CHADEMA sasa ijipange kweli

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Chama cha Demokrasia na Maendeleo sasa kinapaswa kujipanga kweli kweli kama kinataka kubakia katika ramani ya siasa za Tanzania na hatimaye kuwa chama kinachoweza kuaminiwa kuliongoza taifa letu muda si mrefu ujao. Viongozi, wanachama na mashabiki wake hawawezi kuendelea kuficha vichwa vyao mchangani kwasababu wanaamini wanapendwa na hivyo hawataki kufanya mabadiliko ya lazima ya kuamua hatima ya chama hicho.

Kuna mambo mawili ambayo yanatishia hatima ya chama hiki licha ya maneno mazuri ya kujipa moyo. Jambo la kwanza ni matokeo ya uamuzi wa kubadili gia angani mwaka jana na la pili ni ujio na umaarufu wa Rais John Magufuli.

Baada ya kufanya uamuzi ambao ulitushangaza baadhi yetu wa kumuondoa Katibu wao Mkuu ambaye walimuandaa wenyewe na kumpitisha kuwa mgombea urais na badala yake kumchukua mgombea wa urais kutoka CCM – chama tawala – na kumfanya mgombea wake CHADEMA ilijipa jeraha ambalo bado hawajakubali kuwa ni jeraha.

Mojawapo ya matokeo yaliyoambatana na uamuzi huu ni pamoja na kusababisha mpasuko wa kifikra ndani ya chama hicho, kwa wanachama na mashabiki wao. Wapo ambao waliona kuwa uamuzi ule ulikuwa ni wa lazima na wanaapa hata leo kuwa umekinufaisha sana chama kuliko kukiumiza. Hawa wanaonesha namba za matokeo ya urais na ongezeko la wabunge wachache bungeni lakini pia wanaonesha jinsi CHADEMA ilivyofanya vizuri kwenye baadhi ya maeneo kuliko ilivyokuwa nyuma.

Wale ambao wanaamini katika kubadili gia angani hawako tayari kufikiria mara mbili uamuzi wao ule kwani kunaweza kuwafanya waonekane hawakufanya uamuzi wa hekima na hivyo wameamua kuyatetea kwa namna yoyote. Hili si jambo baya hasa kama wanafanya hivi wakiwa ni waamini wa kweli wa mabadiliko yale. Na hadi hivi sasa inaonekana ni kweli wanaamini hili.

Upande wa pili wa hili ni wale ambao baada ya kubadili gia angani walishindwa kuielewa CHADEMA kabisa. Hawakuelewa ulazima wa kubadili gia lakini zaidi hawakuelewa ulazima wa kuachana na ajenda dhidi ya ufisadi ambayo ilikuwa imeitofautisha CHADEMA na CCM kwa muda mrefu. Wapinga ufisadi karibu wote walikuwa ni mashabiki wa asili wa CHADEMA lakini baada ya chama kuamua kukumbatia na kutolea udhuru wale ambao walituhumiwa kwa ufisadi kwa muda mrefu wakiwa ndani ya CCM wapinga ufisadi wengine wote ilibidi wajiulize kama imani yao iliwekwa mahali pasipostahili.

Hawa wengine waliumizwa kwasababu kuwa waliwekeza imani yao kwa uongozi ambao walijua uko tayari kushika nchi; kwamba dakika za mwisho walijionesha kuwa hawakuwa wamejipanga ilikuwa ni kikwazo kikubwa cha kifikra kwa wengi.

Jambo la pili ni kuwa ajenda ya ufisadi tangu wakati ule wa kampeni mara moja ikahamia kwa John Magufuli. Haikuhamia kwa chama. Kama ilivyokuwa kwa CHADEMA kuwa ajenda ya mabadiliko iliondolewa kwa chama ikawekwa kwa mtu na ajenda ya vita dhidi ya ufisadi haikupelekwa kwa chama ikapelekwa kwa mtu. Watu hawa wawili – Lowassa akiwa CHADEMA na John Magufuli akiwa CCM waliamua kubeba ajenda ambazo hawakuwa nazo tangu awali; Lowassa hakuwa sehemu ya mabadiliko na Magufuli hakuwahi kuwa bingwa wa vita dhidi ya ufisadi. Mabadiliko ya watu hawa wawili yalibadilisha mwelekeo wa siasa za nchi; wapo wana CCM waliokuwa wanaamini katika Lowassa (kama walivyoimba wengine kule Dodoma) ambao waliamua kumfuata Lowassa “alipo wawepo”. Na upande mwingine wapo wana CHADEMA walioamini katika vita dhidi ya ufisadi kiasi kwamba hawakuwa tayari kubadilika na wakaamua kumuunga mkono Magufuli.

