CHADEMA stop the campaigns NOW!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA stop the campaigns NOW!!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tuko, Sep 28, 2010.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nimeweka title kali kidogo kwa sababu nataka kudraw attention ya wadau wa CHADEMA. Actually mi ni mdau wa CHADEMA na niko huku jimboni, bega kwa bega na mgombea ubunge tunapambana na mwanaccm mmoja.

  Pamoja na umuhimu na juhudi tunazofanya katika kampeni zetu, naomba, timu za wagombea udiwani, ubunge, na rais, zifikirie kutoa muda (pengine kwa kusimamisha kampeni), na kujipanga jinsi ya kuzuia wizi wa kura. Nimegundua kuwa inaweza kuwa ni sawa na mtu unapita ukipanga miche bora, kumbe nyuma yako shetani anapita akizingoa na kupanda magugu. Mwisho wa siku ukigeuka nyuma huna kitu.

  Yafuatayo (naamini yamefanyiwa kazi), naomba tuyape majibu yake

  Tutahakikishaje kura zetu zinalindwa katika maeneo ambayo hamna wagombea ubunge na/au udiwani? Hii Tanzania ni kubwa aisee, tusi assume tu kuwa kuna watu watakuwa mawakala, CCM are very smart in that. Ni nani atakayepita na kuhakiki majina na idadi ya wapiga kura katika maeneo haya ya pembezoni yatakapobandikwa hizo cku 8 kabla ya uchaguzi? Yapo mengi ambayo inabidi tuyaangalie...

  Naomba pamoja na mbinu nyingine, tuangalie kama hizi zitatusaidia; Kuweka mawakala zaidi ya mmoja kila kituo (kwa ticket ya vyama vingine vidogo vinavyoshiriki uchaguzi) ili kupunguza urahisi wa kununuliwa, kuanza kuunda timu za mawakala kila jimbo, na pengine Dr Slaa anapopita aseme sentensi chache kuwapa moyo na hamasa (ikiwezekana hata kukutana na baadhi yao wakati wa mapumziko), kuwasiliana na wagombea wote wa ubunge na kuwaelekeza namna ya kuomba kopi ya daftari la wapiga kura kwa maeneo yao, ili kulikagua na kujipanga kutokana na kila kituo kinavyoonekena (huku kwetu tunafanya juhudi, karibia tunalipata), wanaCHADEMA naomba muongeze mbinu hapa...
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Tupo wote kwenye hilo lakini karata turufu ya CCM ni kuwanunua mawakala wa Chadema ili wasaini matokeo ya mezani badala ya kuhesabu kura.

  Chadema wakiweza hilo basi ushindi hauna utata hata kidogo.
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Yes. Insemekana wameshaandaa mabilioni kwa kazi hiyo. Hata hivyo inabidi tufanye kila linalowezekana kuifanya hiyo kazi ngumu. majimboni, waandaliwe wapiganaji wa kupita kila kituo kuangalia hali halisi siku ya kampeni (pikipiki inatosha kwa kazi hiyo). Camera (za kawaida au za simu), ziwepo standby, hasa yale maeneo korofi, kurekodi hali au tukio lolote linalotia mashaka

  CHADEMA people, where are you? Toeni mbinu bw. saa nane naenda kwenye kikao cha kujipanga kwenye jimbo letu. Nipeni inputs za kwenda kudiscuss huko...
   
 4. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuko nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa, naongezea - CHADEMA iwekeze zaidi katika kuhakiki wapiga kura na kuhakikisha mawakala wao (wa uhakika) wanakuwepo katika vituo vyote (namaanisha katika majimbo yote) katika ile wiki ya uchaguzi hadi matokeo yanatangazwa. Ni vyema kuanza kudunduliza fedha sasa kwa ajili ya kuwawezesha mawakala. Gharama za mawakala nchi nzima ni kubwa kuliko tunavyodhani, hivyo ni vyema mipango ifanyike sasa. Watanzania wapenda maendeleo tutawachangia kwa kadri tutavyoweza.
   
 5. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Moja la nyongeza, hata kabla ya wakati wa kupiga kura kufika tumeisha habarishwa juu ya watu wanaotumwa kununua kadi za kupigia kura kwa wananchi. Hilo nalo ni muhimu sana kuliangalia katika kipindi hiki na pia kutafuta kujua hizo kadi za kupigia kura baada ya kununuliwa wanaozinunua watazitumiaje katika kuchakachua matokeo? Dr. Slaa na wagombea wengine iwe wa urais, ubunge na udiwani katika kampeni zao juu ya mbinu hiyoa na kuwashauri wananchi wasikubali kuuza vitambulisho vyao kwa sababu wakikamatwa watafunguliwa mashtaka na watakaopata shida ni wao. Wasidanganyike!
   
 6. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ninaiunga mkono hoja. Mwaka 2000 nilishududia kwa macho yangu majulimsho ya Kura katika jimbo la Uchaguzi. Siku kura zilipojulimshwa na kwa mabishano makali, Prof. Lipumba alimzidi Mkapa kwa kura zaidi ya 500. lakini kesho asubuhi yalipobandikwa kwenye mbao za matangazo, Mkapa alimzidi Prof. Lipumba kwa zaidi ya kura 2000.

  CHADEMA kama mnasikia, bila kuwa na Mpango-mkakati wa kulinda Kura, harakati zote zitakwenda na maji.
   
 7. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  [/QUOTE]

  Hili si la Chadema, ni la wapenda mageuzi wote. popote ulipo uwe tayari kuwa wakala, uwe tayari kulinda kura zisichakachuliwe. tukishirikiana tutawashangaza.
   
 8. G

  GAGL Senior Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono hoja asilimia mia kwa mia
   
 9. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  A very well written article and a genuine concern that need addressing.

