GE2025 CHADEMA: Polisi wilaya ya Tarime na uhamiaji hawajui alipo John Heche, bado hajafikishwa kituoni hapo

GE2025 CHADEMA: Polisi wilaya ya Tarime na uhamiaji hawajui alipo John Heche, bado hajafikishwa kituoni hapo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo chadema kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kimesema kuwa wamefika katika kutuo cha Polisi Sirari ambapo hapo jana Jeshi la Polisi ilisema kuwa Heche amesafirishwa Kutoka Da es Salaam hadi hadi kituo hapo lakini mpaka leo Makamu mwenyekiti hajafikishwa kituoni hapo.

Pia Soma:
1761205354533.png

1761212961727.png

1761213016206.png
 
Duh nchi ilipofika nadhani vyama vya siasa vifutwe tu turudi chama kimoja maana kuna faida mtu ufe kisa kutofautiana political ideology?

Kuna ulazima gani kusema ni democratic Country na hatuwezi vumilia opposition.
 
Watakuwa wameshamuua na kumtupa pori la Katavi . Samia amechagua kutoka madarakani kwa njia ya fedheha kubwa. Damu hizi anazomwaga kamwe haziwezi kumuacha salama malipo yake yatakuwa hapahapa duniani.
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo chadema kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kimesema kuwa wamefika katika kutuo cha Polisi Sirari ambapo hapo jana Jeshi la Polisi ilisema kuwa Heche amesafirishwa Kutoka Da es Salaam hadi hadi kituo hapo lakini mpaka leo Makamu mwenyekiti hajafikishwa kituoni hapo.

Pia Soma:
View attachment 3492225
hawawezi sema alipo wanaogopa ile reaction ya watu wa kanda maalum!
 
Watakuwa wameshamuua na kumtupa pori la Katavi . Samia amechagua kutoka madarakani kwa njia ya fedheha kubwa. Damu hizi anazomwaga kamwe haziwezi kumuacha salama malipo yake yatakuwa hapahapa duniani.
Mawazo ya Kinyumbu
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo chadema kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kimesema kuwa wamefika katika kutuo cha Polisi Sirari ambapo hapo jana Jeshi la Polisi ilisema kuwa Heche amesafirishwa Kutoka Da es Salaam hadi hadi kituo hapo lakini mpaka leo Makamu mwenyekiti hajafikishwa kituoni hapo.

Pia Soma:
View attachment 3492225
Ridhiwani na Abdul wanaweza kuamuru auawe kwamba amekuwa msumbufu, toka Ridhiwani alipokabidhiwa hukumu la ‘kumuhifadhi’ Polepole ndiyo imeonekana jinsi alivyokamatia mambo yaliyo ya moto.
 
Habari ndo hiyo.. Hadi sasa Heche hajulikani alipo.

Pamoja na Jitahada za kumtafuta, hadi sasa hajapatikana...

Uhamiaji wanasema hawajui alipo, na Polisi Mkoa wa Mara wanasema hawajui alipo.

Jeshi la Polisi jana lilimkamata Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche katika Viunga vya Mahakama Dar na kumpeleka kituo cha Kati..

Polisi Tarime wamesema hakuna Kesi yoyote ya Heche wanayoichunguza

Lakini baadaye taarifa ikatoka kwamba amesafirishwa kwenda Mkoa Mara kwasababu ambazo hazijaelezwa.
 
Labda hawajafika wapo njiani embu tutumie masaa ya safari kwa bus tokea muda waliotoa taarifa
 
Tarime fanyeni kama juzi watamtoa walipomficha. Msisinzie wala msilale ingieni kazini kumtafuta Heche.

Chadema huwa hamsomi alama za nyakati. Mliacha vipi aende bila wakili?
 
Back
Top Bottom