Magufuli aliposhinda urais – bila ya shaka kwa msaada mkubwa sana wa wapinga ufisadi – alikuja na ajenda ya kusafisha nchi na kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma. Aliingia akiwa mkali katika matumizi ya fedha za umma na madaraka kiasi kwamba kwa siku chache tu jina lake likatangazwa Afrika nzima (kama siyo duniani) kuwa Tanzania imepata mpiga vita ufisadi. Hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kama Lowassa angeweza kujipatia umaarufu wa namna ile; Lowassa mwenyewe katika kampeni yake hakujionesha kuwa anataka kuingia kuongoza vita dhidi ya ufisadi zaidi ya kutoa ahadi za kuwapa neema watu wa makundi mbalimbali!

Magufuli ameingia na gia ya kusafisha na kupanga upya serikali; kuleta nidhamu na uwajibikaji na kuona taifa linafanya kazi kweli kweli kama kweli tunataka kuendelea. Kosoa kosoa nyingi ambazo tunaziona hasa kutoka upinzani kubwa ni za kisiasa; ni zile zenye kujaribu kupata pointi za kisiasa. Tatizo la hili ni kuwa kama Magufuli atafanya anayoyaahidi – na tumeona ameanza – na wananchi wa kawaida yaani ‘wanyonge’ wakaona anatetea maslahi yao ni vigumu kuona ni jinsi gani upinzani unaweza kuimarika isipokuwa miongoni mwa wasomi (elites).

Hata masikini na wanyonge wanaoonekana wanashabikia upinzani watakapoona kuwa maslahi na mahitaji yao yanatimizwa chini ya Magufuli utafika wakati tutaona mikutano ya upinzani ikivutia wafanyakazi na watu ambao maslahi yao yamepotea sasa.

NI kwa sababu hiyo CHADEMA ni lazima ikae chini hasa sasa baada ya kumpata Katibu Mkuu mpya; ni lazima ijiulize kwa uwazi kabisa na ukweli (candidly) ni wapi walikosea, walikosea vipi na ni vipi wasahihishe makosa yao. Lakini pia ni lazima wajiulize ni kwa namna gani chini ya kiongozi maarufu kama Magufuli CHADEMA bado kinaweza kubakia chama makini na muhimu? Ni vipi maeneo yanayoongozwa na CHADEMA yanaweza kuwa mfano wa kiutawala na mafanikio? Je, kuendelea na maandamano ya kupinga au kushambulia tu ni mkakati mzuri? Haya ni maswali ambayo viongozi na wanachama wa CHADEMA wanapaswa kuyatafutia majibu.

Nje ya hapo ndoto ya kushika madaraka katika miaka kumi ijayo itaendelea kuwa ndoto ambayo waota ndoto yake hawaamki kwani wanaamini kuwa ndoto yao ni maisha ya kweli.
 
Kwa uongozi huu wa kukurupuka na udikteta wananchi watawachoka soon,Magufuli mwepesi sana kwa wapinzani,ngoja uone
 
Kama chaguzi wenyewe kama za Z'bar Siwezi kukukatalia.

Ila naona Huwezi kula, kulala Bila kutoa Chadema.
 
Mleta uzi unakopi habari ya raia mwema unatuletea hapa unajisifu kwamba na wewe ni mchambuzi.leta yako sio kukopi.
 
Mkuu umeongea ukweli tupu........Kwa sasa haijulikani CDM inasimamia nini......mrengo wanaoufuata na Sera havijulikani.....kimekuwa chama cha matukio tu.....
 
Mm nashangaa hv Dr mihongo angeweza kuleta wabunge wengi kama ilivyo kwa sasa? Jibu hangeweza kwa hiyo angalia faida na hasara
 
Umejuaje kuwa hangeweza......kumbuka tayari ilishaundwa ukawa ( wakati inaundwa Lowasa alikuwa na wana ccm wenzake wanawakejeli wapinzani kwa hoja mbali mbali, kama tume huru, matokeo ya rais kupingwa mahakamani)

Sijui kwa nini hamuoni kuwa nguvu ya kuungana ndio imeleta wabunge wengi na sio Lowassa.....
 
Mkuu umeongea ukweli tupu........Kwa sasa haijulikani CDM inasimamia nini......mrengo wanaoufuata na Sera havijulikani.....kimekuwa chama cha matukio tu.....
Hivi adui hasa wa ACT ni nani? Ni CCM au CDM?
 