  Itabidi nimtafute mgombea wangu wa ubunge nijitolee kusaidia kwenye kituo changu
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180

  Kama unakwenda kwenye kikao wakumbushe wenzako kwamba CHADEMA ni ya wote kwa sasa hakikisheni kwamba;
  1. Ziundwe kamati za wakereketwa kwa majimbo yote bila kujali kuna wagombea udiwani na ubunge ktk jimbo husika, lengo ni kulinda kura za rais msiweke wa vyama tofauti.
  2. Kumbukeni kwa kila jimbo lazima wapo wanpenzi wa Dr.Slaa hata kama hakuna wagombea ubunge
  3. Leo asubuhi nimeongea na jamaa yangu yuko Ludewa anasema Dr.Slaa anao wapiga kura wengi lakini chadema hakijaweka wagombea ubunge na udiwani ni vema kupwapata wapenzi wa chadema ili walinde kura za slaa Ludewa.Chama kiwalipe posho na kuwapa ahadi pia baada ya ushindi-post election benefits
  4. Kwa kufanya hivyo lazima tutapata watu ambao hawatakubari kurubuniwa na hata wakiwepo ni wachache kwani watu wanataka mabadiliko.
  5. CHADEMA msipuuze hata jimbo moja msiangalie uwakilishi wa wabunge an diwani tu kwani Dr.Slaa anapendeka nchi nzima hasa Ludewa wanalalamika hamjawafikia
  6. WEKENI WAKALA KWA KILA JIMBO MKUBALI HASARA KWANI MANUFAA YATAFUTA HASARA HIYO.HUUU NI NUWEKEZAJI KWA CHADEMA REWARDS WILL BE REALIZED COME 1st september2010
  Nawasilisha
   
 11. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chadema sio Dr Slaa na Mh Mbowe pekee yao,CHADEMA ni ya watanzania wote wapenda mabadiliko.
  Haya ni mabadiliko ya Lazima.na lazima tushinde.
  Tanzania bila ku-overhaul serekali nzima tutarudi kwenye utumwa na umaskini wa kutupwa.
  Sasa kazi ya kulinda kuhesabu kura ni yako na mimi
  .pale ulipo.
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  historia inaonyesha vyama tawala huwa haviogopi yote hayo, huwa vina-deal na mtangaza matokeo tu!sijui umejitayarishaje!
   
 13. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kuna vituo vingapi vya kupiga kura Tanzania nzima? Je kila mkoa/wilaya (chama) unaweza kushiriki vipi kuandaa wasimamizi wake, na pale inapobidi kuwasambaza siku ya kupiga kura bila kujali eneo analoishi ili kuzuia uwezekano wa kuhongeka hata kabla ya siku ya kura. Naamini kila mkoa/wilaya/jimbo likijipanga vyema kwa kufuata maelekezo na usimamizi wa taifa, mabadiliko yanaweza kuonekana.
   
 14. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe inaonyesha ni mtaalamu sana wa mbinu za kuiba kura. Je huko CCM ndiyo ilikuwa shughuli yako huko kabla mwaka huu hujaruka ukuta? :becky:
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Wameanza kuandikisha shahada za kupigia kura siku zote sikujua kwamba hii kazi inafanyika jana usiku mnamo saa nne nilitembelewa na mjumbe wa nyumba kumi kwa sababu wanajua mimi ni mwana CCM wakaniambia wanataka kujua kama shahada yangu niliihakiki wakati tume ilipita kuandikisha upya daftari la wapiga kura ,nikawambia sikuhakiki kwa sababu niliwasikia tume kama huna tatizo na kipande chako huna sababu ya kwenda huko wakasema basi tunataka kuandikisha wanachama wetu ili tuone wangapi watatupigia kura ,mimi nikawambia mwaka huu mimi nitapigia upinzani kwa sababu naipenda sana nchi yangu siwezi kuiweka rehani kwa miaka mingine mitano
  Basi wakaniambia eti watakuja kuongea tena na mimi leo kwani wanaona labda nilikuwa na uchovu wa Kazi kwa hiyo haukuwa muda mwa faka wa kuongea wakiondoka waliataka kuacha chupa ya mvinyo
  nikajiuliza hivi kweli kura yangu naweza nikaiiuza kwa chupa ya mvinyo
  Lazima mkakati thabiti ufanyike wa kuhakikisha tunalinda kura wenzetu wa pinzani wanaweza kuandikisha watu watakao jitolea hata bila kulipwa na vyama na kushirikiana na wananchi wenye mapenzi mema kuhakikisha haki inatendeka leo nimetayarisha maji ya pilipili wakija nawamwagia ha ha
   
 16. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaishi Mbezi ama Kimara? :becky:
   
 17. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu uko kwenye team ya kuhakiki wapiga kura toka sisi m?
   
 18. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Niko nyanda za juu kusini, nitajitolea ktk kituo changu bila malipo yoyote.
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  CUF na CHADEMA na vyama vingine (kasoro TLP) vinapaswa kushirikiana kuhakikisha CCM haifanikiwi kuiba kura zao. Tofauti zao zibaki kisera ila vita yao iwe kuingoa CCM tuu. Kati yao yeyote akishinda kuna uwezekano wa kushirikiana katika kuijenga upya nchi hii.
  Nimesema kasoro TLP kwa vile tayari bosi wa TLP anampigia kampeni kiongozi wa CCM, tunadhani huo ndio msimamo wa chama chao maana hakuna kiongozi mwingine wa TLP aliyempinga mwenyekiti wao katika hizo kauli zake
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kweli wanatakiwa mawakala walio na moyo wa uzalendo, hapa tu ndio ccm wanaposubiri kuwashangaza watu wanaotegemea kuona mabadiliko.
   
Loading...