CHADEMA si Legelege-Dr Slaa

CHADEMA si Legelege-Dr Slaa

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kamwe chama hicho hakitakubali kuwa legelege katika kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba inayowaunganisha wanachama wote.
Alisema kuwa licha ya kuzushiwa propaganda nyingi ikiwemo udini na ukabila, lakini chama hicho kimefanikiwa kuzishinda hali aliyoelezea imewakomaza katika safari yao ya kuchukua madaraka.

Kauli hizo alizitoa jana mjini Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya CDT, ikiwa mwanzo wa ziara yake ya kukiimarisha chama.

Dk. Slaa alisema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010, chama hicho kiliwaahidi Watanzania kuwa kama kingeshika dola, kingekuwa imara kusimamia serikali itakayowatumikia wananchi.

Alibainisha kuwa ili kuitimiza ahadi hiyo, chama hicho kamwe hakiwezi kuwa legelege kwa wanachama na viongozi wasiotaka kufuata katiba na taratibu za chama.

"Watanzania tulieni, tulieni, tulieni. Chama hiki kipo kwa ajili ya kuwatumikia ninyi na kusimamia maslahi yenu. Acheni ushabiki kwenye masuala mazito," alisema.

Dk. Slaa alisema amekuwa akipigiwa simu na watu wengi wakimuulizia hali ya mambo inavyokwenda ndani ya chama hicho, hasa baada ya uamuzi wa Kamati Kuu kuwavua uongozi baadhi ya makada wake akiwemo mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

"Mimi nawaambia watulie tu… Nawaambia waviamini vikao vya chama chao, ndani ya CHADEMA hakuna mtu mkubwa kuliko katiba. Wote hapa tunaunganishwa na katiba.

"Chama hiki kimepita kila aina ya propaganda ikiwemo hii ya juzi ya ugaidi, zote tumezishinda na tutaendelea kuzishinda. Hata hii ya sasa inayosukumwa na mipango ya hujuma inayopangwa na CCM, wakishirikiana na vyombo vya dola na watendaji wa serikali, tunazidi kuimarika na kutukomaza kwenda kushika dola.

"Wakati wa kampeni mwaka 2010 tuliwaambia Watanzania kuwa tunakwenda kusimamia maslahi ya Watanzania. Tulisema elimu bure, mwaka jana wameamua kutuiga, tulisema vifaa vya ujenzi vishuke, pia wameamua kutuiga, lakini wameshindwa kutekeleza," alisema kiongozi huyo huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi hao.

Dk. Slaa alisema kuwa CCM wameshindwa kutekeleza kile kilichokuwa kikisemwa na CHADEMA, ambayo sasa inaamini ikiingia madarakani itatimiza mambo iliyowaahidi wananchi.

Safari yapata matatizo

Ziara ya Dk. Slaa jana iliingia dosari baada ya magari aliyokuwa akiyatumia kupata hitilafu za kiufundi zilizosababishwa na kile kinachodaiwa ni mafuta machafu waliyoyaweka katika kituo kimoja cha mafuta kilichopo wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Mafuta hayo yaliyafanya magari yaliyokuwa kwenye msafara huo kushindwa kwenda mwendo uliotarajiwa, na hivyo kusababisha Dk. Slaa na timu yake kufika katika viwanja vya mkutano saa 12 jioni.

Dk. Slaa leo anatarajia kwenda mkoani Kigoma ambako atahutubia mikutano mbalimbali ya hadhara pamoja na kufanya shughuli za kuimarisha chama kila eneo atakalolitembelea.

Source:Tanzania Daima Alhamisi

Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria mkutano..........

Slaa+kuhutubia+Kahama+1..jpg

Dr Slaa akiaga umati huo huku wananchi wakiwa na hamu ya kuendelea kumsikiliza..........
Slaa+kuagana+na+wananchi.jpg
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kamwe chama hicho hakitakubali kuwa legelege katika kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba inayowaunganisha wanachama wote.
Alisema kuwa licha ya kuzushiwa propaganda nyingi ikiwemo udini na ukabila, lakini chama hicho kimefanikiwa kuzishinda hali aliyoelezea imewakomaza katika safari yao ya kuchukua madaraka.

Kauli hizo alizitoa jana mjini Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya CDT, ikiwa mwanzo wa ziara yake ya kukiimarisha chama.

Dk. Slaa alisema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010, chama hicho kiliwaahidi Watanzania kuwa kama kingeshika dola, kingekuwa imara kusimamia serikali itakayowatumikia wananchi.

Alibainisha kuwa ili kuitimiza ahadi hiyo, chama hicho kamwe hakiwezi kuwa legelege kwa wanachama na viongozi wasiotaka kufuata katiba na taratibu za chama.

"Watanzania tulieni, tulieni, tulieni. Chama hiki kipo kwa ajili ya kuwatumikia ninyi na kusimamia maslahi yenu. Acheni ushabiki kwenye masuala mazito," alisema.

