SlidingRoof.Heshima mbele!
Kwanza kabisa nikushukuru na nikupongeze kwa kutoa maoni yako.
Inawezekana unadhamira njema au mbaya.Au yawezekana kama ilivyokawaida yako kupinga pinga kila kitu kama ambavyo ulivyokuwa ukitumia kwenye jina lako lingine la awali.Nilidhani ulivyokuja kivingine ungebadilika kumbe sivyo.Tuyaache hayo,ngoja nirudi kwenye hoja.
Kuhusiana na hoja yako ya kuwa Cabinet yetu kuwa namapungufu nakubaliana na wewe.Lakini ukumbuke kuwa CHADEMA ina Wabunge 48 tu na Cabinet yetu ni ya watu 39. Katika Kuunda Baraza kivuli la watu 29 isingekuwa rahisi kila mmoja kumpatia taaluma yake kwani kuna wizara wangengongana na nyingine zingekosa kabisa watu. Lakini vili vile unatakiwa kujua pia sio wabunge wote wa CHADEMA wanaelimu kama hiyo unayaoitaka wewe. Tuna Wabunge 23 wa majimbo na kati yao 22 wamepewa Wizara bila kujali elimu zao kwa kuwa kwa kufanya hivyo basi wizara nyingi zingekuwa hazina wasemaji.Kati yao 16 tu wanatoka Viti Maalumu. Kwa chama chochote cha upinzani unapounda baraza kivuli huangalii CV za watu pekee vile vile kuna suala zima la siasa,umaeneo,jinsia n.k.Hivi ni baadhi ya vigezo vilivyotumika.Ndio maana unawaona kina Joseph Mbilinyi,Lema,Regia na wengineo. Vile vile ndugu yangu lazima ujue kuwa na PHD au uzoefu fulani sio hoja katika ufanisi wa kazi duniani pote.Ndio maana pamoja na uwepo wa PHD nyingi sana Tanzania lakini bado tunamatatizo makubwa ya msingi.leo Mnyika anaweza kuperform vizuri sana kuliko maprofesa na madaktari wengi ndani ya Bunge. Elimu sio kipimo cha ufanisi kwa mtazamo wangu.
Pili. Ni mapema mno kuanza kulikosoa baraza kivuli,baraza hili limeundwa mwezi februari hata miezi miwili haijaisha wala mafunzo kwa baraza hili hayajafanyika.
Tatu. Kama kuna Mbunge wetu yuko bize na Facebook au JF huo ni uhuru wake na kila mtu ana haki ya kufanya hivyo.Kila mmoja anaratiba zake kwani kuupdate status Facebook inachukua siku nzima?Wewe unapataej muda wa kufuatilia na wenzeko Facebook na kuandika huku JF?unafikiri mwenye kazi ni waizri peke yake?hata nyinyi mnapaswa kuwa bize kwenye maeneo yenu ya kazi.Sote tunategemeana.Uwaziri ni Political post na nyie ndio watendaji wenyewe.Nchi haiendelei kwa matamko na barua.Vitendo ndio vinabdili nchi.Hata hivyo Kila mtu ana haki ya kurelax na kumake fun.Kama wewe unamatatizo yako na huwezi kuwa na muda wa kuenjoy hilo ni tatizo lako.Usifanye maisha kuwa magumu.
Nne.Mkumbuke pia si kila mtu hupenda kufanya kazi kwa kutumia vyombo vya habari.Wapo wanaofanya kazi kimya kimya sio lazima nyie mjue kila kitu. Kila waziri wa CHADEMA anajua misimamo ya Sera za chama kulingana na hata ukituamsha usiku wa maneno utapewa misimamo yetu ya kisera na wameshafanya kazi kadhaa na wengine tupo kwenye maandalizi ya hoja binafsi kuhusiana na maslahi ya wafanyakazi.
Tano.Kwenye baraza letu majority ni wanaume na wanawake wote waliopewa nafasi wanaangalau digrii maoja na kuendelea.Acha mfumo dume,bado hujabaidlika tu?usitumie akili zako kujenga hoja zinazohitaji facts.
Sita.Naomi Kaihula yuko kwenye wizara sahihi kabisa.Kwa taarifa yako ni mmoja wa waanzilishi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania na ni Mwalimu.
Saba,Binafsi nakubaliana na wewe uwezo wangu ni mdogo kupewa Wizara,sio ya kazi na Ajira tu kama unavyoona wewe,sistahili kupewa Wizara yeyote ile lakini kwa kuwa ninajitambua kwamba ni mtu wa kujifunza na kujisomea na ni mchapakazi na hata walionipendkeza wanatambua hilo naamini nitafanya vizuri kama ilivyo kawaida yangu na mtakuja kushangaa.Kuna msemo unasema usikisifu kitabu kwa gamba lake la nje.Huwa najifunza haraka na kuendana na mazingira yaliyopo.Fuatilia rekodi zangu kuanzia shule ya msingi,sekondari,chuo kikuu na hata CHADEMA.Kumbuka hapa naongea in public na kuna watu wengi tu humu wanonifahamu vizuri.Give me enough time.
It can be done play your part.
Aluta Continua
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira