tanzania tuitakayo!
TANZANIA,nakupenda sana.
Jana niliikosoa CDM ktk thread "kujilimbikizia madaraka" Kuna mchangiaji mmoja aliniuliza maswali ya msingi kuhusu hoja zangu. Nilimjibu tena kwa urafiki, wala hakunitukana, kunidhalau au kunikejeli. Tulifikia mahala, tulikubaliana na nikajiona sina hoja. Matusi mengi hapa huwekwa na Mamluki wa CCM. Ktk psychology tunaamini "the facts will speak for themselves" angalia mikutano ya chaguzi za CCM. UWT - Dar walitukanana, CCM- Nzega Matusi then Bunduki nk. Huu ni ushahidi tosha CCM hoja zimewashinda, kilichobaki ni Propaganda, Matusi, Vurugu na Nduvu ya Dora.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake na kugundua ni wagumu mno kukubali kukosolewa pale Chama kinapo kuwa kimekwenda visivyo.
Viongozi wa CHADEMA karibuni wamebebeshwa mzigo wa kuzuka kwa vurugu kwenye mikutano mingi na kusababisha mauaji.Hizi ni shutuma nzito,lakini pro-CHADEMA wengi wamekuwa wakikabili yeyote atakaye-challenge uhusika wa CHADEMA katika haya kwa dhihaka,matusi na kejeli.
Hata mambo kadhaa yaliyo ikumba na kuitikisa CHADEMA hujibiwa kwa dhihaka,kejeli na hata matusi toka kwa pro-CHADEMA wengi na hata viongozi mara nyingine.
Mimi kama miongoni mwa mashabiki wa CHADEMA nakuwa na wasiwasi kwa mwenendo huu,CHADEMA itakapo shika dola si itageuka kipofu na kuwa mbaya kuliko CCM?
Nashauri pro-CHADEMA tugeuze mtazamo na kuitazama CHADEMA kwa mtazamo chanya na kujibu hoja kwa hoja na wala si matusi,dhihaka na kebehi.Hii haijengi bali inabomoa chama.
Viongozi wa CHADEMA nao wawe responsible kwa kutupeleka watanzania kuelekea Tanzania tuitakayo!
TANZANIA,nakupenda sana.

Hapo kwenye blue,
Mikutano mingi ya Chadema imefanyika hapa tanzania na hata nje ya nchi, mfano mikutano ya M4C iliyofanyika Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, n.k.
Jiulize bila unafiki, watu wangapi waliuawa kwenye mikutano hiyo? Je Iringa aliyeua mwandishi ni Chadema, Maana ameshakamatwa na polisi!!!
Wewe na wenzako mnataka Chadema wakubali kila uongo unaotolewa na CCM dhidi yake, ndio muone kuwa wanakubali kukosolewa. Chadema watakubali kukosolewa pale watakapoambiwa ukweli tu, na sio uongo wa CCM.
Wana-JF wote ambao ni wafuasi wa CCM, jaribuni kuwa objective, msishangilie mauaji yanayofanywa na polisi, halafu mkasingizia Chadema.
Bila polisi, hakuna mauaji ya raia kwenye mikutano ya Chadema
(mfano, mikutano ya Chadema iliyofanyika Arusha bila ulinzi wa polisi, haikusababisha mauaji yoyote).
Kumbukeni kuwa Daima, atawalaye kwa upanga, hakika, atakufa kwa upanga.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa viongozi wa CHADEMA na wafuasi wake na kugundua ni wagumu mno kukubali kukosolewa pale Chama kinapo kuwa kimekwenda visivyo.Viongozi wa CHADEMA karibuni wamebebeshwa mzigo wa kuzuka kwa vurugu kwenye mikutano mingi na kusababisha mauaji.Hizi ni shutuma nzito,lakini pro-CHADEMA wengi wamekuwa wakikabili yeyote atakaye-challenge uhusika wa CHADEMA katika haya kwa dhihaka,matusi na kejeli.Nashauri pro-CHADEMA tugeuze mtazamo na kuitazama CHADEMA kwa mtazamo chanya na kujibu hoja kwa hoja na wala si matusi,dhihaka na kebehi.Hii haijengi bali inabomoa chama..
Bwana Kamwela, ni vigumu kumpa jibu chanya mtu anayedhihaki, anatukana na kutetea uovu na kupaka wengine matope. Angalia thread yako ukianzia maneno HIZI NI SHUTUMA NZITO.... na nikuulize maswali: 1. Kuna mtanzania gani aliye objective asiyejua kuwa CDM haiui ila polisi wanaua kuidhoofisha CHADEMA? 2. Je, polisi wangetulia kama walivyotulia kwenye maandamano ya kuwakomboa waliowekwa ndani ajili ya sensa huko DSM kuna mtu angeuawa? 3...Wewe msimamo wako kuhusu hili ni huu niliouona?. 4. Kama unasema CDM imeua utasemaje wewe ni shabiki wa CDM? 5. Nimekuona ukisoma thread ya mafilifili, utumbo huo ujibiwe vipi?
 
Gud point kaka inatakiwa ifike kipindi tukubali kuwa hakuna binadamu walio kamili, na ili kufika hasa pale tunapotaka tunahitaji watu wa kutukosoa, kwani siku zote kukosolewa kunamjenga mtu kuwa na maono chanya, hili jambo limekuwa likiniumiza kichwa na sisi vijana tusitumie macho kutazama, bali tutumie macho kuona vile tunavyovitazama.

Kukosolewa kunonesha ni jinsi gani wanaokukosowa wanamapenzi ya dhati kwako a hawataki uharibikiwe bali wanataka ufikie mafanikio unayoyaota. tukumbuke kuwa kesho ni matokeo ya kile tulichokifanya leo, kama tukiharibu leo, kesho yetu haitokuwa salama kamwe.

Hapo kwenye blue, uko sahihi kabisa, ila tu kama kuna ukweli ndani yake (yaani, kuna ukweli kwenye point inayokosolewa). Penye uongo, hata wewe utakataa, maana ni oungo. Mfano, jamaa aje hapa JF halafu aandike kuwa wewe heroone, ndiye uliyetekeleza yale mauaji ya mwandishi kule Iringa, hivyo unatakiwa kutubu na kukubali kukosolewa. Je ?? Utakubali kukosolewa katika hilo??
Watanzania, penye ukweli, watu hukubali kukosolewa, ila hapa JF, kuna watu wako kwenye 'ajira' ya CCM. Wanalipwa kwa kuleta uongo kila siku ili kuchafua wengine. Inasikitisha maana mpaka viongozi CCM wanasema uongo ili kuchafua wengine.
 
Si slaa tu , waitwao makamanda wote hawaonekani si Iringa hata Morogoro hawaonekeni. Wanaopata madhara ni watu dhalili hasa hawa wanaoandika humu ndani na CDM haiwajui. Kelele nyingiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Hata ARUSHA hamkuona? Kamwela anazungumzia suala la kuwa objective mbona mnaleta ushabiki? Inamaana darasa hili haliwahusu?
 
Mkuu hayo ungeyapeleka makao makuu au kwenye vikao rasmi vya Chama sio ulete hapa jamvini kishabiki sasa uanafaidika na nini kuiweka hapa au kuongeza idadi ya post? Hizo ni tabia za magamba sasa umepost nenda kwa nape ukachukue chako

Wakati mwingine jaribu kujenga kama great thinker sio kila muda kuleta kubisha tu.
 
Mkuu hayo ungeyapeleka makao makuu au kwenye vikao rasmi vya Chama sio ulete hapa jamvini kishabiki sasa uanafaidika na nini kuiweka hapa au kuongeza idadi ya post? Hizo ni tabia za magamba sasa umepost nenda kwa nape ukachukue chako

hawa ni mfano wa wale wapuuzi wachache wasiotaka kukosolewa. jenga hoja sio kubwabwaja tu hapa.
 
Mkuu huo upostive unaouzungumzia ungeanzia kwako the way u luk at think from a netural angle.....if may ask
  1. CDM wamewahi kua?
  2. M4C lindi na Mtwara walikufa wangapi?

M4C Mtwara na Lindi ilikuwa ni njia tu ya kuelekea kwa masangoma ndomaana haikuwa na mauaji
 
Back
Top Bottom