Chadema strategist mnalijua hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema strategist mnalijua hili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kulwa12, Dec 26, 2011.

 1. k

  kulwa12 Senior Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naomba niwakumbushe wanamikakati ya kisiasa ( political strategists) wa chadema juu ya hili.

  Chama chochote cha kisiasa kinacholenga kuchuku uongozi wa dola lazima kipitie hatua kuu mbili za kimkakati katika ukuaji

  (1)unity of opposition
  hii ni hatua ya kwanza ya kimkakati katika ukuaji wa chama,ambayo chama kinajipambanua kama chama halali cha upinzani (legitimate political oppostion) pia kinatumia muda mwingi katika hatua hii kupinga sera,maamzi na mambo mbalimbali yanayofanywa na chama tawala,hii ikiwa na lengo la kupata public attention na kutengeneza political base na zaidi kupata wawakili shi (wabunge) zaidi bungeni na kua kambia rasimi ya upinzani (chadema imepitia hatua hii).

  Na mnaweza kulifanya hili kwa kuchagua agenda mmoja kuu ya kukitambulisha chama chenu na kuvutia wanachama na kujipambanua kama chama cha upinzani (chadema ilifanya hili kwa kuchagua vita zidi ya ufisadi/mafisadi na ruswa kama ajenda yake kubwa)katika hatua hii kinachowaunganisha ni upinzani wenu kwa chama tawala (unity of opposition),lakini hatua hii tu haiwezi kukifanya chama kupata uungwaji mkono wa kutosha ili kupata uongozi wa dola.

  (2)unity of construction

  hii ni hatua ya pili ya kimkakati ambayo ndio inakiiandaa chama kuchukua uongozi wa dola.katika hatua hii nguvu kubwa inawekwa katika kuuza sera mbadala kwa wananchi,na zaidi kueleza mtawafanyia nini wananchi katika nyanda zote afya,elimu,ajira nk,na pia mnaaenda mbali zaidi kutekeleza kwa vitendo kwa wananchi baadhi ya mambo ambayo yako ndani ya uwezo wenu.Katika hatua hii,mnaonesha majibu saidi kwa matatizo ya wananchi na sio kutumia muda mwingi kukosoa chama tawala kimekosea nini bila kuonesha majibu mbadala:

  Angalizo kwa chadema:

  Mimi naamini chama cha chadema kimeshapita katika hatua ya kwanza ya ukuwaji(unity of opposition) na kinatakiwa kwenda hatua ya pili sasa (unity of construction),hii itafanya chama kijiweke wazi zaidi kwa wananchi walio wengi na kuonesha nini tofauti yake ya kisera katika nyanda zote ukilinganisha na chama tawala (ccm).

  hii itajenga kuaminika kwa chama,pia kuonesha wapiga kura kwamaba chama sasa kimeiva na kikotayari kuchuo dola.Vyama vingi vya upinzani vinafanya kosa la kubaki katika hatua ya kwanza tu ya ukuwaji,hii haiwezi kukifanya chama kishinde na kupata dola,kitaishia kupata wabunge tu!,inakifanya chama kieendelee kuonekana mbele ya umma kama chama cha upinzani tu,na sio chama kinachoweza kuchukua dola! Strategist wa chadema liangalie hili,msisubili kuuza ilani ya uchaguzi 2015 mkategemea ndani ya kampeni mtajijengea uhalali wa kutosha kuonekana mbele ya wapiga kura kama chama dola.

  Onesheni chama tawala kimeshindwa tayari na ni adui dhaifu,nendeni katika hatu ya pili ya ukuwaji (unity of construction) itawapa nafsai ya kuuza zaidi sera zenu kwa wananchi na sio kutumia muda wote kuuza agenda mmoja(ufisadi) na kuipinga serikali tu,wakati ni huu wa kutoka kuwa chama cha upinzani kwenda kuwa chama chenye kujiaanda kushika dola.

  Na hata ikitokea chama kikapata uongozi wa dola moja kwa mmoja bila kupitia hatua ya pili ya ukuwaji,hakitakua na manufaa na kitapoteza umaarufu wake mapema,kwani wananchi wanakua hawajui hasa kwa undani sera za chama hichi,na nini hasa kinalenga kuwafanyia wananchi kama kipaumbele katika kutatua matatizo yao!

  Kwani mara nyingi chama kinapewa madaraka kwa imani kitatatua matatizo yote kwa wakati mmoja.

  Hili ndilo lilolikuta chama kipya cha democratic cha japan,ilibidi waachie madalaka baada ya miezi mitatu tu ya kushika dola.
  Politica strategist.
   
 2. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Well said mkuu
   
 3. C

  Choveki JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kwani vyama na wanasiasa wa Tanzania wana strategist? nadhani mara nying wanaenda na ma Opportunist.
  Na ndiyo maana miaka 50 baada ya uhuru bado siasa zetu ni bora liende! Je umeiona ile post ya wanasiasa wanavyolala bungeni? Wengine hadi udenda (ndiyo udenda) unawatoka, si chama tawala si upinzani wote mbonji mtindo mmoja!
   
 4. k

  kulwa12 Senior Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsante mkuu
   
 5. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Tutalifanyia kazi wazo lako.
   
 6. k

  kulwa12 Senior Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  safi sana mdau,tunajenga kwa njia hii.
   
Loading...