Chadema sasa imarisheni tovuti yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema sasa imarisheni tovuti yenu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Richard, Apr 2, 2012.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Ni furaha kuona kwamba katika miaka ya hivi karibuni chama cha CDM kimeweza kwa kiasi kikubwa kufanya kampeni nchi nzima kuelimisha wananchi.

  Ni katika kazi hiyo ndio tumeona wapiga kura wakipata mwanga na mwono juu ya kuchambua ipi pumba na upi mchele katika kufanya maamuzi ya nani anafaa kupewa mkataba wa kuwaongoza iwe jimboni au kule ikulu.

  Mimi ni mmoja wa vijana ambao nimekuwa nikifanya kazi kwenye mazingira ya techonology nikiwa ughaibuni na nimekuwa nikiguswa sana na mwenendo mzima usio wa kasi wa ukuaji wa sekta hii na hususan kwenye siasa.

  Ingawa serikali nyingi zinazoendeshwa na vyama vyenye kukumbatia ufisadi zimekuwa zikiangalia kwa makini mwenendo wa mawasiliano ya jamii kwenye mtandao, bado vijana ambao wamekuwa wakijifunza technology hizi wamekuwa hatua nne mbele.

  Vijana wa karne hii sasa wanafahamu kuwasiliana kwa kutumia simu za mikononi ambazo tayari zina mtandao wa internet hivyo kuweza kufanya usafirishaji (live streaming) wa habari kuwa wa rahisi zaidi.

  Nilipata nafasi ya kutembelea mji wa Benghazi nchini Libya mwanzoni mwa mwaka 2011 kabla ya vurugu za kisiasa hazijaanza na hatimae kuja kumtoa madarakani aliekuwa raisi wa nchi hiyo Muamar Gadaffi. Niliweza kuona mbinu mbali mbali za wanaharakari katika kujaribu kufikisha ujumbe kwa wale wasioleewa hususan nje ya Libya.

  Moja ya mbinu kubwa kabisa kuweza kutumiwa na wanaharakati hao ilikuwa ni mawasiliano ya mtandao wa internet ambapo kulikuwa na ofisi yenye web server. Kazi ya server hii ni kuhakikisha inahifadhi taarifa zote muhimu za matukio yaliyojiri siku hiyo na kuzisambaza kwa watumiaji popote pale walipo duniani yote hayo ikiwa "live" au "live smooth streaming public points".

  Pia server hiyo ina kazi ya kusambaza taarifa hizi kwa server zingine kulingana na na maelekezo ya system admins. Pamoja na harakati hizi serikali inaweza kufunga mtandao wa internet nchi nzima ikitaka kwa kuogopa kuona kwamba labda kuna sababu ambazo hazipo.

  Sasa leo nimetembelea tovuti ya CDM na kwa kweli sijafurahishwa baada ya kuona kwamba mara ya mwisho kufanya masahihisho ilikuwa ni tarehe 28/02/12.

  Pili, tangia matokeo ya uchaguzi yatoke jana hakuna habari hizo kwenye tovuti hii wala hata angalu sentesi yenye "maquee" kuonesha "headline" kwamba Nasari ashinda kiti cha Arumeru Mashariki.

  Je kwanini imekuwa hivyo kwani jambo hili ni dogo sana kuzingatia ukubwa wa chama chetu hiki kwa sasa kipo kila kona ya nchini mwetu.

  Nnapenda kutoka mawazo yangu kwamba wahusika hasa kurugenzi ya habari na uenezi ni lazima waiboreshe tovuti hii na kuanzia leo iendeshwe kitaalam- yaani ikichapisha habari live na kupokea mambo mbalimbali kutoka kwa sisi wanachama tulio mbali lakini tulio karibu kwa sababu ya technology.

  Hii nimetoa tu kama ukumbusho kwani niliwahi kutoa maoni yanayolingana na haya hapo awali nafikiri miaka miwili iliyopita ambaypo ylikuwa yakishauri chama chetu hiki kukazania kuelimisha wapiga kura.

  Kurugenzi hii itafute mtaalam ambae atalipwa kulingana na kazi yake na apewe "requirements" zote na "live streaming" iwe mojawapo.

  Raisi Barak Obama na Raisi wa sasa wa Russia Vladmir Putin wameshinda chaguzi za urais katika nchi hizo baada ya kuona kwamba wakitumia "social media" inaweza kulipa na walijitahidi kutoa muda wao kufanya mahojiano na wapiga kura kupitia mwenye mtandao wa "internet", hivyo "engagement" yao mtandaoni imewasaidia sana.

  Server inaweza kuhifadhiwa mahala popote pale duniani na ikaendeshwa "remotely" bial shida yoyote. Pia njia ambayo inatumika kwa sasa ya kutuma ujumbe kwa njia ya simu za mikononi bado ipo limited kudogo ikizingatiwa kwamba ni mitandao miwili tu na Vodacom na Zain ndio inatoa fursa hii.

  Inaweza kutengezwa pia njia kwenye web server hiyo hiyo kwa ajili ya kupokea texts messages na mambo yote yakawa mswano.

  CDM haitujachelewa tuanze sasa na iwe haraka.

  Aluta continua.

  Hakuna kulala mpaka kieleweke.
   
 2. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ni ushauri makini!
  Viongozi wetu wanatumia vichwa kufikiri.
   
 3. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Ukitumia sana kichwa kwa kila kitu utanyonyoka nywele na kuzeeka haraka.
   
Loading...