Elections 2010 CHADEMA stop the campaigns NOW!!!!

Dawa ni kukaa mita mia moja kutoka kituoni kulinda wasilete kura feki na kuziingiza ndani
 
Nitajitolea kulinda kura za Upinzani na sihitaji kulipwa pesa zaidi ya mabadiliko tu. Tufahamu pia kwamba si kila atayetaka kujitolea apewe hiyo kazi, hapana tuzingatie historia ya mtu toka kabla ya kampeni kuanza mpaka wakati huum, tunaounga mkono mabadiliko tunafahamiana iwe ni ofisini, mataani au vijiweni. Nipo tayari kuhakikisha sisiem wanafungasha virago mwaka huu.
 
kwa kuna haja kubwa ya kujitolea kuwa mawakala ili kuziba mianya ya mbinu mfu ambazo wamezoea kuzitumia, hii ni kazi ya kila mmoja wetu mpenda maendeleo na mabadiliko ya kweli. Tanzania yenye neema inawezekana, na uchaguzi wa mwaka huu ndiyo utaamua kama watanzania tuko serious au tu wasanii. tuhamasishe, tupige kura , tulinde kura
 
Kweli wanatakiwa mawakala walio na moyo wa uzalendo, hapa tu ndio ccm wanaposubiri kuwashangaza watu wanaotegemea kuona mabadiliko.

CHADEMA USHINDI TAYARI.Ili wakabidhiwe serikali lazima waudhihirishie ulimwengu kuwa wanaweza kulinda RASILIMALI ZA NCHI ZIKIWEMO KURA ZA WAPIGA KURA VINGINEVYO WATANZANIA HATUTAWAELEWA.SISI TUKO BEGA KWA BEGA NANYI ila jukumu la uongozi ni kutoa mikakati watekelezaji ni sisi kwani tuko pamoja.TUNATAKA MIKAKATI IANDALIWE TUPEWE MUDA MUAFAKA.
 
nadhani a fair move ni kwamba tupige vita wizi wa kura bila kujali itikadi ya chama au nini.... kumbukeni kwaamba njia nzuri ya kupinga maovu ni kufanya kwa vitendo

My point: CCM, KAFU, CHADEMA na vyama vingine vyote... msiibe au kuchakachua kura!!!

Tanzania bila wizi inawezekana
 
Dawa ni kukaa mita mia moja kutoka kituoni kulinda wasilete kura feki na kuziingiza ndani
hata ukae mita kumi mazee... wanaotumika ni wanawake, tena wamejitanda kanga na ushungi na huruhusiwi kumkagua... walishapraktis na imelipa maeneo fulani ya tanganyika
 
Nakubaliana na mtoa mada kwamba Chadema kama wanataka ushindi ni lazima wajipange kulinda vituo vyote vya kupigia kura, hata vile ambavyo hawajasimamisha wagombea wa udiwani au ubunge. Ni lazima waandae timu ya walinzi wa kura kila kituo watakaofanya kazi ya ulinzi kwa muda wote na wasiondoke kituoni mpaka matokeo yatangazwe. Vilevile inabidi waandae watu wa kuwaletea mahitaji ya muhimu palepale kituoni, mahitaji kama vile chakula na maji. Ikibidi wawashirikishe wapigakura wote wanaoitakia mema nchi yetu.

