CHADEMA sasa imekuwa pango la wanyang'anyi

CHADEMA sasa imekuwa pango la wanyang'anyi

Son of Gamba

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2012
Posts
4,718
Reaction score
6,979
Inasikitisha sana kuona chama kilichokuwa na sifa hapa nchini kupinga vita ufisadi na rushwa, ndio kinakuwa chama kikuu cha kupokea mafisadi ya kila namna. Inasikitisha sana hasa ikizingatiwa kuwa Mafisadi haya yanajiunga na chama hiki baada ya kukatwa kutoka CCM. Mtu kama Lowassa, ameondoka CCM sababu ya kukatwa na sio ameondoka kwa kupiga vita rushwa na ufisadi. Lowassa hana mapenzi ya dhati na CHADEMA. Lowassa ni kama mtu anayeshika mwamvuli wakati mvua inanyesha, ili asilowane maji. Lowassa amenyeshewa mvua CCM kakimbilia mwamvuli ambao ni CHADEMA.

Hakika kwa hili CHADEMA wamepoteza mwelekeo kabisa, ni kama mbwa anapoamua kula matapishi yake mwenyewe! Kwa hili wamewakatisha tamaa Watanzania waliokuwa wanawaamini kuwa wapo kwa ajili ya kupambana na rushwa na ufisadi na sio kuwakumbatia mafisadi. CHADEMA walipaswa kuwa makini sana na maamuzi yao. Mimi binafsi simlaumu Lowassa kwenda CHADEMA bali nawalaumu sana CHADEMA kukosa msimamo dhabiti. Lowassa ameingia CHADEMA ili kujaribu kutimiza ndoto zake binafsi za kuingia Ikulu na sio eti ana mapenzi na CHADEMA. Lowassa ana uchu wa madaraka, na sababu ameyakosa CCM sasa anajaribu kama atayapata CHADEMA. Mtu kama huyu ni hatari sana, na viongozi wa CHADEMA walipaswa kulibaini hili mapema sana.

Binafsi naamini kabisa ndani ya CHADEMA wapo watu wenye upeo wa kufikiri na kuchambua mambo, ambao tayari wameshahoji hili swala na watachukua maamuzi sahihi kabisa, hata kama hawataondoka CHADEMA lakini kura zao hawatampa huyu Fisadi Lowassa siku ikifika.

Mtu ambaye hawezi kuzisimamia kauli zake mwenyewe, kamwe hataweza kusimamia matakwa ya watu wengine pia. Lowassa ameonyesha dhahiri kabisa kuwa ni mtu mwenye kigeu geu. Mtu kama huyu kuwa Rais ni hatari sana. Kwa kauli yake mwenyewe alisema kamwe hataondoka CCM, tena akasisitiza kuwa mtu asiyemtaka ndio aondoke CCM. Lakini cha ajabu yeye ndio amekuwa wa kwanza kuondoka.

Leo hii anasema anataka kuwa rais ili awakomboe Watanzania kutoka kwenye lindi la umaskini. Hivi kigeu geu kama huyu ambaye bado hajaupata huo urais ameshaonyesha kutoaminika na kauli zake mwenyewe, je, akiwa Rais tutaamini vipi kuwa hatageuka na kufanya mambo anayoyataka yeye kwa faida yake na marafiki zake ambao pasipo shaka wote tunajua kuwa ni mafisadi kama yeye???? Hivi CHADEMA tutawaamini vipi tena kama wameshindwa kusimamia kauli zao sasa hivi, je itakuwa vipi hawa CHADEMA watakaposhika madaraka ya nchi na kuwa chama tawala??

Nimesikitika sana kuona chama nilichoamini kuwa ni chama bora cha upinzani sasa kimegeuka na kuwa pango la wanyang'anyi. Hivi inawezekana kweli mbwa mwitu akaingia kwenye kundi la kondoo na kuwa mchungaji wa kondoo na kondoo wakabaki salama??? Tuache ushabiki, tukubali ukweli, kwa hili CHADEMA wamechemka mbaya! CHADEMA wamewafanya Watanzania kama chapati. Unaigeuza upande huu kisha unaigeuza upande wa pili au wamewafanya Watanzania kama samaki, unamla upande huu kisha unageuza upande wa pili pia unakula!

Ukweli ni kwamba kama itatokea Lowassa akashinda urais(ingawa naamini hawezi kushinda urais), ushindi utakuwa ni wa Lowassa na friends of Lowassa na hautakuwa ushindi wa CHADEMA. Ushindi utakuwa ni wa Lowassa na familia yake na wale wote atakaotoka nao CCM. Lowassa atakuwa na kiburi mbaya sana sababu itajulikana wazi kabisa bila ya yeye CHADEMA si lolote, si chochote. Ingekuwa bora mara elfu kama CHADEMA wangemsimamisha mtu mwingine mbali na Lowassa na kushinda uchaguzi hapa tungesema CHADEMA wameshinda urais.

Najua mpo humu ndani watu mtakao toa matusi na kashfa mbali mbali kuhusu mada hii. Lakini huo ndio ukweli, mpende, msipende CHADEMA sasa limekuwa pango la Mfisadi na wala rushwa, ambao wamekatwa na vyama vyao sasa wameamia CHADEMA ili wapate nafasi za kuendeleza matakwa yao binafsi. Kwanini wasubiri kukatwa ndio wakimbilie CHADEMA??????

TAFAKARI, CHUKUA HATUA.​
 
kwanza huna elimu ya siasa kwakuwa politics determine who has power not who the truth ,,,,,,,,,,,am proud of being CHADEMA na kama mwanachama natambua kwamba kupata mwanachama ni product nzur ya siasa za chadema
 
CCM ndilo lilikuwa pango la wanyang'anyi kwa miongo kadhaa, sasa wanatoka adharani kujisalimisha.
 
