TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,868
- 5,753
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimehusishwa na harakati chafu za kukisambaratisha chama cha Alliance for Change and Transparent-TANZANIA (ACT-TANZANIA) ili kumkomoa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe anayehusishwa na chama hicho.
Akizungumzia uhusika wa CHADEMA kwenye mgogoro unaoendelea ndani ya ACT-TANZANIA, Katibu Mkuu wa muda wa ACT, SAMSON MWIGAMBA amesema Mwenyekiti wa muda wa ACT-TANZANIA, KADAWI LIMBU anashirikiana na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kukimaliza chama chao kutokana na kuhofia ACT ikiwa ni pamoja na kumshughulikia ZITTO ili aonekane ni mwanasiasa asiyefaa.
MWIGAMBA alisema baashi ya matamko na maamuzi ya chama yamekuwa yakiandaliwa kwenye moja ya CHUMBA CHA HABARI NCHINI AMBACHO MMILIKI WAKE NI MKEREKETWA WA CHADEMA.
Akithibitisha hilo, Mwigamba lisema ushahidi wa analolisema upo kwani Mwenyekiti wao ni MSHIRIKA KWENYE MOJA YA MAKUNDI YA MTANDAO WA KIJAMII WA WABUNGE WA CHADEMA, ambapo aliwahi kutuma ujumbe wenye kuwaeleza kuwa amekamilisha kazi ya KUWATIMUA yeye na prof.KITLA.
Chanzo: RAI NGUVU YA HOJA.