nashy
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 679
- 141
Chadema sasa kweli imeonesha ukomavu wake kisiasa, baada ya mmoja wa viongozi wake wa ngazi ya juu, Dokta W. Slaa kukiri kuwa sasa kazi ya kuishinda CCM ni ngumu.
Dk. Slaa amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na Viongozi wenzake katika kikao cha tathmini kilichofanyika katika eneo la wazi la Mini Market iliyo karibu na Rose View katika barabara ya Dik Dik, Leganga, katika mji wa USA RIVER, wilayani Arumeru, mkoani Arusha.
Baada ya kujiridhisha kuwa sasa ushindi haupo, katika kikao hicho, wameafikiana kwa pamoja kuanzisha siasa za uzushi katika mitandao na magazeti, mbalimbali nchini, huku wakiweka bajeti ya sh. Milioni 11, kwa ajili ya kazi ya kuvigiribu vyombo hivyo vya habari kuandika habari hizo. Mambo mengine ni pamoja na kumwagiza Ndg. Rwakatare kushirikiana kwa karibu na Mbunge wa Arusha Mjini kwa ajili ya kuandaa makundi ya vijana kutoka mkoani Kilimanjaro, na Arusha ili kujirundika siku ya kupiga kura na baada ya zoezi la kupiga kura, ili kufanya fujo zitakazowezesha matokeo kutotangzwa, na baadae kuvurugika kabisa.
Aidha wamekubaliana siku hiyo kuhakikisha kuwa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Meru, linapata misukosuko ya kutosha kupitia vijana wao hao.
Ungekuwa karibu ningekuzaba vibao, maana hata uongo hujui kusema mara amekomaa kisiasa, mara aandae makundi ya vurugu, unataka kuwaaminisha nini wasomaji wa thread yako? Anayewatuma mwambieni awapeleke shule kwanza walau mjue hizi propaganda vizuri. No consistency na unachokiandika. Go to hell with your ccm