ACT adui wake mkubwa ni umasikini, ujinga na maradhi.....non of ur mention
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo sasa kinapaswa kujipanga kweli kweli kama kinataka kubakia katika ramani ya siasa za Tanzania na hatimaye kuwa chama kinachoweza kuaminiwa kuliongoza taifa letu muda si mrefu ujao. Viongozi, wanachama na mashabiki wake hawawezi kuendelea kuficha vichwa vyao mchangani kwasababu wanaamini wanapendwa na hivyo hawataki kufanya mabadiliko ya lazima ya kuamua hatima ya chama hicho.

Kuna mambo mawili ambayo yanatishia hatima ya chama hiki licha ya maneno mazuri ya kujipa moyo. Jambo la kwanza ni matokeo ya uamuzi wa kubadili gia angani mwaka jana na la pili ni ujio na umaarufu wa Rais John Magufuli.

Baada ya kufanya uamuzi ambao ulitushangaza baadhi yetu wa kumuondoa Katibu wao Mkuu ambaye walimuandaa wenyewe na kumpitisha kuwa mgombea urais na badala yake kumchukua mgombea wa urais kutoka CCM – chama tawala – na kumfanya mgombea wake CHADEMA ilijipa jeraha ambalo bado hawajakubali kuwa ni jeraha.

Mojawapo ya matokeo yaliyoambatana na uamuzi huu ni pamoja na kusababisha mpasuko wa kifikra ndani ya chama hicho, kwa wanachama na mashabiki wao. Wapo ambao waliona kuwa uamuzi ule ulikuwa ni wa lazima na wanaapa hata leo kuwa umekinufaisha sana chama kuliko kukiumiza. Hawa wanaonesha namba za matokeo ya urais na ongezeko la wabunge wachache bungeni lakini pia wanaonesha jinsi CHADEMA ilivyofanya vizuri kwenye baadhi ya maeneo kuliko ilivyokuwa nyuma.

Wale ambao wanaamini katika kubadili gia angani hawako tayari kufikiria mara mbili uamuzi wao ule kwani kunaweza kuwafanya waonekane hawakufanya uamuzi wa hekima na hivyo wameamua kuyatetea kwa namna yoyote. Hili si jambo baya hasa kama wanafanya hivi wakiwa ni waamini wa kweli wa mabadiliko yale. Na hadi hivi sasa inaonekana ni kweli wanaamini hili.

Upande wa pili wa hili ni wale ambao baada ya kubadili gia angani walishindwa kuielewa CHADEMA kabisa. Hawakuelewa ulazima wa kubadili gia lakini zaidi hawakuelewa ulazima wa kuachana na ajenda dhidi ya ufisadi ambayo ilikuwa imeitofautisha CHADEMA na CCM kwa muda mrefu. Wapinga ufisadi karibu wote walikuwa ni mashabiki wa asili wa CHADEMA lakini baada ya chama kuamua kukumbatia na kutolea udhuru wale ambao walituhumiwa kwa ufisadi kwa muda mrefu wakiwa ndani ya CCM wapinga ufisadi wengine wote ilibidi wajiulize kama imani yao iliwekwa mahali pasipostahili.

Hawa wengine waliumizwa kwasababu kuwa waliwekeza imani yao kwa uongozi ambao walijua uko tayari kushika nchi; kwamba dakika za mwisho walijionesha kuwa hawakuwa wamejipanga ilikuwa ni kikwazo kikubwa cha kifikra kwa wengi.

Jambo la pili ni kuwa ajenda ya ufisadi tangu wakati ule wa kampeni mara moja ikahamia kwa John Magufuli. Haikuhamia kwa chama. Kama ilivyokuwa kwa CHADEMA kuwa ajenda ya mabadiliko iliondolewa kwa chama ikawekwa kwa mtu na ajenda ya vita dhidi ya ufisadi haikupelekwa kwa chama ikapelekwa kwa mtu. Watu hawa wawili – Lowassa akiwa CHADEMA na John Magufuli akiwa CCM waliamua kubeba ajenda ambazo hawakuwa nazo tangu awali; Lowassa hakuwa sehemu ya mabadiliko na Magufuli hakuwahi kuwa bingwa wa vita dhidi ya ufisadi. Mabadiliko ya watu hawa wawili yalibadilisha mwelekeo wa siasa za nchi; wapo wana CCM waliokuwa wanaamini katika Lowassa (kama walivyoimba wengine kule Dodoma) ambao waliamua kumfuata Lowassa “alipo wawepo”. Na upande mwingine wapo wana CHADEMA walioamini katika vita dhidi ya ufisadi kiasi kwamba hawakuwa tayari kubadilika na wakaamua kumuunga mkono Magufuli.