Jambo jingine ni kwamba, tume ya uchaguzi inatumiwa na ccm ili ishinde. Mbinu wanayotumia ni kwamba, tume imeandaa vituo hewa vingi vya kupigia kura. Idadi ya vituo hivi ni miongoni mwa vituo vyote vilivyoandaliwa na tume kwa uchaguzi wa mwaka huu. Vituo hivi vinatumikaje? Vituo hivi vinapangiwa wasimamizi na tume lakini havina wapiga kura! Masanduku ya kura katika vituo hivi huletwa kituoni yakiwa tayari yamejaa makaratasi ya kura ambazo ccm hushirikiana na tume kufanikisha hilo zoezi. Makaratasi haya huwa tayari yameshapigiwa kura kwa mgombea wa ccm wa aidha udiwani, ubunge au urais. Masanduku haya huwekewa kura chache za wapinzani ili kuonesha kwamba watu wa vyama mbalimbali walishiriki kupiga kura katika vituo hivyo hewa. Je, kadi za kupigia kura katika vituo hivi hewa hutoka wapi? Ccm hufanya uchakachuaji huu siku kadhaa kabla ya siku ya kupiga kura wakishirikiana na tume kwa kutumia kadi ambazo hununuliwa kutoka kwa wapiga kura ambao hupewa pesa kidogo kati ya Tshs 5,000 na 50,000. Hili zoezi tayari limeshaanza kwa hiyo Chadema watch out! Baada ya zoezi hili, hizi kadi huchomwa moto. Rejea kadi zilizochomwa kwenye ofisi za tume kule KEKO kweye majengo ya Bohari kuu (GOVERNMENT STORE).

Chadema, pamoja na kupiga kampeni, lakini pia hakikisheni munaandaa mikakati ya kulinda kura za watanzania ambao kwa hali ya pekee wamejiandaa kukipigia chama chenu. Mkifanikiwa hilo, USHINDI NI WENU! Mungu awabariki! Amen!
 
Kweli wanatakiwa mawakala walio na moyo wa uzalendo, hapa tu ndio ccm wanaposubiri kuwashangaza watu wanaotegemea kuona mabadiliko.

Je hii ya katiba ya nchi kuhusu kumtangaza rais na hakuna kuhojiwa na chombo chochote cha sheria tumejipangaje nayo?

Utaratibu wa
uchaguzi wa
Rais Sheria
Na.20 ya 1992
Na.20 ib.5
Sheria Na.34
ya 1994
Na.34 ib.10


41 (6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi
kuliko mgombea mwingine yeyote.

(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.


Wakati na muda
wa kushika
madaraka ya
Rais
Sheria ya 1984
Na.15 ib.9

42.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema
iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa
kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla
ya kupita siku saba. (Katiba haisemi chochote kama rais aliyetangulia atakatlia ikulu)
(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtu
aliyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katika
ibara ndogo ya (3), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miaka
mitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais.
(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-
(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti
hicho atakula kiapo cha Rais; au…..
 
Yes. Insemekana wameshaandaa mabilioni kwa kazi hiyo. Hata hivyo inabidi tufanye kila linalowezekana kuifanya hiyo kazi ngumu. majimboni, waandaliwe wapiganaji wa kupita kila kituo kuangalia hali halisi siku ya kampeni (pikipiki inatosha kwa kazi hiyo). Camera (za kawaida au za simu), ziwepo standby, hasa yale maeneo korofi, kurekodi hali au tukio lolote linalotia mashaka

CHADEMA people, where are you? Toeni mbinu bw. saa nane naenda kwenye kikao cha kujipanga kwenye jimbo letu. Nipeni inputs za kwenda kudiscuss huko...


Hivi mtu ukifuatwa unapewa pesa, ukubali kusaini matokeo yoyote yale ya kura, NI LAZIMA UFANYE HIVYO? Huwezi kupokea kisha wakati wa kusaini, kama hukubaliani nayo, UNAKATAA? Huu ni ujinga ambao Watanzania tunapaswa KUACHANA NAO! Si kila anayekupa pesa ukampigie kura unampigia, na si kila anayekupa pesa ukubali matokeo ya kura unafanya hivyo!

Wenye nguvu na utashi wa kuamua ni SISI! Mbona tunajiuza wenyewe hata utu wetu na akili zetu? Mbona tunakuwa WATUMWA wakati tupo huru?
 
Jamani, naomba nifahamishwe hivi ni kweli CHADEMA originally ilikuwa ni CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO? Is this true?
 
Back
Top Bottom