CHADEMA sasa imekuwa pango la wanyang'anyi

CHADEMA sasa imekuwa pango la wanyang'anyi

Son of Gamba

Mkuu,tamaa ni mbaya sana. Mbowe kaamua kuuza chama na hapo tunaamini kuwa chadema ni NGO na si chama cha siasa. Zao ni kutafuta wafadhili wa ndani na nje ya nchi. Sasa kwa mfadhili wa awamu hii,wameangukia pabaya.
 
Last edited by a moderator:
Mnajua nyie watu wa CCM mnavyozidi kupayuka ndio wenzenu CDM wanazidi kuwapokea sababu tangu lini nyie Gambaz mkaipenda chadema hadi kuionea Huruma nakuishauri isichukue makapi Ikifa sindio afadhali ibaki CCM peke yake kwani kuwepo kwa chadema nyie mnanufaika nanini
 
Lowassa amefuata taratibu zote za chama na amekuwa mwanachama. Amefuata taratibu zote za chama katika kukiwakilisha chama kuwa mgombea urais. Tatizo lako ni kwamba labda wewe hukusoma Katiba ya Chadema wakati unajiunga nacho (kama kweli wewe ni mwanachadema). Lowassa na friends of Lowassa wana haki zote za kuwa wanachama wa Chadema. Kukatwa siyo sababu tosha ya kuanza kuita watu wanyang'anyi. Tunajuaje kama wewe hukukatwa huku ulikokuwa kabla ya kukimbilia Chadema? Ungekuja hapa na kusema Katiba ya Chadema ina mapungufu inaruhusu hata manyang'anyi (pamoja na wewe) kujiunga tungekuelewa.

Lowassa amebadilisha msimamo, amefanya maamuzi magumu tunapaswa kumpongeza. Wapo wanasiasa nguli Tanzania wanaoheshimika wakina Warioba, Salim Ahmed Salim wamechoshwa na CCM lakini hawana ujasiri na uthubutu wa Mhe. Lowassa. Hivi wewe hujawahi badilisha msimamo wako maisha yako yote? N wewe tukuite kigeugeu?
 
Sio kosa lako,umeandika kama unahitaji bwana vile,lowassa kaondoka ccm sababu hakuna demokrasia ya kweli.
 
Je ni sahihi kwa chama tawala chenye vyombo vinavyozuia Na kupambana Na rushwa kuwa Na hao wala rushwa Na mafisadi Na kutowachukulia hatua? Au wakienda chadema ndio mafisadi wakiwa CCM safi?

Mkuu hapa sasa wewe unaongea kinyume. CHADEMA kupitia Dr. Slaa alisema Lowasa ni fisadi na akikasirika aende mahakamani watakutana huko maana ushahidi anao. CHADEMA nzima ikaanza kuimba wimbo huo kuwa Lowasa ni fisadi. Wengine kama mchungaji Msigwa wakaenda mbali zaidi kwa kusema, nanukuu,"atakayemchagua Lowasa akapimwe akili". Hii ina maana Lowasa alikuwa fisadi akiwa CCM na kwa sasa kwa vile amehamia CHADEMA amekuwa msafi. Upo hapo?
 
Mvua inyeshe jua liwake TUTAONDOA MFUMO WA KIFISADI WA CCM HATA KWA KUMTUMIA SHETANI. Mrema akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alifanikiwa kwa kutumia wahanga wa ujambazi kukamatpa Majambazi halisi na Silaa kibao.
 
Mafisadi CCM hawawezi kuisha mfumo unaruhusu nyerere aliiacha ccm ya wakulima Na wafanyakazi lakini Leo ni ya wafanyabiashara wakubwa Na masikini
 
Hilo neno fisadi lishapoteza maana Yake.Chadema tunakazi moja tu kuchukua dola na kusambaratisha mtandao wa mafisadi (CCM).mengine yote ni historia. tushasema hatufukui makaburi.
 
Son of Gamba,ulichokiandika kinaakisi wasiwasi wangu juu ya Lowassa.

Kwa uhakika simuamini hata kwa asilimi ZERO.Mnisamehe sana wapenzi wa Lowassa.
 
cd na dvd za kila aina zitatumika kuinusuru ccm hisipotee,lkn wananchi na watanzania wamesha amua kuiondosha ccm tu wajiandae kuwa kub

View attachment 273208

SAFARI.jpg

View attachment 273210

Ukawa and CCM.jpg

View attachment 273217

View attachment 273218

Niliahidi.jpg

J. K..jpg

profilepic 2015.JPG



mizambwa
inaniuma sana!!!
 
Mkuu hapa sasa wewe unaongea kinyume. CHADEMA kupitia Dr. Slaa alisema Lowasa ni fisadi na akikasirika aende mahakamani watakutana huko maana ushahidi anao. CHADEMA nzima ikaanza kuimba wimbo huo kuwa Lowasa ni fisadi. Wengine kama mchungaji Msigwa wakaenda mbali zaidi kwa kusema, nanukuu,"atakayemchagua Lowasa akapimwe akili". Hii ina maana Lowasa alikuwa fisadi akiwa CCM na kwa sasa kwa vile amehamia CHADEMA amekuwa msafi. Upo hapo?

Sasa lowasa keshajieleza na anaonekana hana hatia,mafisadi wamebakia ndani ya ccm vipi mbona unatokwa na mate kibao wewe ni kati ya wale waliogawana za escrow pale 6tanbic bank nini?
 
Son of Gamba,ulichokiandika kinaakisi wasiwasi wangu juu ya Lowassa.

Kwa uhakika simuamini hata kwa asilimi ZERO.Mnisamehe sana wapenzi wa Lowassa.

Huna haja ya kuwa na shaka wala wasiwasi juu ya wewe kujiondoa cdm,hata jana alihamia makongoro na vyovyote atakuwa na wapiga kura angalau 5000 wataisadia cdm kusonga mbele
 
Back
Top Bottom