CHADEMA sasa ni taasisi imara zaidi

CHADEMA sasa ni taasisi imara zaidi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,484
Ni chama kikubwa kwa sasa tena kilichokua kwa viwango vya kukua.Ni chama kulichosaidiwa na CCM kuwa imara kwa ujinga tu wa CCM. CCM ilifanikiwa kutumia mbinu za kishenzi kuviua au kuvidhoofisha vyama vingine vilivyokua na nguvu na ikafanikiwa.

Lakini CCM kwa mbinu hizohizo za hovyo imegonga mwamba kwa Chama makini CHADEMA. Matokeo yake sasa CCM baada ya kushindwa kuiua CHADEMA sasa inajiua,imejnyonga yenyewe.

Nilikua nasubiri kwa hofu kifo cha CHADEMA 2013, 2014 CHADEMA iko hai. Kizuri zaidi kwangu na wengi wetu CHADEMA imeimarika na kukua mara dufu na hii ndio ikiwa ni mbaya kwa CCM. Sasa hivi CHADEMA ilipofikia hata Mbowe na Slaa waking'atuka CHADEMA itasonga mbele.Na jambo la kushangaza CHADEMA inapiganiwa, inatetewa na kujengwa na watu isiowafahamu na wala sio waajiliwa wala sio viongozi wake.

Mimi binafsi ni mmoja wa voluntier ninaeipigania kwa akili na nguvu zangu zote pia nimegundua kuna watu wengi wanaipigania CHADEMA kwa hiari zao na kwa siri kubwa. Mbinu chafu zimeshindwa sasa CHADEMA jipangeni kwa hila za kuandiiisha wapiga oura na kuzuia wizi wa kura 2015 ndo hii.
 
CDM ni mpango wa Mungu huo. Yatakufa yatakiacha chama hiki kikidunda
 
Chadema ni makini kwa kuteka watu muulize msack majibu anayo lakini siyo chama cha kutumikia watanzania.
 
Target ya ilikuwa kuimaliza CHADEMA kabla ya 2012.

Malengo yamekwama, wamekosa muelekeo tena.
Chadema chama cha kikabila na ukoo kwa upande huo kweli kiko imara make kama hujatokea mikoa yao uongozi ndani ya chama hupati.
 
CDM ni mpango wa Mungu huo. Yatakufa yatakiacha chama hiki kikidunda
Mkuu unazungumzia mungu yupi aliyeko chadema yani dhambi zote hizi wanazofanya chadema mpaka kumwagia watu tindikali tindikali bado awe nao hapana huyo mungu siyo huyu tunayemjua labda kama wanaye mungu mwingine tengeru.
 
Chadema chama cha kikabila na ukoo kwa upande huo kweli kiko imara make kama hujatokea mikoa yao uongozi ndani ya chama hupati.
Kama Kinana vile.

ok Watanzania tupo Tayari kuongozwa na ho wachaga wa kaskazini.
 
CDM ni mpango wa Mungu huo. Yatakufa yatakiacha chama hiki kikidunda
Mungu yupi mkuu? Huyo mungu atakuwa dhaifu sana amekubali Chadema kiwe chama cha upinzani.
 
Mkuu unazungumzia mungu yupi aliyeko chadema yani dhambi zote hizi wanazofanya chadema mpaka kumwagia watu tindikali tindikali bado awe nao hapana huyo mungu siyo huyu tunayemjua labda kama wanaye mungu mwingine tengeru.

Ukishindana na Chadema utazeeka mapema. I love u chadema
 
Ni kweli lakini kuna baadhi ya maeneo watu wameshindwa kutofautisha kati ya ccm na chadema kimatendo. Kwa mfano kipi kilichofanya wakose wabunge wa viti maalumu mikoa ya ruvuma, dodoma, njombe na hata tabora? Huu ni udhaifu uleule wa kiccm?
 
Chadema ni chama cha kupiga ruzuku
Ni chama ambacho hakina malengo endelevu.
Hakina mradi wowote zaidi ya kutegemea ruzuku na misaada kutoka kwa wafadhiri.
Ni chama ambacho kimepanga toka 1992 mpaka leo licha ya kuwa na wabunge 49 lakini viongozi wake wanamajumba Dubai na Ulaya.
 
Mungu yupi mkuu? Huyo mungu atakuwa dhaifu sana amekubali Chadema kiwe chama cha upinzani.

Maccm msiogope; Alituhakikishia kwa uhakika mno yule aliyetoroka kule zoo kuwa 2012 Pasaka haipiti kabla Chadema hakijafa na kufutika kwenye kumbukumbu za vyama Tz.
Nadhani he is right. Labda kule zoo wao huhesabu miaka tofauti na sisi. Kikwetu, huu 2015 mwaka wa uchaguzi na Chadema kinawanyima usingizi hao majifisadi na wale woote wanao waungu mkono ka nyiye. Tulieni, hiyo ni rasha rasha tu, masika not yet.
 
Mkuu unazungumzia mungu yupi aliyeko chadema yani dhambi zote hizi wanazofanya chadema mpaka kumwagia watu tindikali tindikali bado awe nao hapana huyo mungu siyo huyu tunayemjua labda kama wanaye mungu mwingine tengeru.

hivi like sanamu la igunga mmeshalilipa? linalalamika kutoswa na ccm baada ya kulidanganya lijitoe muhanga mlipe mabilioni ya epa
 
ccm ilishaishiwa mbinu ndio maana wrote tumeshuhudia mbinu za kuwahonga wali na T-shirt wapiga kura zikibuma na hivyo kuokolewa na mapingamizi ya kihuni kwenye uchaguzi
 
Back
Top Bottom