Je ni sahihi kwa chama tawala chenye vyombo vinavyozuia Na kupambana Na rushwa kuwa Na hao wala rushwa Na mafisadi Na kutowachukulia hatua? Au wakienda chadema ndio mafisadi wakiwa CCM safi?
 
kama ushindi utakuwa friends of lowasa na sio chadema basi lowasa angehamia act au tlp kama wewe mjinga unavoamini.son of gamba
 
kwanza huna elimu ya siasa kwakuwa politics determine who has power not who the truth ,,,,,,,,,,,am proud of being CHADEMA na kama mwanachama natambua kwamba kupata mwanachama ni product nzur ya siasa za chadema

Hawa wafungwa wanauelewa mpana sana wa siasa kuliko wewe. Hebu pitia haya mawazo mujarabu uache kuendekeza taarabu :

Tanzanian inmates in HK prisons have made the following comments: 1. Edward Lowassa's craving for the presidency ("craving" not too strong a word, he's made so many attempts - see https://en.wikipedia.org/wiki/Edward_Lowassa) is a serious concern. His main motivation seems to be power, not the good of the country. 2: Lowassa's close friendship with JK and CCM over so many years ....is he now likely to expose and clean up the corruption installed by CCM? 3. Slaa has worked so hard for so many years to build up Chadema, and has tireless and fearlessly exposed corruption in Tz. He was in a winning position to take Tz to a new level of government ....why has he been preferred to someone with highly questionable credentials? 4. So many prominent people are leaving CCM to join Chadema. Is their motive the good of the country or ambition to have power? 5. People in the Philippines keep electing bad politicians, because they are media stars etc. Is Tz going to fall for the same trap?
 
Wakuu, tukiondoa hii ishu ya reachmond isio na ushahidi wa wazi kwamba Mh Lowasa anahusika,ni ishu gani nyingine ambayo Mh Lowasa ameifanya katika nchi hii ambayo inaweza kuonyesha kwamba yeye ni fisadi??.
 
Dozi inakolea vzr kwann ukawa msimuombe na JK,NAPE,KINANA WAJIUNGE NANYI
 
Kumekuwepo na mawazo(kwa wakosoaji wa chadema) binafsi nayahita mawazo bapa,juu ya chadema kula matapishi yake hasa kwakitendo cha kumpokea waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashifa ya Richmond,mh Edward Lowassa,kiukweli dhana ya kula natapishi ni dhana dhaifu na isiyokuwa na nashiko ktk harakati za ukombozi,kwa takilibani miaka 50 ya utawala wa ccm maisha ya watanzania yamegubikwa na wingu zito kama zile harakati za kupambana na maambukizi ya virusi hatari vinavyosambaratisha kinga ya mwili,kwa dhana hiyo ikiwa matapishi yanaweza kudhibitika kutibu ugonjwa huu ni mjinga tu mwenye maradhi hayo atakataaa kuyatumia matapishi,hivyo ccm ni maradho sugu ambayo dawa yake imepatikana nayo ni matapishi(lowasa)nilazima tuyale ili tuwe salama,kazi njema wakuu
 
Wakuu, tukiondoa hii ishu ya reachmond isio na ushahidi wa wazi kwamba Mh Lowasa anahusika,ni ishu gani nyingine ambayo Mh Lowasa ameifanya katika nchi hii ambayo inaweza kuonyesha kwamba yeye ni fisadi??.

Lowasa hana kashfa na hata hiyo ya richmond ameshaielezea na wahusika wote wamakaa kimya na ukimya huu tunaamini kuwa lowasa aliwajibika kuinusuru serikali ya baba Ritz,leo hii baada ya miaka 8 lowasa akiwa nje ya serikali tumeshuhudia kashfa kibao zikifanywa na viongozi mbalimbali wa serikali ya ccm,ma ccm ni wachafu sana
 
Hawa wafungwa wanauelewa mpana sana wa siasa kuliko wewe. Hebu pitia haya mawazo mujarabu uache kuendekeza taarabu :

Cd na dvd za kila aina zitatumika kuinusuru ccm hisipotee,lkn wananchi na watanzania wamesha amua kuiondosha ccm tu wajiandae kuwa kub
 
Son of Gamba

Siku zote ninaamini, "Ukiwa Maarufu; Utakuwa Na Harufu."

Ninadhani umaarufu wake ndo unamfanya awe "Habari Kuu Kila Kuchapo".

Nimeikumbuka kauli ya mh. Kikwete wakati akimnadi Lowasa wakati wa mkutano wa kampeni zake za uraisi mwaka 2010 akiwa jimboni Monduli, alimwinua Lowasa na kusema, "Hili ni jembe, nipeni nikafanye kazi naye."

Ninajaribu kuamini kuwa, hata Kikwete alijua wazi kuwa Lowasa si fisadi labda kama na yeye alisema uongo, tumlaumu hata yeye pia.

Lkn kama alifanya ili kuwahadàa wananchi wa Monduli kwa kusudi la kumpa kura, basi si dhambi kwa CDM kumnadi kuwa ni safi na si fisadi. Au anakuwa ni fisadi kwa vile CDM wanasema kuwa ni msafi; lkn hakuwa fisadi wakati ule alipotambulishwa na Kikwete kwa vile alikuwa ni boss wa ccm?

Tuweni wakweli jamani!
 
Last edited by a moderator:
Hakuna Mkuu ni chuki binafsi Na Mkuu lowassa amewaambia wampeleke mahakamani au watoe ushahidi
 
Back
Top Bottom