Magufuli aliposhinda urais – bila ya shaka kwa msaada mkubwa sana wa wapinga ufisadi – alikuja na ajenda ya kusafisha nchi na kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma. Aliingia akiwa mkali katika matumizi ya fedha za umma na madaraka kiasi kwamba kwa siku chache tu jina lake likatangazwa Afrika nzima (kama siyo duniani) kuwa Tanzania imepata mpiga vita ufisadi. Hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kama Lowassa angeweza kujipatia umaarufu wa namna ile; Lowassa mwenyewe katika kampeni yake hakujionesha kuwa anataka kuingia kuongoza vita dhidi ya ufisadi zaidi ya kutoa ahadi za kuwapa neema watu wa makundi mbalimbali!

Magufuli ameingia na gia ya kusafisha na kupanga upya serikali; kuleta nidhamu na uwajibikaji na kuona taifa linafanya kazi kweli kweli kama kweli tunataka kuendelea. Kosoa kosoa nyingi ambazo tunaziona hasa kutoka upinzani kubwa ni za kisiasa; ni zile zenye kujaribu kupata pointi za kisiasa. Tatizo la hili ni kuwa kama Magufuli atafanya anayoyaahidi – na tumeona ameanza – na wananchi wa kawaida yaani ‘wanyonge’ wakaona anatetea maslahi yao ni vigumu kuona ni jinsi gani upinzani unaweza kuimarika isipokuwa miongoni mwa wasomi (elites).

Hata masikini na wanyonge wanaoonekana wanashabikia upinzani watakapoona kuwa maslahi na mahitaji yao yanatimizwa chini ya Magufuli utafika wakati tutaona mikutano ya upinzani ikivutia wafanyakazi na watu ambao maslahi yao yamepotea sasa.

NI kwa sababu hiyo CHADEMA ni lazima ikae chini hasa sasa baada ya kumpata Katibu Mkuu mpya; ni lazima ijiulize kwa uwazi kabisa na ukweli (candidly) ni wapi walikosea, walikosea vipi na ni vipi wasahihishe makosa yao. Lakini pia ni lazima wajiulize ni kwa namna gani chini ya kiongozi maarufu kama Magufuli CHADEMA bado kinaweza kubakia chama makini na muhimu? Ni vipi maeneo yanayoongozwa na CHADEMA yanaweza kuwa mfano wa kiutawala na mafanikio? Je, kuendelea na maandamano ya kupinga au kushambulia tu ni mkakati mzuri? Haya ni maswali ambayo viongozi na wanachama wa CHADEMA wanapaswa kuyatafutia majibu.

Nje ya hapo ndoto ya kushika madaraka katika miaka kumi ijayo itaendelea kuwa ndoto ambayo waota ndoto yake hawaamki kwani wanaamini kuwa ndoto yao ni maisha ya kweli.

La Gazette
 
Hakika hapo kwenye kubadili gear angani hunichekesha sana..
 
Chadema? mmmmmmh! dhambi ya usaliti itawatafuna saaaana! Watabadili gia angani hadi gia zote ziishe! Yani hao jamaa nawaona bado kabisa. Kwa mwendo wao wa sasa, labda uwezo wangu wa kufikiri upungue saana, labda ndipo watanishawishi; tofauti na hapo wajipange saaaana!
 
Labda Magufuli aunde chama kipya ambacho sio CCM.

Kwa CCM hii, na aina ya watu wanaoiunda, bado Chadema wana nafasi kubwa sana. Hii CCM bado ni ile ile kama wanavyoimba wenyewe. Ni hadi tuone chaguzi zao wanaziendesha vipi, chama kinaisimamiaje serikali, n.k ndio tutasema sasa vyama vya upinzani vijipange.

Kama vile CCM walivyokuwa wakidai kuwa ajenda sio ufisadi pekee, vivyo hivyo leo inaweza kuelezwa kuwa ukiacha ajenda ya ufisadi ambayo Magufuli anapewa credit ya kuishughulikia ipasavyo, bado ana deni kubwa la kuijenga nchi katika maeneo mengi. Hata huu ufisadi, bado uko ktk ngazi ya juu na wahanga wengi wamekwa ni watendaji kama vile wakuu wa mashirika na vitengo vya serikali. Bado tunataka kuona wanasiasa wakubwa wakiguswa kwa mfano kashfa ya Escrow.

Hata Kikwete alianza kama mfalme kwa kupata 80% na ilifikia watu wakasema upinzani utakufa lakini tunajua alimalizaje. Kwa ujumla dunia haijawahi kuyachoka mabadiliko, na Biblia kitabu ninachokiamini sana, ilikwishamaliza kila kitu kwa kusema "Heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo wake"!
 
Back
Top Bottom