Chadema tufanya haya tunaongoza nchi mwaka 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema tufanya haya tunaongoza nchi mwaka 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kisendi, May 24, 2012.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana JF haya ni mawazo yangu:
  Yafuatayo yakifanywa na chadema tutashika dola mwaka 2015

  - Kuwa karibu na wastaafu wote wa kipindi cha mwl nyerere ili watupe muongozo wa dola
  - Kuwajibika hasa majimboni kwetu kwa kufanya vikao na wananchi walala hoi angalau kuweza kuanzisha mifuko ya kijamii na kufungua mashina, kujenga ofisi ndogo ndogo kila kata
  - Kuacha kutoa matamko yasiyo na tija bali kuwa na mtu mmoja tu wa kutoa matamko
  - Kupata wanachama wengi wasomi na wasio wasomi ngazi za kitaifa ba vijiji
  - Kutizima nani akigombea uraisi 2015 atakuwa na mvuto na uwajibikaji, si mwepesi wa kukasirika, si mwepesi wa kufunga watu, awe tayari kuinyosha tanzania hasa katika utimiaji wa pesa za walipa kodi
  - kuwa karibu na wafanyabiashara kwa maslahi ya taifa na si chama
  - kuwa na muona wa kitaifa na si ukanda
  - kuandaa watu ambao hawatakuwa na njaa na tamaa ya utajiri wa haraka haraka
  - kuwa wavumilivu wa kisiasa ndani ya chama
  - kuwatoa wale wote wanakiuka maadili ya chama bila kubagua
  - kuweka makada kila mkoa, kila wilaya wenye utalaamu wa uchumi na maendeleo
  - kuacha kuwa wababe kwa kila jambo
  - kupunguza matamko yasiyo ya tija ilihali bado hatujashika hatamu
  - kutopokea wanachama ambao wana damu na historia ya CCM kama sh*b*d*
  - Binafsi Dr Slaa, au ((Sitta/magufuli)- wakijiunga dakika za mwisho nchi itakuwa imekombolewa) wanafaaa kugombea Uraisi kupitia CDM maana Zito bado kidogo labda miaka ijayo.
  - Dr Slaa anafaa kuwa waziri mkuu, Mbowe kuwa mwenyekiti wa chama
  - Tukifanya haya na maneno tunayoyapata kutoka ndani wana ccm wenyewe wamekata tamaa kwahiyo tujipange tu. Kweli tujipange na tuache kukurupuka please mbowe ukipata hii thread fanyia kazi haya mambo, na wanatanzia ambao wako tayari kuongoza nchi basi wajongee ofisi za chadema wachukue kadi maana upepo uko CDM sasa kazi kwetu.
   
Loading...