CHADEMA tumekuwa watu wa kusahau mapema

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,339
21,435
Salamu nyingi kwenu,

Ndugu zangu CHADEMA wenzangu leo hii tunapaza sauti na kuvimba mashavu kisa tu Masha amekatiliwa kwani yeye ni nani asikatiliwe.

Na hii si mara ya kwanza Masha kukatiliwa ya kwanza sisi CHADEMA tulimkataa tukamchagua Wenje Nyamagana.

Leo Masha amejipaka rangi gani nzuri ya kuonekana ni muhimu, alikuwa waziri wa lipi la kukumbukwa alifanya ndugu zangu tuache unafiki panapobidi.

Hapakupigwa kura ya wazi kila mmoja ametumia utashi wake ndugu zangu tusisahau mapema kiasi hicho.

Tujifunze sio kila tunachoshindwa tutafute mchawi.

Ahsanteni
 
Mbowe kasha piga hela hapo noma sana
tapatalk_1485892146512.jpeg

Hatari sana....
 
Nafikiri mkuu wewe si chadema na kama ni chadema basi ni ile ya dkt mihogo msubiri anakuja!
 
Chama cha Kidemokrasia kinataka kwenda Mahakamani kuomba kina Wenje wawe Wabunge japo kura Nyingi zimewakataa

Mbowe Ana arosto ya Kisiasa kipindi hiki tumuombee arudi sawa!
Hakuna zaidi ya hilo,misingi ya chama imepotea!
 
Wafuasi wengi wa vyama ni bendera fuata upepo, yaani hata kama kuna uozo ndani ya vyama vyao wao wanatetea tu eti kwa kuwa kasema au kafanya kiongozi wao, kwenye ukweli lazima usemwe, kukaa na kushabikia hata uozo ni tatizo.
 
Ukiona huridhiki na chama cha CHADEMa vyama na Vicoba vipo vingi unajiunga navyo huko unatoa madukuduku yako na kugombea nafasi ambazo unaona wewe kuna watu wameshindwa au hawana uwezo wa kufanya
 
Bado wapo kwenye zama za giza ukimsema ndio anajirebisha!
 
Hujui kua chadema wanaamin ..ukisha toka ccm ukajiunga chadema wew ni asset kubwa sana....subir bado siku sepenga akipewa nyadhifa ndani ya chadema ndo utaongea lugha zote ziishe
 
Ukiona huridhiki na chama cha CHADEMa vyama na Vicoba vipo vingi unajiunga navyo huko unatoa madukuduku yako na kugombea nafasi ambazo unaona wewe kuna watu wameshindwa au hawana uwezo wa kufanya
Hakuna mwenye hati miliki ya chadema isipokuwa chadema kwa wote ukikosea lazima upewe ukweli,tafakari maneno ya mkapa wajinga na malofa alikuwa na maana kubwa!
 
Umeandika wakusome au dhihaka Kwa chadema. Masha ni chadema no blah blah tena za kiccm. Alikuwepo ujingani na kufanya yaliyo ya kijnga ila Sasa ameelemika
 
upinzani wa kweli utapatikana siku chadema ikisambaratika(Self natural death).
Wamewaaribu vijana mitandaoni wameugua ugonjwa wa kuwa an mitazamo Hasi juu ya kila kitu nchini huku wakiwa na uwezo ulio chini ya wastani wa kujenga hoja na kutoa suluhisho la KIbunifu.
Usahihi ni kinyume chake!
 
CCM ndiyo inatakiwa isambaratike kwa mustakabali chanya wa nchi yetu na si kinyume chake.
 
Back
Top Bottom