CHADEMA sasa yaliwa njama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA sasa yaliwa njama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 10, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,404
  Likes Received: 81,431
  Trophy Points: 280
  CHADEMA sasa yaliwa njama

  Mwandishi Wetu
  RAIA MWEMA
  Februari 9, 2011
  [​IMG]CUF, CCM wahofiwa kushirikiana

  [​IMG]Kamati ya Slaa, Zitto, Cheyo zakamiwa


  [​IMG]Lissu, Mdee watema cheche Bungeni


  MBINU zimeandaliwa kuhakikisha Kamati nyeti za Bunge, hasa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe haziwi mikononi mwa wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Taarifa za awali zilibainisha kuwa uamuzi wa CHADEMA kuunda Kambi rasmi ya Upinzani bila kuvishirikisha vyama vingine, hususan Chama Cha Wananchi (CUF) kwa madai kuwa ni chama tawala Zanzibar, ulilenga 'kukamata' kamati tatu muhimu zinazohusika na usimamizi wa moja kwa moja wa mwenendo wa serikali.

  Mbali na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma iliyokuwa ikiongozwa na Zitto, kamati nyingine ni ya Hesabu za Serikali za Mitaa iliyokuwa ikiongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibroad Slaa na Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu iliyokuwa ikiongozwa na John Cheyo.

  Raia Mwema imebaini kuwa mipango ya chini chini imekuwa ikifanyika kuhakikisha kamati hizo haziongozwi na wabunge wa CHADEMA na kwamba mianya inayoweza kutoa fursa wa kamati hizo kuongozwa na wabunge hao imeanza kuzibwa.


  Kati ya hatua zinazotajwa kulenga kuziba mianya ya wabunge wa CHADEMA kutwaa uongozi wa kamati hizo ni pamoja na mabadiliko ya kanuni yanayopigiwa chapuo na Chama Cha Wananchi (CUF) kuondoa neno “rasmi” katika Kambi Rasmi ya Upinzani.
  Mantiki inayotajwa katika kuondoa neno rasmi ni kuliweza Bunge kutambua kambi nyingine za upinzani Bungeni ambazo zinaweza kutoa wabunge wa kugombea uenyekiti wa kamati hizo nyeti.

  “Wanafanya hivyo kwa sababu kwa sasa ni CHADEMA pekee ndiyo inayoweza kuwasilisha majina ya wabunge kwa ajili ya kuwania kuteuliwa kuongoza kamati tatu muhimu katika uhai wa Bunge kutimiza jukumu lake la msingi la kuisimamia serikali. Kwa kawaida, jina la mgombea hutoa Kambi Rasmi ya Upinzani na wajumbe wa Kamati husika hupiga kura kumchagua.

  “Endapo neno rasmi litaondolewa kikanuni katika kutambua Kambi Rasmi ya Upinzani maana yake vyama vingine vitakula njama na CCM na kuwasilisha jina la mgombea wao na wakamchagua an hivyo uwajibakaji wa Mwenyekiti wa Kamati husika ukawa wa mashaka kwa kuwa kwa mfano, kama Mwenyekiti atatoka CUF ambacho ni chama tawala Zanzibar lazima maslahi yaSerikali yazingatiwe tu,” alisema mtoa taarifa wetu kabla ya azimio kuhusiana na kanuni kupitishwa jana.

  Raia Mwema limebaini kwamba kutokana na njama hizo, hali ya wabunge wa vyama vya upinzani katika Bunge linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma bado ni tete na dalili za awali zinabainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi kupitia wabunge wake kikionekana kufanikiwa kuimega kambi hiyo kisiasa.

  Wabunge waliochangia hoja iliyowasilishwa Bungeni na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, walidhihirisha wazi mgawanyiko mkubwa kati ya CHADEMA kwa upande mmoja na vyama vingine vya upinzani vya CUF, NCCR-Mageuzi na UDP wakiungwa mkono wa wabunge wa CCM kwa upande mwingine.

  Hoja ya Ndugai ilitokana na barua zilizoandikwa na wabunge wawili wa upinzani, Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF) na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, ambao walitaka kubadilishwa kwa kanuni za Bunge kuwalazimisha CHADEMA kushirikisha vyama vingine katika kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

  Kafulila alianza kwa kuonyesha umuhimu wa kuwa na umoja katika kambi ya upinzani lakini alionekana kuwapiga kijembe CHADEMA kwa kuonyesha kwamba hawana nia ya umoja huku akitoa mfano wa NCCR-Mageuzi kuongoza Kigoma na kukosa nafasi ya kutambuliwa bungeni.

  Aliyeonekana kukerwa na CHADEMA waziwazi alikuwa ni Hamad Rashid, ambaye bunge lililopota alikuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni, ambako yeye alieleza wazi kwamba CUF imekuwa na uungwana kushirikisha vyama vingine ikiwamo CHADEMA wakati walipokuwa na wabunge wengi.

  Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), naye alianza moja kwa moja kwa kutaka vyama vilivyoshindwa kukubali matokeo na kwamba vyama vya siasa visichochee vurugu, kauli ambayo ilionekana kushangiliwa na wabunge wa CCM.

