..exactly.
..hakuna matamko ya chama kuna matamko ya viongozi individually.
..pia walipaswa kuimarisha ngazi za kanda, mikoa, wilaya, etc.
..kwa mtizamo wangu Dr.Slaa alitimka kabla mfumo wa uongozi wa cdm haujakomaa. Sasa ilitakiwa anayefuatia aimarishe ule msingi uliowekwa na Dr.
..mikutano ya hadhara ina uzuri na ubaya wake.
..cdm ilikuwa inajaza umati wa watu ktk mikutano yao lakini ikija wakati wa uchaguzi matokeo siyo mazuri.
..kwa mtizamo wangu elimu inayotolewa kwa mikutano ya hadhara uwezekano mkubwa ni ya papo-kwa-papo / muda mfupi na hivyo haieleweki kwa walengwa.
..vilevile mikutano mikubwa ya viongozi toka makao makuu haiwajengei uwezo viongozi wa ngazi za chini. Chama kinapaswa kuwafunda viongozi huko mikoani na wilayani waweze kufanya shughuli za chama na wasiwe wategemezi kwa makao makuu ktk kukijenga chama.
..pia huu ni wakati wa ku recruit vijana ktk chama. Mnyika, Heche, Waitara, Halima Mdee, ..by 2020 watakuwa tayari wako kundi la wazee.
Cc
Nguruvi3,
Mag3