GE2025 CHADEMA: Tumepata taarifa ya Tundu Lissu kutaka kupewa sumu

GE2025 CHADEMA: Tumepata taarifa ya Tundu Lissu kutaka kupewa sumu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,662
Reaction score
59,100
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini.

Taarifa hizi zimetolewa usiku huu wa leo, tarehe 02 Julai 2025, kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya kuaminika. Miongoni mwa waliotoa kauli kuhusu suala hili ni Mhe. David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), ambaye kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika:

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini."

Chadema inachukulia taarifa hizi kwa uzito wa hali ya juu. Hili si jambo la kupuuzia, hasa tukikumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kulengwa na vitisho, mashambulizi au uonevu wa aina mbalimbali, huku taarifa nyingi tulizowasilisha kwa mamlaka husika zikipuuzwa au kutochukuliwa hatua yoyote.

Tunazitaka mamlaka husika, likiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuchukua hatua za haraka, huru na za kina kuchunguza madai haya mazito. Tunaitaka Serikali kutoa kauli ya wazi na kuwajibika kuhakikisha usalama wa Mhe. Tundu Lissu akiwa kizuizini.

Pia, soma; IDU tunafatilia njama za kumuwekea Lissu sumu Gerezani

Tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, Mashirika ya Haki za Binadamu, Mabalozi na wahusika wengine wote wa kimataifa kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kushinikiza uwajibikaji, ulinzi wa haki za binadamu, na kuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Imetolewa leo Jumatano, tarehe 02 Julai 2025

Brenda Rupia

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

IMG-20250702-WA0153(1).jpg

=====

UPDATES: 03 Julai 2025

======

Serikali imekanusha tuhuma zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zikiihusisha na kinachodaiwa kuwa ni kuwepo mpango wa kumwekea sumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Serikali imewaomba wananchi kupuuza taarifa hizo kwa kuwa hazina ukweli wowote.

Soma hapa chini kwa urefu..

TAARIFA KWA UMMA

Julai 3, 2025

Serikali ya Tanzania inakanusha tuhuma zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zikiihusisha Serikali na kinachodaiwa kuwa ni kuwepo mpango wa kumwekea sumu mshtakiwa Tundu Antipas Lissu.

Serikali inawaomba wananchi kupuuza taarifa hizo kwa kuwa hazina ukweli wowote. Tundu Antipas Lissu, anayetajwa na wanasiasa hao wa nje ya nchi, pamoja na taarifa kwa umma ya chama chake cha siasa, anakabiliwa na mashtaka Mahakamani kwa mujibu wa Sheria na anashikiliwa gerezani mpaka hapo shauri lake litakapohitimishwa na Mahakama.

Serikali haijawahi kuwa na mpango wa kumwekea sumu mtu yeyote aliyopo gerezani wala haina mpango wa kufanya hivyo kwa mtu yeyote. Taarifa hizo zimechapishwa kwa nia ovu ya kuchafua sifa na heshima kubwa ya Tanzania na tayari mamlaka zimeanza kuchukua hatua dhidi ya waliohusika kuchapisha na kusambaza uongo huo.

Gerson Msigwa

Msemaji Mkuu wa Serikali

Idara ya Habari MAELEZO na Ofisi ya msemaji Mkuu wa Serikali
IMG-20250703-WA0007.jpg
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha umma kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zinazodai kuwa Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuna mipango ya kuwekewa sumu akiwa kizuizini.

Taarifa hizi zimetolewa usiku huu wa leo, tarehe 02 Julai 2025, kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya kuaminika. Miongoni mwa waliotoa kauli kuhusu suala hili ni Mhe. David McAllister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya (European Parliament), ambaye kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameandika:

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za kutisha za jaribio la kumtilia sumu kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu akiwa kizuizini."

Chadema inachukulia taarifa hizi kwa uzito wa hali ya juu. Hili si jambo la kupuuzia, hasa tukikumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa viongozi wa Chadema kulengwa na vitisho, mashambulizi au uonevu wa aina mbalimbali, huku taarifa nyingi tulizowasilisha kwa mamlaka husika zikipuuzwa au kutochukuliwa hatua yoyote.

Tunazitaka mamlaka husika, likiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuchukua hatua za haraka, huru na za kina kuchunguza madai haya mazito. Tunaitaka Serikali kutoa kauli ya wazi na kuwajibika kuhakikisha usalama wa Mhe. Tundu Lissu akiwa kizuizini.

Tunatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, Mashirika ya Haki za Binadamu, Mabalozi na wahusika wengine wote wa kimataifa kufuatilia kwa ukaribu suala hili na kushinikiza uwajibikaji, ulinzi wa haki za binadamu, na kuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia nchini Tanzania.

Imetolewa leo Jumatano, tarehe 02 Julai 2025

Brenda Rupia

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

Poa, soma;

IDU tunafatilia njama za kumuwekea Lissu sumu Gerezani
View attachment 3391862
Mbona hii ni Taarifa mbaya sana.
 
Mwaka huu waganga wa kienyeji wamenufaika sana na hela za Sir100. Kuanzia wale wa visomo Gombero na Tongoni mpaka wale wa tunguli na vibuyu Mlalo na Kwedikwazu alipokua kwenye ziara ya mkoa wa Tanga.

Huko Kanda ya Ziwa kile kikosi kilichokua kinamlinda Jiwe kiliitwa na kufanya kazi. Commoro wameandaliwa magwiji wa visomo.
 
Back
Top Bottom