CHADEMA: Tuko tayari kwa UKUTA 01/09/2016

CHADEMA: Tuko tayari kwa UKUTA 01/09/2016

UMOJA WA KUPINGA UDIKITEKTA TANZANIA(UKUTA) umekuwa gumzo nchini,umewatoa waliojificha kuonekana wasemaji wa vyombo vya dola,lakini kumeibua pia zana za kivita na mafunzo kwa majeshi yetu ya usalama wa raia na mali zake. Kumeibua mafunzo ya utumiaji rungu na mafunzo mbalimbali ya kukabiliana na adui.

Adui ni nani,muktadha mzima wa mafunzo haya umelifanya jeshi la polisi kuwa msemaji wa serikali kitendo kinachopelekea kazi za wasemaji wa serikali kuonekana watumishi hewa,kwa kuwa jeshi limepoka majukumu ya kada hiyo. Adui hapa mkubwa anayepingwa na jeshi hili ni mpinga demokrasia kukandamizwa na mpinga katiba kukanyagwa.

Hapo ndipo dhana potofu na ombwe la weredi kwa taasisi zetu linapojidhihirisha wazi. Maudhui ya hoja ya ujenzi wa UKUTA ilipaswa kujadiliwa kwa kina kuliko kuwatishia wananchi ambao ndiyo walipa mshahara na wanunuzi wa silaha zinazotumika leo kuwatishia wananchi wenye mrengo unaokinzana na mawazo ya mtu mmoja asiyetaka kufuata utawala wa sheria.

Nguvu kubwa inayotaka kutumika inapingana kabisa na demokrasia katika kuitekeleza misingi ya utawala bora yenye kuheshimu utawala wa sheria,na hapo kiongozi aliyeko madarakani anapoonekana mtawala mwenye fikra za udikitekta kwa kuzuia sheria za kimamlaka kutenda kwa mujibu wake. Vinginevyo ijulikane kuwa maamuzi ya nchi hii yanafanyika Lumumba pia ni kipindi cha chama kushika hatamu.

Mbaya zaidi dhana nzima ya UKUTA inatafsiriwa kinafki na wakuu wa vyombo vya dola kwa kujipendekeza kwa rais anayedhani kuwa anajaribiwa pasi na kujua ameapa kuilinda na kuhifadhi katiba aliyoapa kuilinda. Mwalimu J K Nyerere aliwahi kusema,tunataka rais atakayeheshimu katiba,na kupitia katiba hiyo tutamwapisha vinginevyo hatufai.

Jukumu na wajibu wa vyama vya siasa ni kufanya kazi ya siasa,ikiwa pamoja na mikutano ya hadhara na maandamano,majukumu yote hayo yapo kisheria,unapotoa tamko la kuikana sheria na kujiona upo juu ya sheria hakika unapaswa kuhojiwa pamoja na kuelekezwa kuwa urais si ufalme au uchifu.

Hoja ya CHADEMA kupinga matumizi mabaya ya madaraka ina mashiko na ipo kisheria kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano kuwa , 26(1) kila mtu ana wajibu wa kufuata na kuitii katiba hii na sheria za Jamhuri wa Muungano. Jukumu la polisi ni kulinda wanasiasa hao maandamano na mikutano yao inakuwa salama na haifanyiwi vurugu ili walilolikusudia kulizungumza walizungumze,unapozuia mdomo kusema unataka mikono iseme! Kama hofu ya serikali hii ni kusemwa wajirekebishe.

Hali ya nchi ni tete,mandhari inajionyesha kuwa nchi ipo vitani. Maandalizi na vitisho vinavyotolewa ni kinyume na tangazo la kuwa Tanzania ni nchi ya amani. Ajabu hata viongozi wa dini wamegeuka wanafiki kuegemea upande mmoja ilihali wakitaka meza ya majadiliano,unawezaje kusuluhisha wakati jaji umeshaonyesha uko upande upi? Kitendo cha sheikh wa mkoa wa DSM kusema kuwa CHADEMA watii mamlaka ya viongozi wa serikali ilihali alishindwa kuukemea upande wa serikali ulioapa kupitia katiba na vitabu vitakatifu vya Mungu,kunamuondolea sifa ya kuwa mpatanishi.

Unafiki na uoga wa madaraka unatoka wapi,kwa nini tunahangaikia tulipoangukia badala ya kushughulikia tulipojikwaa,naiona dosari ya kiuongozi ndani ya utawala huu,mafanikio ya serikali yako rais JPM hayatakuwa na tija kwa kuzuia vyama vingine vya siasa kufanya kazi zao zinazotambulika kisheria,huwezi kuzuia ufisadi ukafanikiwa ikiwa nawe ni fisadi wa kimamlaka. Jizuie kwanza kufanya siasa ndipo uwazuie na wengine,na ukifanya hivyo,tutahoji mamalaka iliyokuwa fursa hiyo ya kuzuia.