  Wabunge hao walionekana kuungwa mkono na wabunge wa CCM waliochangia, akiwamo Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene na Mbunge wa Viti Maalumu Stella Manyanya, ambao walionekana wazi kuirushia vijembe CHADEMA.

  Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA, Halima Mdee, yeye alichangia huku akikatishwa mara kwa mara na kelele za wabunge wa CCM na hata baadhi ya vyama vya upinzani, lakini na yeye alionekana kurusha vijembe wazi wazi kwa CUF na CCM.

  Aliyeonekana kuwa mwiba kwa CUF, NCCR-Mageuzi na CCM alikuwa Mbunge wa Singida Mashariki, kupitia CHADEMA Tundu Lissu, ambaye alieleza wazi kwamba azimio hilo litakuwa na lengo la kuua upinzani na kuzuia uwajibikaji wa serikali.

  Lissu ambaye alikuwa mjumbe katika Kamati ya Kanuni iliyojadili barua za Kafulila na Hamad, alibainisha wazi kwamba alipinga moja kwa moja kubadilishwa kwa kanuni kutoa nafasi kwa vyama ambavyo yeye alisema vina mahusiano na CCM.

  “Barua ya Hamad na Kafulila ilikuwa ya kuomba badiliko ya kusema wenyeviti wa kamati za usimamizi wa fedha za umma watatokana na kambi rasmi ya upinzani bungeni, walisema ombi ili wao waruhusiwe kushika hizo nafasi za uenyekiti ili wagombee ambako vyama vyao havikufikisha asilimia 12.5,” alisema Lissu.

  Lissu ambaye aliingiliwa mara kadhaa na wabunge wa CCM na Spika Anne Makinda, alisema kwamba lengo la kubadili kanuni ni kuua upinzani rasmi bungeni na kwamba hakubalini na mpango huo.

  “Lengo la azimio hili kama inakusudiwa ama la, ni kuua upinzan. Chama cha CUF kina Makamu wa Rais, kimeunda serikali na CCM na kwa maneno yao wenyewe upinzani umekufa Zanzibar na hakuna kambi ya upinzani… ni kwa kupigiwa kura na chama chenye wabunge wengi ndio maana wanapiga makofi, kwa hiyo namna pekee, hii ni kambi rasmi ya upinzani itakayojengwa na kura ya CCM.

  “Haiwezekani wale ambao tunataka kuwaondoa madarakani wakatujengea kambi ya upinzani lakini si hayo tu, kitakachotokea, tukiruhusu chama kama UDP kama cha Cheyo kushikilia nafasi hizo kwa kuungwa mkono na CCM, maana yake ulinzi wa fedha za umma utapotea. Kwa utaratibu huu Watanzania wasahau kusikia ufisadi tena,” alisema Lissu.

  Kabla ya vikao vya Bunge kuanza mjini Dodoma, tayari Kambi rasmi ya Upinzani inayotambuliwa na Mabunge ya Jumuiya ya Madola kwa mujibu wa kanuni, ikiongozwa na CHADEMA, imekuwa katika msuguano na CUF.

  CUF ndicho kilichokuwa chama rasmi cha upinzani Bungeni, kambi iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashidi Mohamed, lakini sasa Kambi hiyo inaongozwa na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, bila kukishirikisha chama hicho kwa madai kuwa ni sehemu ya chama tawala katika moja ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mvutano wa vyama hivyo (CUF na CHADEMA) umeanza kuathiri vyama vingine vya upinzani vyenye wabunge wachache, hali inayotoa mwanya kwa wabunge wa CCM kudhibiti mwenendo wa Bunge.
  Moja ya njia inayotajwa kuweza kuzidi kudhoofisha Kambi ya Upinzani Bungeni ni kufanya mabadiliko ya kanuni, ili kanuni hizo zisitambue Kambi rasmi na badala yake zitamke Kambi ya Upinzani, hali inayoweza kuwapa nguvu wabunge wa CCM kuhodhi mhimili huo wa dola, bila kuwapo nguvu rasmi ya upinzani.

  Hadi vikao vya Bunge vinaanza mjini Dodoma, wabunge wa vyama vya upinzani wamekuwa hawana mipango ya pamoja kama ilivyo kwa CCM, ikibainika kuwa CHADEMA wamekuwa wakiendelea na vikao vyao, CUF na vyama vingine vyenye wabunge wachache vikijiangalia mustakabali wao katika kuta za ukumbi wa Bunge.

  Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, CHADEMA wanatimiza masharti ya kanuni kuunda Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni lakini kumekuwapo na wito wa kutaka wabunge wa vyama vingine washirikishwe kwenye kambi hiyo ili kujenga kambi imara zaidi.
  Hata hivyo, CHADEMA kupitia Kamati Kuu yake imeelekeza wabunge wake kutounda Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kukishirikisha Chama Cha Wananchi (CUF) kwa kuwa tayari ni chama tawala katika sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo pia hutoa wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri.

  Katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Wawakilishi hutoa wawikili rasmi ambao huwa ni wabunge wa Bunge la Tanzania na hivyo shughuli au majukumu ya baraza hugusa pia utendaji wa Bunge. Kutokana na Baraza hilo kugusa utendaji wa Bunge, kwa sasa halina Kambi ya Upinzani baada ya CUF kuwa sehemu ya utawala, mazingira yanayotumiwa na CHADEMA kuikataa CUF kwenye kambi.

  Lakini wakati hayo yakitokea wasiwasi umetanda kuwa huenda Spika wa Bunge, Anne Makinda akatumia mamlaka yake kinanuni kuzidi kuidhoofisha Kambi rasmi ya Upinzani ili kuwa na kambi ndogo ndogo zisizo na nguvu.

  Tayari CHADEMA imeonyesha hali ya wasiwasi katika taarifa yake iliyoandaliwa na Mkurugenzi wake wa Masuala ya Bunge na Halmashauri, John Mrema.

  Inaelezwa kuwa wasiwasi wa CHADEMA umetokana na mamlaka ya kanuni aliyopewa Spika kubadili kanuni za Bunge. Kanuni hizo zinazompa nguvu Spika kufanya hivyo, hata kama kwa maslahi ya chama tawala ni pamoja na kifungu cha 152 (3) kinasoma; “Spika kwa kushauriana na Kamati ya Kanuni za Bunge atakuwa na madaraka ya kuzifanyia marekebisho au mabadiliko Nyongeza za kanuni hizi,kulingana na mahitaji ya wakati,kadri atakavyoona inafaa”.

  Inaelezwa kuwa kutokana na kanuni nyingine kumpa Spika uwezo wa kuunda Kamati ya Kanuni za Bunge, ambayo inaweza kubadili kanuni, hali ya sintofahamu imetanda.

  “Spika ametumia vifungu vya kanuni kuamua kuunda Kamati ya Kanuni ili kuhakikisha kuwa wanafanyia marekebisho kanuni zilizopo na lengo likiwa ni kuondoa uwepo wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni na hivyo kuondoa nguvu za Kambi rasmi kuweza kuisimamia serikali na haswa kwenye kamati tatu za Bunge zinazojulikana kama kamati za kudumu za Bunge zinazosimamia fedha za umma , ambazo kwa mujibu wa kanuni zinapaswa kuwa na wenyeviti kutoka kwenye kambi rasmi ya Upinzani Bungeni,” anaeleza Mrema katika taarifa yake.

  Kutokana na hali hiyo, CHADEMA kimetoa angalizo la mapema kwa kulaani yoyote ya Spika na ama Bunge kufuta utaratibu huu na kuamua kuanzisha utaratibu mpya , ambao ni kinyume kabisa na utaratibu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola.

  Katika kulaani CHADEMA imeeleza kuwa, hatua ya Spika na ama Bunge kujaribu kufuta neno kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni , kwani huku ni kujaribu kuua utamaduni wa kidemokrasia ambao umejengeka Duniani pote wa kuwa chama kikuu cha Upinzani ndicho kinakuwa na mbadala wa Chama kinachotawala na hivyo wana wajibu wa kuisimamia serikali iliyoko madarakani , kwa kuteua mawaziri vivuli (mbadala).

  “Tunalaani hatua yoyote ya Spika na au Bunge ya kutaka kulazimisha chama ambacho kipo madarakani yaani kinatawala upande mmoja wa muungano , eti kiwe ni chama cha upinzani upande wa pili wa Muungano , yaani CUF hakiwezi kuwa na sifa ya kuwa chama cha upinzani wakati huo huo kikiwa ni sehemu ya chama tawala upande wa Zanzibar. Na ndio maana Baraza la Wawakilishi wamefuta kambi rasmi ya upinzani kwani hakuna chama cha upinzani ndani ya SMZ.
  “Tunawataka Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao kupaza sauti zao kuhakikisha kuwa kanuni za Bunge hazibadilishwi ili kukidhi matakwa fulani yenye lengo la kudhoofisha nguvu ya Upinzani Bungeni.

  “Tunamtaka Spika atueleze lengo la kubadilisha kanuni sasa ni nini haswa na ni kwa masilahi ya nani? Tutaendelea kufuatilia jambo hili kwa ukaribu , kwani ni kubwa na likiachwa lichezewe litafanya serikali kutotimiza wajibu wake kikamilifu na hakutakuwa na mtu ama chombo rasmi cha kuhoji mambo hayo.
  [​IMG]
   
 2. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ccm kwanini wao wanajiona ndo wana haki ya ku dikteti mamlaka yote ya uongozi wa nchi, hili kosa ni sawa na uhaini, wananchi tumechagua na sasa wanahodhi mamlaka yetu pia, jamani tufike wakati tuseme hapana
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CCM ama kweli sikio la kufa.................... Nilidhani baada ya kunyimwa kura na wananchi wangetafauta sababu au kwa kwa vile wanajua sababu tayari wangejirekebisha kwa kuwahudumia wananchi wao wanahangaika kuua upinzani ambao wanawawakilisha mamilioni ya wananchi.

  Mungu atusaidie Tanzania ili elimu ya uraia ienee kwa kasi zaidi. Vinginevyo watu wataendelea kufa kwa umaskini na maradhi.
   
Loading...