Safari yapata matatizo

Ziara ya Dk. Slaa jana iliingia dosari baada ya magari aliyokuwa akiyatumia kupata hitilafu za kiufundi zilizosababishwa na kile kinachodaiwa ni mafuta machafu waliyoyaweka katika kituo kimoja cha mafuta kilichopo wilayani Kibaha mkoani Pwani.
viwanja vya mkutano saa 12 jioni.
Dk. Slaa leo anatarajia kwenda mkoani Kigoma ambako atahutubia mikutano mbalimbali ya hadhara pamoja na kufanya shughuli za kuimarisha chama kila eneo atakalolitembelea.

Source:Tanzania Daima Alhamisi

Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?

Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?
 
Last edited by a moderator:
Mkombozi wetu Wilbroad Slaa (PhD) usisahau kuongelea mgao wa umeme unaotuletea umaskini mkubwa na kuminya ajira kwa vijana.
Dr Slaa wewe ni sauti ya Simba, ukiongea magamba wanatetemeka maana wamezoea Kikwete sauti ya KASUKU....
 
Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?

Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?

Acha kujigeuza msukule, Kikwete huwa anahutubia hadi saa tatu usiku kama mchawi hamsemi kitu. Watu wamemsubiri mkombozi wao toka saa nane hadi saa 12 halafu apite bila kuongea chochote sio uungwana.
Ni mbulumundu pekee anayeweza kujiaminisha kuwa kama watu wanashangilia huwezi kuwaambia tulieni.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?

Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?
Mkuu hivi unategemea Tanzania Daima wataandika nini, hata hiyo habari wameandika kiujanja ujanja kiukweli hali ni mbaya Chadema.
 
Last edited by a moderator:
ukweli ni kwamba mzee slaa alifika kahama saa 9 alasiri lakini alishindwa kufika uwanjani kwa kile kilichokuwa kinaonekana mjini hapo kuwa kuna dalili za kuzomewa na kufanyiwa fujo, hata hivyo mkutano haukuwa na watu kabisa mpaka ilipofika saa 11;30 aliamua kwenda kuwasailimia wananchi wachacche waliokuwepo uwanjani, lakini alipokaribia uwanjani alikutana na watu wmebeba mabango yaliyomzomea na mengine kuandikwa jina la zitto.

nashangaa leo eti wanadanganya kuwa alihutubia mkutano mkubwa, na wandanganya kuwa waliweka mafuta machafu mkoani pwani...teh teh....waseme ni kituo gani kama wanajiamini.

Leo yatakayomkuta kigoma ni mpya hatakaa asahau.... Brigedia Nyakarungu
 
mkuu molemo kuna gazeti linasema kwamba dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la tanzania daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?

Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?

toa ushahidi na unachokiandia.au unakimuhemuhe
 
Jf cku hizi ina vichaa! ? Wapi muh rais amehutubia mkutano wa nje had saa tatu Ucku?

Dog punguza viroba
 
Kuna picha za Nov 2011 ziliwekwa kwenye thread na Kurugenzi ya Habari CHADEMA zikidai ni mkutano ulifanyika Wilayani Kahama jana wakati ni ulaghai wa kiwango cha juu kabisa.

Imebidi MOD's waifunge hiyo thread.

Wananchi wameisha anza kuuelewa ulaghai wa CHADEMA na kwa sasa CHADEMA wako desparate mpaka wanachakachua picha.

Ukweli utaendelea kujipambanua kila siku
 
ben saanane: Nimekubali braza kazi za chadema na matendo yenu ya wazi bila uoga, hivyo naomba kadi ya chama nipo mwanza mjini mtaa wa sahara.

chama kinachukua maamzi magumiu sio kama magamba wanaogopana
 
ulitaka waandikeuongo utakaokufurahisha? yaani roho inawauma kweli mnavoona cdm inazidi kuchanja mbuga. na sasa msaliti/pandikizi lenu zzt lazma litoswe. andaeni sherehe ya kulipokea. nashauri wewe uwepo siku ya mapokezi.

Mkuu hivi unategemea Tanzania Daima wataandika nini, hata hiyo habari wameandika kiujanja ujanja kiukweli hali ni mbaya Chadema.
 
Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?

Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?

Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
 
Jf cku hizi ina vichaa! ? Wapi muh rais amehutubia mkutano wa nje had saa tatu Ucku?

Dog punguza viroba

Wakupunguza viroba ni wewe kwani huna data then bado unaleta ligi ya kijinga kabisa. Kwa kukusaidia tafuta mida ya kwisha kwa mikutano ya ziara ya Mwanza ya huyo nisiyetaka hata kumtaja jina wiki chache zilizopita halafu ndio uje na huo upuuzi wako.
 
kuna picha za nov 2011 ziliwekwa kwenye thread na kurugenzi ya habari chadema zikidai ni mkutano ulifanyika wilayani kahama jana wakati ni ulaghai wa kiwango cha juu kabisa.

Wananchi wameisha anza kuuelewa ulaghai wa chadema na kwa sasa chadema wako desparate mpaka wanachakachua picha.

Ukweli utaendelea kujipambanua kila siku

mi nilikuwepo mkuu watu walikuwa nyomi hadi juu ya miti asikwambie mtu
 
Back
Top Bottom