CHADEMA tuboreshe intelijensia yetu, Katibu Mkuu na Mwenyekiti rekebisheni makosa

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,189
27,237
Habari wanaJf, leo kuna jambo ambalo ninapenda kueleza ambalo kiukweli linanishangaza sana na kuniacha mdomo wazi.

Nakiri kuwa nilikuwa ninaamini sana tabia tulizonazo sisi washabiki wa chama hazijafika kwenye uongozi wa juu wa chama, lakini sasa tulipo naona mambo yanakuwa tofauti kabisa.

Katibu mkuu wa chama amezungumzia kuhusu suala la kuchapishwa karatasi za kura tu kwa sababu kuna taarifa anayo kutoka vyanzo vyake.
Hizi taarifa za hivi zilianza twitter kama tetesi/uzushi na zikapokelewa na mashabiki, ila sikujua kuwa na viongozi wa vyama nao wamezipokea na kwenda kuzungumzia.

Hapa ndio tatizo ninapoliona, katibu mkuu hupaswi kufanyia kazi kila tetesi au uzushi unaozushwa mitandaoni bali inatakiwa uwe na intelijensia ya kutosha kujua undani wa jambo hilo.

Kuna siku kuna mtu alizusha raisi amewaita wakurugenzi wa halmashauri wote dodoma, kwa bahati mbaya mgombea wetu uraisi naye akalichukua jambo hilo na kwenda kulizungumza kwenye kampeni zake(hili lilikuwa kosa kubwa sana) kwa nini kwa sababu linaondoa credibility ya mengine anayoyanadi.

Watu wapo ofisini mikoa tofauti wapo na wakurugenzi wao wakiendelea na majukumu yao, ghafla wanaona mgombea wetu chadema anasema wakurugenzi wote wa halmashauri wameitwa dodoma. Hapa ni lazima hawa watumishi watapata mashaka sana juu yetu kwa kuwa wataona mengi tunayozungumza ni uongo
Jingine,mgombea wetu wa chama na mwenyekiti mbowe waliita press wakaeleza mengi mazuri ila ghafla wakaeleza kuwa Rais atakuwa na mapumziko ya siku 8 (tarehe 4-12), hii ilianza kama uzushi huko twitter lakini bila kuchukua muda wa kutafakari chama kupitia mwenyekiti na mgombea urais wote kwa pamoja wakalibeba jambo hili moja kwa moja huku ikiwa sio jambo la kweli.

Hapa tayari chama kama chama kuna tatizo kwenye intelijensia, hivyo kuna mikakati ya lazima yapaswa kufanywa ili kuokoa na kurudisha intelijensia ya chama kama zamani.

Ushauri:
Chama hakipaswi kuokota kila habari inayozushwa huko twitter, badala yake hii kazi inabidi ibaki kwa mashabiki. Wao wakisema la uongo au la uzushi lolote kuna kuwa hakuna athari yoyote kwa chama.

IMG_20201011_104334.jpg
 
Wameingia choo cha kike kama lissu alivyotumiwa Meseji ya kudanganywa Rais amekutana na wakurugenzi

Ila jana Mnyika aliongea kiuoga kiuoga maana hawana uhakika na wanachokisema
 
Tatizo wenzako wanapumulia mashine. Kama mna akili anzieni kwenye corona, muone mlivyowajinga na wapumbavu ktk nchi hii. Mlidakia hoja za wazungu kumbe mlikuwa mmeshaandaliwa kuvuruga amani ya nchii. Sasa mlishashindwa kila jambo linawadodea.
 
Anayepumulia machine ni huyo mwalimu na phd holder ambaye hawezi kuandika sentensi moja ya kiingereza kilichonyooka
 
Wameingia choo cha kike kama lissu alivyotumiwa Meseji ya kudanganywa Rais amekutana na wakurugenzi

Ila jana Mnyika aliongea kiuoga kiuoga maana hawana uhakika na wanachokisema
Na zamu hii tutawasugua kweli kweli, si mmeomba kusuguliwa
 
Anayepumulia machine ni huyo mwalimu na phd holder ambaye hawezi kuandika sentensi moja ya kiingereza kilichonyooka
Yaani CCM tumewashika zile rungu mbili mmebakiza kupiga kelele tu, sasa na kalio zimedakwa. Safari hii lazima kuwakomesha kabisa kwa usaliti na ukibaraka wenu. Haiwezekani mtumwe na wazungu kuja kuleta ukoloni tena ktk nchi yetu. Mgekuwa na mgombea ambaye hajatumwa tungebishana sera ila kwa sasa ni mwendo wa kuwakomoa vibaraka nyie na subirini baada ya uchaguzi washenzi nyie lazima muhame nchi mabwege wakubwa vibaraka wa wazungu
 
Weeee Mwanaccm kindakindaki.

Ukweli nikua kama katibu mkuu wa chama, iyo ni haki yake na wajibu wake.

Lazima tuhoji.
 
Wasi wasi ni akili Twitter ni chanzo cha habari cha haraka zaidi duniani
 
Tatizo wenzako wanapumulia mashine. Kama mna akili anzieni kwenye corona, muone mlivyowajinga na wapumbavu ktk nchi hii. Mlidakia hoja za wazungu kumbe mlikuwa mmeshaandaliwa kuvuruga amani ya nchii. Sasa mlishashindwa kila jambo linawadodea.
Umekazania Corona yaani kwa miaka mitano maendeleo ni kuondoa Corona CCM mnalaana nyingi.
 
Back
Top Bottom