Jeshi la polisi ni chombo cha umma,epukeni kutumika vibaya kwa kuwa mkistaafu mnajiandaa kuwa wakuu wa mikoa na wilaya,kazi yenu inataka weredi na he kina,vinginevyo mtaharibu sifa ya jeshi na kuonekana chombo cha ukandamizaji na uharibifu wa mali ya umma.
 
Mkuu uko vizuri. Kimsingi hii issue ni ndogo sana - KATIBA NA SHERIA ZIHESHIMIWE. Wakati wa mchakato wa Katiba Mpya ilitungwa sheria na ikapitishwa kwa mbwembwe na "walio wengi" kwamba endapo Katiba Mpya haitapatikana then iliyopo ita-prevail. Ni jambo la kusikitisha Katiba Mpya haikupatikana na hata hiyo iliyopitishwa na Bunge kwamba ita-prevail nayo ndio hivyo tena.
 
Maandamano yaliyopangwa na Chadema, ya tarehe 1 septemba waliyoyabatiza kama UKUTA, yamebaki kwenye makaratasi tu na media, ikiwemo mitandao ya kijamii.

Ni ukweli usiopingika kwamba raia wamesikia kuhusiana na UKUTA lakini wenye kushiriki hakuna. Raia wamekataa , hawaoni sababu ya kushiriki jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Raia wengi hata wale waliopo kwenye ngome za Chadema kama wanavyodai wao, wamevutiwa sana na utendaji wa Rais Magufuli na hawaoni sababu za kuvuruga jitihada zinazoendelea kwani zitawarudisha kule wasikotaka kuwepo.

Mfano mzuri ni Arusha, ambako, tatizo la umeme lilijenga chuki kwa serikali toka kwa wananchi , sasa hakuna tena, na wananchi wanafurahia na kukubali juhudi za wazi kabisa za Rais kuhakikisha kua lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi linafanikiwa. Juhudi za makusudi za awamu hii ya tano kujenga sub stations zaidi ya nane ,ni kiashirio tosha cha nia ya makusudi ya awamu ya tano kulifanya tatizo la umeme Arusha kua historia.

Ukiachana na hilo, mwito umekua mdogo sana kwa wananchi, kama inavyodhaniwa na vyombo vya habari kuhusu ushiriki wao katika maandamano ya septemba mosi. Ukijaribu kuzungumza na wananchi mmoja mmoja hakuna anayeonesha nia wala hamu ya kushiriki.

Hilo linatuacha na maswali ya nani watakaoshiriki maandamano hayo, moja ya kada ambazo inaweza kushiriki ni wale vijana wa mtaani ambao hawana ajira za kudumu, na ambao ni rahisi kuwapa chochote ili kushiriki.

Kwakua nia ya dhati ya wananchi wengi ya kushiriki maandamano haipo, kuna kila dalili za baadhi ya watu kununuliwa na wahusika ili washiriki maandamano.

Vyombo vya usalama viangalie kwa ukaribu namna miamala ya wahusika wakuu wa maandamano hayo inavyokwenda, hii ikiwa ni pamoja na watu wa karibu wa wahusika wakuu, kwani kuna dalili za matumizi ya fedha katika kuhamasiha kwa maandamano ya septemba 1 yaliyopangwa kufanyika ambayo yamekosa mwitikio, na kubaki tu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
 
Walishindwa kushawishi watu walinde kura zao, leo wanataka tuwe sehemu ya kukwamisha maendeleo na mabadiliko ya kweli...
 
Watanzania ni mbumbumbu wa katiba yao ndo maana watawala wanaongoza nchi kwa mihemuko kuliko kufuata katiba,mbaya hata viongozi wa dini pamoja na usomi wameingia mtego wa umbumbumbu huo.
 
mw
Walishindwa kushawishi watu walinde kura zao, leo wanataka tuwe sehemu ya kukwamisha maendeleo na mabadiliko ya kweli...
Mwitikio wa wananchi kushiriki maandamano ya septemba mosi haupo, ukuta imebakia kwenye media tu mkuu, ingawa wahusika wanawahadaa watu kua yatakuwepo, ukweli ni kwamba hakuna anayetaka kupoteza muda wake kutetea mafisadi.
 
Back
Top Bottom